IPTL yazua Kizaazaa Mahakamani

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,830
2,000
Dar es Salaam. Kampuni za Pan Africa Power Solution Tanzania Limited (PAP) na Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), zimewasilisha maombi ya kutaka Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) akamatwe kwa kukiuka amri ya Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB) kwa kufuta Hati za Malipo ya Kodi za Mauzo ya Hisa (Capital Gain Certificate).

Kampuni hizo mbili, ambazo ziko kwenye mgogoro wa umiliki, ndizo zinahusika kwenye sakata la uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya kuuza umeme unaofuliwa na IPTL, kwa Shirika la Umeme (Tanesco), wakati wa kusubiri uamuzi wa mahakama katika kesi ya kupinga tozo hilo.

PAP, ambayo inadai imenunua hisa zote za IPTL, ndiyo iliyolipwa fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti hiyo na kuamsha mjadala mkubwa bungeni ulioisha kwa Bunge kufikia uamuzi wa kuwawajibisha kisheria wote waliohusika, wakiwemo mawaziri.

Lakini uamuzi huo wa Bunge haukuwa tamati la sakata hilo baada ya kampuni hizo mbili kukata rufaa TRAB dhidi ya Kamishna wa TRA na Msajili wa Kampuni na Leseni (Brela) zikipinga kusudio la kufuta hati hizo.

Jana kampuni hizo mbili ziliwasilisha maombi ya hati ya kutaka Kamishna Mkuu wa TRA akamatwe, zikidai kuwa amepuuza amri hiyo iliyomzuia kutekeleza azma yake ya kufuta Hati za Malipo ya Kodi ya Mauzo ya Hisa.

Katika maombi hayo walalamikaji hao wanadai kuwa licha ya TRAB kutoa zuio hilo Novemba 26, 2014, Kamishna Mkuu wa TRA, ambaye ni mlalamikiwa wa kwanza, alitoa amri ya kuziondoa hati hizo siku iliyofuata, yaani Novemba 27, 2014, bila kujali amri hiyo.

Walalamikaji hao pia wanaiomba TRAB, baada ya kumkamata Kamishna Mkuu wa TRA, itoe amri afungwe kwa kudharau amri halali iliyotolewa na bodi na pia imwamuru akidhi matakwa ya amri ya TRAB ya Novemba 26.

Pia walalamikaji hao wanaiomba TRAB imwamuru mlalamikiwa huyo, kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo pamoja na amri nyingine ambazo itaona kuwa zinafaa.

Maombi hayo ya PAP na IPTL ya hati ya kumkamata na kuamuru Kamishna Mkuu wa TRA afungwe yamepangwa kusikilizwa leo na Katibu wa TRAB, Respicius Mwijage.

Hati ya kiapo inayounga mkono maombi hayo inaeleza kuwa mlalamikiwa, akiwa ni raia wa Tanzania, siyo tu kwamba alipaswa kuwa mtiifu kwa mamlaka ya bodi hiyo, bali pia alipaswa kutekeleza sheria za nchi ambazo bodi hiyo ni sehemu yake.

Hati hiyo ya kiapo ya mkurugenzi wa operesheni wa IPTL, Parthiban Chandrasakaran, inaeleza kuwa kwa kitendo hicho cha kutotii amri ya bodi hiyo, mlalamikiwa amepoteza sifa ya kuwa mtumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia inaelea kuwa kama bodi hiyo isipotumia mamlaka yake kukubali maombi hayo ya kutoa amri inayoombwa, basi walalamikaji watapata hasara isiyoweza kufidiwa.

Inafafanua hasara hizo kuwa ni pamoja na kodi nyingine ambazo tayari PAP wamelipa TRA kwa ajili ya kuendesha biashara.

Pia hati hiyo ya kiapo inafafanua kuwa kuondolewa kwa hati hizo kutahatarisha biashara ya walalamikaji ambayo wamekuwa wakiiendesha tangu walipota hati hizo.

Inaendelea kueleza kuwa kwa kuwa walalamikaji wako katika hatari ya kuvunja mkataba na Shirika la Umeme (Tanesco), na wadau wengine, jambo hilo litasabaisha vita ya kimahakama na hivyo kulipa fidia zisizo za msingi.

Hati hizo namba 004965600 na 0049657 zilitolewa na TRA Desemba 23, 2013, kwa ajili ya uuzaji wa hisa baina ya kampuni ya Mechmar Corporation (Malaysia) Berhard iliyokuwa ikimiliki asilimia 70 ya hisa za IPTL na Piper Links Investment Limited na kati ya Piper Link na PAP.

Hata hivyo baadaye, Novemba 19, 2014 TRA ilitoa taarifa ya siku sita kwa Brela ikionyesha kusudio la kuziondoa hati hizo kwa madai kuwa mkataba wa madai ya mauzo ya hisa hizo ulikuwa ni mkataba wa makubaliano ya uongo.

Wakati Huohuo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kitendo cha kushindwa kuwachukulia hatua wanaotuhumiwa kuchota Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow hadi sasa, ni ishara ya kuwa na Serikali dhaifu.

Mbowe, ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema viongozi waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo walitakiwa wawekwe kando kabla ya hatua zaidi.

"Leo (jana) ni siku ya tano na Rais Kikwete ameshindwa kutoa uamuzi wowote. Hii inaonyesha jinsi tulivyo na Serikali dhaifu," alisema Mbowe wakati akihutubia mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Kata ya Vijibweni, Kigamboni.

"Hadi leo Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka bado yupo ofisini na anasaini nyaraka mbalimbali za viwanja. Inakuwaje hadi leo wezi bado wapo ofisini?"

, kwanini wanalindwa?" alihoji.

"Wanapewa muda wa kukaa ofisini kujipanga ili hata Rais Kikwete atakapochukua uamuzi, wawe wamejipanga na kuchukua kidogo kilichokuwepo."

Mbowe alisema sakata la Escrow lilitikisa nchi na kwamba kitendo cha watuhumiwa kutochukuliwa hatua hadi leo tafsiri yake ni kwamba viongozi wa Serikali wanalindana.

Chanzo:Mwananchi


MAONI YANGU
Tutasikia mengi mwaka huu. Tukumbuke kwamba Singasinga aliinunua IPTL kitapeli kwa kutumia nyaraka za kugushi. Ujinga huu unawezekana kwa Tanzania tu--kwamba tapeli na fisadi mkubwa anaweza kuja akatapeli na kuiba mabilioni ya fedha za umma halafu akaiweka serikali mfukoni mwake.

Baba Nyerere fufuka uone watawala uliowaacha wanavyotishwa na mafisadi.
:israel:
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
15,230
2,000
Kama ana haki atashinda kesi. Hakuna haja ya kuanza kutoa hukumu nje ya mahakama!
 

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,943
1,225
Singasinga amepeleka madai mahakamani akitaka Mkurugenzi wa TRA akamatwe na kufunguliwa mashtaka na ikibidi afungwe jela miaka mingi sana. Hii imetokea baada ya Mkurugenzi huyo kukusudia kufuta hati ya mauzo ya hisa ya IPTL. Ndipo Singasinga akakimbilia mahakamani kuweka zuio; pamoja na kutaka bosi huyo wa TRA akamatwe mara moja.

Vyanzo: Mwananchi & Mtanzania.

MAONI YANGU
Tutasikia mengi mwaka huu. Ujinga huu unawezekana kwa Tanzania tu--kwamba tapeli na fisadi anaweza kuja akatapeli na kuiba mabilioni ya fedha za umma halafu akaiweka serikali yake. Baba Nyerere uone watawala uliowaacha wanavyotishwa na mafisadi.
:israel:
Namkumbuka sana Nyerere na ile kauli yake ya tajiri moja kuweka serikali mfukoni, ndio haya ya huyu Singasinga wakuu. Huyu jamaa anatoa kiburi wapi?. Nani yuko nyuma yake?. kwa nini anachezea serikali kiasi hichi?.

Anatoa funzo gani kwa wananchi wanaoamini serikali yao?. vyombo vya dola mko wapi?. serikali mbona mnadhalilishwa na huyu jamabzi?. Inasikitisha sana aisee
 

MUSONI

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
890
1,000
Haya yote yanatokea kwa kutokuwa wazi katika haya maswala na maeneo mengine mengi....huko kwingine kwenye hisa za mwanzo mbona hakuzungunziwi....MERCHMA...nk.....
 

Nanu

JF-Expert Member
May 29, 2009
1,224
1,195
Ukichelewa kuchukua hatua dhidi ya mtuhumiwa yeye anachukua hatua.
Kwa hili tu la nyaraka kughushiwa na akaunti kufunguliwa ndivyo sivyo basi hatua ilikuwa muhimu kuchukuliwa. Labda kama taarifa au ripoti na mapendekezo ya bunge yalikuwa porojo tu.
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,830
2,000
Namkumbuka sana Nyerere na ile kauli yake ya tajiri moja kuweka serikali mfukoni, ndio haya ya huyu Singasinga wakuu. Huyu jamaa anatoa kiburi wapi?. Nani yuko nyuma yake?. kwa nini anachezea serikali kiasi hichi?. Anatoa funzo gani kwa wananchi wanaoamini serikali yao?. vyombo vya dola mko wapi?. serikali mbona mnadhalilishwa na huyu jamabzi?. Inasikitisha sana aisee

Mkuu ocampo four inauma sana. natamani Nyerere afufuke leo aone serikali inavyowekwa mfukoni na matapeli. huyu Singasinga sio bure...kutakuwa na mtu nyuma yake na unaweza ukute mkuu wa Magogoni ndiye anayempa jeuri hii!
 

google2014

JF-Expert Member
Sep 1, 2014
585
0
Singasinga amepeleka madai mahakamani akitaka Mkurugenzi wa TRA akamatwe na kufunguliwa mashtaka na ikibidi afungwe jela miaka mingi sana. Hii imetokea baada ya Mkurugenzi huyo kukusudia kufuta hati ya mauzo ya hisa ya IPTL. Ndipo Singasinga akakimbilia mahakamani kuweka zuio; pamoja na kutaka bosi huyo wa TRA akamatwe mara moja.

Vyanzo: Mwananchi & Mtanzania.

MAONI YANGU
Tutasikia mengi mwaka huu. Tukumbuke kwamba Singasinga aliinunua IPTL kitapeli kwa kutumia nyaraka za kugushi. Ujinga huu unawezekana kwa Tanzania tu--kwamba tapeli na fisadi mkubwa anaweza kuja akatapeli na kuiba mabilioni ya fedha za umma halafu akaiweka serikali mfukoni mwake. Baba Nyerere uone watawala uliowaacha wanavyotishwa na mafisadi.
:israel:

Huyu jamaa anatoa matamko tu kwa kutumia wanasheria wake huku yeye kakimbia nchi kwa kuhofia kuwekwa ndani.
 

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,943
1,225
mkuu ocampo four inauma sana. natamani Nyerere afufuke leo aone serikali inavyowekwa mfukoni na matapeli. huyu Singasinga sio bure...kutakuwa na mtu nyuma yake na unaweza ukute mkuu wa Magogoni ndiye anayempa jeuri hii!
Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa serikali hii.........kama ulivyosema hata mimi i guess so huyu jamaa ana mkono mrefu sana.......Bade asipoangalia atangolewa TRA
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,830
2,000
Ukichelewa kuchukua hatua dhidi ya mtuhumiwa yeye anachukua hatua.
Kwa hili tu la nyaraka kughushiwa na akaunti kufunguliwa ndivyo sivyo basi hatua ilikuwa muhimu kuchukuliwa. Labda kama taarifa au ripoti na mapendekezo ya bunge yalikuwa porojo tu.

Singasinga anajua fika kwamba mahakama za Tanzania zinanuka rushwa, so anakimbilia huko akiwa na uhakika kushinda kesi kwa nguvu ya vijisenti alivyo navyo.

Hii yote imetokea baada ya kuwahonga wabunge kumtetea bungeni. kama mapendekezo ya kamati ya Zitto yangebaki kama yalivyokuwa yamependekezwa na kamati (bila kufanyiwa FOMULESHENI) bila shaka huyu Singasinga angekuwa ndani leo hii na asingepata jeuri ya kuitingisha serikali ya CCM.
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,223
2,000
Bosi wa IPTL anakuwa na kibuli kiasi cha kumdharau mkuu wa taasisi ya umma kiasi hiki, Mawaziri na makatibu wanakuwa na kiburi hata kukataa kujiuzuru wakidai mkuu wao ndiye anajua walichokuwa wanafanya na ndiye aweza kuwafukuza!

Je, kuna nini hapa na ni nani kinawapa watu hawa hii jeuri!?
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,565
2,000
Hata ingekua mahakama ya the hague,mahakamani hakunaga siasa,kama hamkujiandaa vyema singasinga lazima awaache keepleft.
 

manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,533
2,000
Namkumbuka sana Nyerere na ile kauli yake ya tajiri moja kuweka serikali mfukoni, ndio haya ya huyu Singasinga wakuu. Huyu jamaa anatoa kiburi wapi?. Nani yuko nyuma yake?. kwa nini anachezea serikali kiasi hichi?. Anatoa funzo gani kwa wananchi wanaoamini serikali yao?. vyombo vya dola mko wapi?. serikali mbona mnadhalilishwa na huyu jamabzi?. Inasikitisha sana aisee
Nyuma yake atakuwapo mbia mwenzie SIMBA mla watu.
 

SaidSabke

JF-Expert Member
Sep 28, 2006
2,071
1,500
mkuu ocampo four inauma sana. natamani Nyerere afufuke leo aone serikali inavyowekwa mfukoni na matapeli. huyu Singasinga sio bure...kutakuwa na mtu nyuma yake na unaweza ukute mkuu wa Magogoni ndiye anayempa jeuri hii!

Hata akifufuka hawezi kufanya kitu kwa sababu misingi ya democrasia na utawala bora tumejiwekea sisi misingi ya dikteta wakati wa mwalimu umepita kaka acha ndoto za alinacha.
 
Last edited by a moderator:

leipzig

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
2,769
2,000
Singasinga anajua fika kwamba mahakama za Tanzania zinanuka rushwa, so anakimbilia huko akiwa na uhakika kushinda kesi kwa nguvu ya vijisenti alivyo navyo. hii yote imetokea baada ya kuwahonga wabunge kumtetea bungeni. kama mapendekezo ya kamati ya Zitto yangebaki kama yalivyokuwa yamependekezwa na kamati (bila kufanyiwa FOMULESHENI) bila shaka huyu Singasinga angekuwa ndani leo hii na asingepata jeuri ya kuitingisha serikali ya CCM.

Wezi wa kuku wangetengenezewa FOMULESHENI mbona ingekuwa powa!
 
Last edited by a moderator:

Morinyo

JF-Expert Member
Aug 26, 2011
2,795
2,000
Singasinga amepeleka madai mahakamani akitaka Mkurugenzi wa TRA akamatwe na kufunguliwa mashtaka na ikibidi afungwe jela miaka mingi sana. Hii imetokea baada ya Mkurugenzi huyo kukusudia kufuta hati ya mauzo ya hisa ya IPTL. Ndipo Singasinga akakimbilia mahakamani kuweka zuio; pamoja na kutaka bosi huyo wa TRA akamatwe mara moja.

Vyanzo: Mwananchi & Mtanzania.

MAONI YANGU
Tutasikia mengi mwaka huu. Tukumbuke kwamba Singasinga aliinunua IPTL kitapeli kwa kutumia nyaraka za kugushi. Ujinga huu unawezekana kwa Tanzania tu--kwamba tapeli na fisadi mkubwa anaweza kuja akatapeli na kuiba mabilioni ya fedha za umma halafu akaiweka serikali mfukoni mwake. Baba Nyerere uone watawala uliowaacha wanavyotishwa na mafisadi.
:israel:

Ni mkurugenzi au Commissioner? Hili sijui ni tatizo lako au la mwandishi.
 

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
7,142
2,000
Katiaka hali takawaida iliatakiwa huyu jamaa awe amesha kamatwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom