IPTL yazua Kizaazaa Mahakamani

Ukimchekea nyani shambani utavuna mabua,jamaa anajua kabisa kwanza kagushi,pia katoa fedha isivyo halali,hajalipa kodi ,sasa kweli naamini maneno ya Mwl Nyerere kuhusu mambo ya rushwa,si ajabu huyu jamaa huko aliko hutamba kuwa ''kaiweka mfukoni serikali''sasa kwa kiburi anataka mteule wa raisi tena mwenye dhamana nyeti afungwe,hapo ndipo tulipofikia ndia kwani watamfanya nini.
 
Kama ana haki atashinda kesi. Hakuna haja ya kuanza kutoa hukumu nje ya mahakama!
wewe vipi? tangu lini mahakama zetu zikatoa haki? wewe hakimu anaitwa dakika tatu! ukiwa na pesa hakimu anakupa ushindi ndani ya dakika tatu! nchi hii haina haki!
 
Singasinga yupo nje. Wanaojiita wasomi sana watz wanatoa matamko na kwenda mahakamani kumtetea tapeli na mwizi. Usafi wa hawa wasomi sana upo wapi. Mmoja si ndo alikuwa brela akafanikisha dili halafu akahamia iptl?
 
Kwa hali hii, ipo siku Singasinga ataingia IKULU na kudai ni mali yake. Nchi hii na viongozi wake ni sawa na MAITI anayetembea.
 
Mtu si mhalifu mpaka ibainike kisheria kwa ushahidi madhubuti - kwa hiyo ana haki ya kupeleka malamiko yake mahakamani. Hilo suala la kama mahakama zinafaa au hazifai halina maana sababu mahakama ndio mahali pekee nchini panatambuliwa kusikiliza malalamio na kutoa maamuzi ya kisheria.

Assumpta umeanza? Hivi unalipwa sh ngapi kutetea WEZI?
 
Ndio maana nchi kama China huwa inapiga risasi mafisadi wote kama hao ili kusiwepo hata na mtu atayejifanya anakwenda sijui mahakamani n.k
 
Uwafute kazi kwa kosa lipo? Kwa kuwa wewe unataka? Au Mengi?


Wanafutwa kazi kwa sababu ni criminals na appointing authority anaogopa kuwafukuza kwani yeye akiwamwagia mboga na wao watamwaga ugali!!! Upo hapo we shori la buku 7?
 
MDA SI MREFU ATASEMA SPIKA NAE AWEKWE NDANI,SABABU AMEKUBAli kumjadili bungeni

Mbona alishasema,aseme mara ngapi?Alipoweka pingamizi la Bunge lisijadili,aliwataka SUPIKA wetu awekwe kwa jela maana hakutii sheriaya Hakimu aliyepokea pesa za Escrow.Acha kabisa,singasinga anajeuri kuliko.Amebakiza kumplekea summons Prof wa Kichina tu,nadhani anasubiria tu akiwafukuza kazi washirika lazima apeleke kesi mahakamani ya kumfunga Rais.

Nyerere aliyasema haya leo tunayaona kwa macho yetu,siyo serikali imewekwa mfukoni kwa Singasinga nadhani imewekwa kwa CHUPI ya Singasinga.

Yaani haiwezekani muwekezaji awe na nguvu kuliko serikali duh!Sijui TISS na JWTZ wanaionaje hili,siwezi kuwasemea maana SAFARI moja huanzisha nyingine
 
Back
Top Bottom