Ni mkurugenzi au Commissioner? Hili sijui ni tatizo lako au la mwandishi.
Yote sawa Md,dg,ceo
Singasinga amepeleka madai mahakamani akitaka Mkurugenzi wa TRA akamatwe na kufunguliwa mashtaka na ikibidi afungwe jela miaka mingi sana. Hii imetokea baada ya Mkurugenzi huyo kukusudia kufuta hati ya mauzo ya hisa ya IPTL. Ndipo Singasinga akakimbilia mahakamani kuweka zuio; pamoja na kutaka bosi huyo wa TRA akamatwe mara moja.
Vyanzo: Mwananchi & Mtanzania.
MAONI YANGU
Tutasikia mengi mwaka huu. Tukumbuke kwamba Singasinga aliinunua IPTL kitapeli kwa kutumia nyaraka za kugushi. Ujinga huu unawezekana kwa Tanzania tu--kwamba tapeli na fisadi mkubwa anaweza kuja akatapeli na kuiba mabilioni ya fedha za umma halafu akaiweka serikali mfukoni mwake.
Baba Nyerere uone watawala uliowaacha wanavyotishwa na mafisadi.
:israel:
Exactly na mimi pia lately nimekuwa nikikumbuka tukio la yule Mgiriki aliyeiambia serikali ya Nyerere kwamba ameiweka mfukoni. Yani ndio exactly walichofanya Rugemalila na Singasinga, wamemwaga mpunga kwa kila waliyedhani ataleta kokolo, kuanzia makatibu wa Rais mpaka makarani wa benki, daaaaah, inasikitisha.Namkumbuka sana Nyerere na ile kauli yake ya tajiri moja kuweka serikali mfukoni, ndio haya ya huyu Singasinga wakuu.
Hata ingekua mahakama ya the hague,mahakamani hakunaga siasa,kama hamkujiandaa vyema singasinga lazima awaache keepleft.
Bosi wa IPTL anakuwa na kibuli kiasi cha kumdharau mkuu wa taasisi ya umma kiasi hiki, Mawaziri na makatibu wanakuwa na kiburi hata kukataa kujiuzuru wakidai mkuu wao ndiye anajua walichokuwa wanafanya na ndiye aweza kuwafukuza!
Je, kuna nini hapa na ni nani kinawapa watu hawa hii jeuri!?