IPTL yazua Kizaazaa Mahakamani

IPTL yazua Kizaazaa Mahakamani

Huu upuuzi unaweza fanyika katika nchi ya tanzania tuu

huyu mpuuzi angefanya upuuzi wake huu kwa nchi makini kama China, leo hii asingekuwa na kichwa chake...kingekwisha kuwa halali ya serikali. natamani wananchi tuasi tuwapige na kuwaua mafisadi na matapeli wote katika nchi hii...tumechoka!
 
Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa serikali hii.........kama ulivyosema hata mimi i guess so huyu jamaa ana mkono mrefu sana.......Bade asipoangalia atangolewa TRA

Hakuna unachojua kwa tarifa yako BDE siyo msafi hata kidogo anafanya hivyo kwa maelekezo ya mtu mmoja anaitwa ......Azizi ambaye anataka PAP waondoke yeye alete kampuni yake ya simbioni power ila kama huyajuai haya mambo utahangaika sana.
 
Singa singa alishausoma uwezo na ulafi wa viongozi wa tanzaina siku nyingi, wote kawaweka mfukoni, mkuu wa nchi yupo kimya tangu hii kashfa iibuliwe. Kwa nchi makini wote wahusika wangekalishwa pembeni kupisha uchunguzi kama kasfa zinawahusu au hapana., lakini yeye kimya na wauhumiwa wanapisha air port kwenda kupumzika nchi za watu na kuweka vyema maswala yao, halafu unasema unaongoza nchi. Nchi inaongozwa na matapeli na wezi ikulu ni rubber stamp tu.

ni bora nchi hii iongozwe na MAITI kuliko kuongozwa na binadamu. sijamsikia rais akilisemea hili ktk mazungumzo yake ya kila mwezi. singasinga ameiweka nchi na maisha ya watanzania milioni 50 mfukoni mwake.
 
Nilipo ona kuwa boss wa IPTL kasema mkurugenzi wa TRA akamatwe mara moja machozi yalinitoka! Ila baada ya kuoma ameenda mahakamani nikajipa tumaini kuwa hata ikitoka hukumu ya kukamatwa, itakuwa imetolewa na sehemu sahihi,maana kwa upeo wangu mkurugenzi wa TRA ni mteule wa Rais, mtu binafsi kutoa agizo la kumukamata, maana yake ni kuwa wewe una nguvu kuliko Rais,Mungu Inusuru Tanzania

Ile kuagiza tu Akamatwe ni km kuifundisha kazi mahakama (kosa) ila tu mahakama ingeona kuna haja ya kumuita mkurugenzi wa TRA ingetuma samans...huyu singaSinga ananifikirisha hata mm nisiekuwa na digree Anatoa wapi jeuri ya kumtisha mtu alieaminiwa na mh Rais?
 
Hakuna unachojua kwa tarifa yako BDE siyo msafi hata kidogo anafanya hivyo kwa maelekezo ya mtu mmoja anaitwa ......Azizi ambaye anataka PAP waondoke yeye alete kampuni yake ya simbioni power ila kama huyajuai haya mambo utahangaika sana.

sasa kama wewe unayajua si uyaweke hapa jukwaani? hii nchi inatopea kwenye mduara wa UFISADI.
 
Mleta mada wacha uchochezi hakuna kitu kama hicho
 
kuna kitu yule msanii pale magogoni anapanga, nyie subirini
 
Kama ana haki atashinda kesi. Hakuna haja ya kuanza kutoa hukumu nje ya mahakama!

"Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu."

- Harrison Mwakyembe
 
Inakuqje walioibiwa wanaogopa kwenda mahakamani
 
Kuna RFK yangu mmoja alisema kama kikwete atapata urais Taifa litajuta wala halitamsahau Leo ndio naamini yaani kiongozi mwenye maamuzi ya mwisho kitaifa abanyamaza kana keamba iptl na escrow ni hela iliyotakiwa kununua chumvi kwenye familia moja hivi so keamba hawawezi kosa chumvi kwa jirani
 
Tulifanya makosa makubwa kuacha chama tawala kikawekwa mifukoni mwa wafanyabiashara, hali hiyo imesababisha serikali iwe ilivyo sasa (kama imewekwa mifukoni au la, fanya utafiti mwenyewe), mahakama nazo???, Bunge!

Kuokoa jahazi ni lazima kuondoa chama tawala kwa wafanya biashara! Akili ya kibiashara inatafuta faida popote pale, hakuna faida hakuna biashara! Wanasiasa wafanya biashara lazima watumie nafasi zao kwa maslahi binafsi, hawawezi hata siku moja kuwasaidia walalahoi, vinginevyo hawatakuwa wafanyabiashara!
Bahati mbaya sana viongozi wa juu na washauri wao hawalioni hili (labda nao ni wafanya biashara)!
 
KARA SINGHA anajua riz1 ndio alichukua pesa kwa kwa sandarusi sasa mtamfilisi vip? anzeni kumfilisi prince riz1
 
Namkumbuka sana Nyerere na ile kauli yake ya tajiri moja kuweka serikali mfukoni, ndio haya ya huyu Singasinga wakuu. Huyu jamaa anatoa kiburi wapi?. Nani yuko nyuma yake?. kwa nini anachezea serikali kiasi hichi?.

Anatoa funzo gani kwa wananchi wanaoamini serikali yao?. vyombo vya dola mko wapi?. serikali mbona mnadhalilishwa na huyu jamabzi?. Inasikitisha sana aisee

haya ndiyo matatizo ya kuwa na viongozi wasiokuwa na maamuzi, tamaa, chokambaya,uwezo mdogo wa kuchambua mambo, sasa nchi inasambaratika.
 
Setti_iptl.jpg


Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi




Posted Ijumaa,Decemba5 2014 saa 9:11 AM



Yaomba kamishna wa TRA akamatwe kwa kukusudia kufuta hati za Malipo ya Kodi ya Mauzo ya Hisa









Dar es Salaam. Kampuni za Pan Africa Power Solution Tanzania Limited (PAP) na Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), zimewasilisha maombi ya kutaka Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) akamatwe kwa kukiuka amri ya Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB) kwa kufuta Hati za Malipo ya Kodi za Mauzo ya Hisa (Capital Gain Certificate).


Kampuni hizo mbili, ambazo ziko kwenye mgogoro wa umiliki, ndizo zinahusika kwenye sakata la uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya kuuza umeme unaofuliwa na IPTL, kwa Shirika la Umeme (Tanesco), wakati wa kusubiri uamuzi wa mahakama katika kesi ya kupinga tozo hilo.



PAP, ambayo inadai imenunua hisa zote za IPTL, ndiyo iliyolipwa fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti hiyo na kuamsha mjadala mkubwa bungeni ulioisha kwa Bunge kufikia uamuzi wa kuwawajibisha kisheria wote waliohusika, wakiwemo mawaziri.



Lakini uamuzi huo wa Bunge haukuwa tamati la sakata hilo baada ya kampuni hizo mbili kukata rufaa TRAB dhidi ya Kamishna wa TRA na Msajili wa Kampuni na Leseni (Brela) zikipinga kusudio la kufuta hati hizo.

Jana kampuni hizo mbili ziliwasilisha maombi ya hati ya kutaka Kamishna Mkuu wa TRA akamatwe, zikidai kuwa amepuuza amri hiyo iliyomzuia kutekeleza azma yake ya kufuta Hati za Malipo ya Kodi ya Mauzo ya Hisa.



Katika maombi hayo walalamikaji hao wanadai kuwa licha ya TRAB kutoa zuio hilo Novemba 26, 2014, Kamishna Mkuu wa TRA, ambaye ni mlalamikiwa wa kwanza, alitoa amri ya kuziondoa hati hizo siku iliyofuata, yaani Novemba 27, 2014, bila kujali amri hiyo.



Walalamikaji hao pia wanaiomba TRAB, baada ya kumkamata Kamishna Mkuu wa TRA, itoe amri afungwe kwa kudharau amri halali iliyotolewa na bodi na pia imwamuru akidhi matakwa ya amri ya TRAB ya Novemba 26.

Pia walalamikaji hao wanaiomba TRAB imwamuru mlalamikiwa huyo, kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo pamoja na amri nyingine ambazo itaona kuwa zinafaa.



Maombi hayo ya PAP na IPTL ya hati ya kumkamata na kuamuru Kamishna Mkuu wa TRA afungwe yamepangwa kusikilizwa leo na Katibu wa TRAB, Respicius Mwijage.

Hati ya kiapo inayounga mkono maombi hayo inaeleza kuwa mlalamikiwa, akiwa ni raia wa Tanzania, siyo tu kwamba alipaswa kuwa mtiifu kwa mamlaka ya bodi hiyo, bali pia alipaswa kutekeleza sheria za nchi ambazo bodi hiyo ni sehemu yake.



Hati hiyo ya kiapo ya mkurugenzi wa operesheni wa IPTL, Parthiban Chandrasakaran, inaeleza kuwa kwa kitendo hicho cha kutotii amri ya bodi hiyo, mlalamikiwa amepoteza sifa ya kuwa mtumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia inaelea kuwa kama bodi hiyo isipotumia mamlaka yake kukubali maombi hayo ya kutoa amri inayoombwa, basi walalamikaji watapata hasara isiyoweza kufidiwa.


Inafafanua hasara hizo kuwa ni pamoja na kodi nyingine ambazo tayari PAP wamelipa TRA kwa ajili ya kuendesha biashara.

Pia hati hiyo ya kiapo inafafanua kuwa kuondolewa kwa hati hizo kutahatarisha biashara ya walalamikaji ambayo wamekuwa wakiiendesha tangu walipota hati hizo.



Inaendelea kueleza kuwa kwa kuwa walalamikaji wako katika hatari ya kuvunja mkataba na Shirika la Umeme (Tanesco), na wadau wengine, jambo hilo litasabaisha vita ya kimahakama na hivyo kulipa fidia zisizo za msingi.

Hati hizo namba 004965600 na 0049657 zilitolewa na TRA Desemba 23, 2013, kwa ajili ya uuzaji wa hisa baina ya kampuni ya Mechmar Corporation (Malaysia) Berhard iliyokuwa ikimiliki asilimia 70 ya hisa za IPTL na Piper Links Investment Limited na kati ya Piper Link na PAP.



Hata hivyo baadaye, Novemba 19, 2014 TRA ilitoa taarifa ya siku sita kwa Brela ikionyesha kusudio la kuziondoa hati hizo kwa madai kuwa mkataba wa madai ya mauzo ya hisa hizo ulikuwa ni mkataba wa makubaliano ya uongo.



DSC_4693.JPG


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Wakati Huohuo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kitendo cha kushindwa kuwachukulia hatua wanaotuhumiwa kuchota Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow hadi sasa, ni ishara ya kuwa na Serikali dhaifu.


Mbowe, ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema viongozi waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo walitakiwa wawekwe kando kabla ya hatua zaidi.



“Leo (jana) ni siku ya tano na Rais Kikwete ameshindwa kutoa uamuzi wowote. Hii inaonyesha jinsi tulivyo na Serikali dhaifu,” alisema Mbowe wakati akihutubia mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Kata ya Vijibweni, Kigamboni.

“Hadi leo Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka bado yupo ofisini na anasaini nyaraka mbalimbali za viwanja. Inakuwaje hadi leo wezi bado wapo ofisini?”

, kwanini wanalindwa?” alihoji.



“Wanapewa muda wa kukaa ofisini kujipanga ili hata Rais Kikwete atakapochukua uamuzi, wawe wamejipanga na kuchukua kidogo kilichokuwepo.”

Mbowe alisema sakata la Escrow lilitikisa nchi na kwamba kitendo cha watuhumiwa kutochukuliwa hatua hadi leo tafsiri yake ni kwamba viongozi wa Serikali wanalindana.

Chanzo Mwananchi
 
Kuna msemo wa Kiarabu " wezi wanapoanza kuzozana, mali iliyoibiwa itajulikana"
 
Tulifanya makosa makubwa kuacha chama tawala kikawekwa mifukoni mwa wafanyabiashara, hali hiyo imesababisha serikali iwe ilivyo sasa (kama imewekwa mifukoni au la, fanya utafiti mwenyewe), mahakama nazo???, Bunge!

Kuokoa jahazi ni lazima kuondoa chama tawala kwa wafanya biashara! Akili ya kibiashara inatafuta faida popote pale, hakuna faida hakuna biashara! Wanasiasa wafanya biashara lazima watumie nafasi zao kwa maslahi binafsi, hawawezi hata siku moja kuwasaidia walalahoi, vinginevyo hawatakuwa wafanyabiashara!
Bahati mbaya sana viongozi wa juu na washauri wao hawalioni hili (labda nao ni wafanya biashara)!
 
Tuache Uoga! Tumekuwa tukikuelezeni uhuni wakinaZitto hamuelewi sasa ndio wakati wa kuumbuka wanasiasa Muflisi. Nyie mmetishia kumpeleka amahakamani sasa yeye tayari yupo huko anawasubiri
 
Tuache Uoga! Tumekuwa tukikuelezeni uhuni wakina Zitto hamuelewi sasa ndio wakati wa kuumbuka wanasiasa Muflisi. Nyie mmetishia kumpeleka amahakamani sasa yeye tayari yupo huko anawasubiri

Hili swala la IPTL sio la kisiasa limejaa mambo mengi ya kisheria za nchi na za kimataifa.Wabunge walikosea mno kulipeleka kisiasa.Mahakama ilikuwa sahihi kabisa hata kulikataza lisiongelee hii kesi sababu walijua wabunge watazidi tu kulikoroga hilo swala.

Watanzania tusipozingatia sheria hasa kwenye mambo ya biashara tutalipa mifaini ma fidia mpaka tukome

Bunge limezua makesi mengine yasiyo na kichwa wala miguu kupitia maazimio yao sababu ya ubishi .

Ushauri kwa watendaji wengine wazingatie sheria wasiburuzwe na mihemuko ya kisiasa kuepuka kupata misuko suko
 
Hivi huyu Singasinga ni nani hadi aitetemeshe serikali kiasi hiki? Serikali ni kama imekufa na imewekwa mfukoni mwa Singasinga. Kwanini wananchi tusiasi na kujichukulia sheria mikononi? Tuwawinde na kuwaua mafisadi wote ktk nchi hii akiwemo Singasinga. Inauma sana!
 
Back
Top Bottom