Ipo siku Rais Samia atamchoka Mdude

Ipo siku Rais Samia atamchoka Mdude

Sitaki kukaa upande wa maamuzi yatayochukuliwa; ila nataka nikae upande wa sisi tunaosoma post za ndugu Mdude;

Kwanini hana uwezo au hataki kutumia lugha yenye staha?

Je akitumia lugha yenye staha kuna mtu atashtushwa na post zake? Nani atashtuka ukiandika kuwa kuna wizi umefanywa na maafisa wa serikali katika taasisi fulani? Hizi ni habari za kila mwaka; ripoti ya CAG huwa inakuja kutukumbusha tu kinachotokea.

Maana wengi wanaongea juu ya mambo yanayofanana na haya ambayo Mdude anayaandika kwa lugha ya staha, na wala huoni raia wakishughulika na post za namna hiyo.

Mdude sio mwanasiasa japo anazunguka kwenye siasa; namna pekee ya yeye kuwa relevant katika sehemu ambayo hastahili kuwepo ni kuwa na controversial posts za namna hii.

Kwa historia ya kilichompata Mdude; kufungwa na kuteswa (kwa mujibu wake) naona kabisa katika mazingira ya sasa ya kisiasa, serikali itajizuia sana kushughulika na Mdude moja kwa moja, badala yake kupitia mlango wa uwani(back-door); CHADEMA italazimika aidha kumyamzisha Mdude ama kumtaka kufanya siasa na sio anachofanya sasa.

Inawezekana Mdude kama atabaki kwenye siasa haitakuwa ndani ya CHADEMA, maridhiano na utengamano wa kisiasa hautoi nafasi tena kwa harakati za Mdude.

Ni suala la muda tu anapoteza relevance kwenye mazingira haya ya sasa.
 
tatizo chawa hampendi mtu wenu asemwe

alivyokuwa anafanya awamu ya tano akachukuliwa hatua mlisema kaonewa,sasa anawaambia ukweli hamtaki kuusikia binafsi sijaona ubaya wowote alioandika hapo kasema UKWELI
 
nyie ndio wezi wa mali za umma
Umeniambaatanisha vipi na hao wezi? Una uhakika na maelezo yako? Ni wapi nilipoipinga kauli ya mdude? Onyesha sometimes usiandike kwa mhemko hata Mimi sifurahishwi na yanayofanyika kwa hio kua muelewa kwanza Ila mkimlazimisha huyu mama kuwafanya mnavyotaka awafanye watanyooshwa watu hadi mtaona huruma nyinyi ndio mtarudi na kusema mama usiwafanye hivyo, kumbuka sakata la MBOWE kupewa furushi la UGAIDI
 
Shida ya Mdude mdomo wake hauna break, au keyboard yake haina break.

Kukosowa ni muhimu sana, lakini mtu mstaarabu kama mama unamkosowa kwa lugha za kiungwana.

Yule shetani wa Chato ndio alistahili kukosolewa in a radical way kwa sababu hakuwa mstaarabu.
Umemalizia kwa kuandika ujinga
Jinga
 
Ukimtesa anafurahi? Hayo sio matatizo ya kisaikolojia?
Naam. Kama tatizo ni mambo ya kisaikolojia, au matatizo ya afya ya akili sijui. Ila kama ndivyo, wale wasio na matatizo ya kisaikolojia hawana haja ya kushindana na mtu mwenye matatizo ya kisaikolojia.
 
Yani kweli unategemea rais Samia aanze kukimbizana na kichaa, ili iweje? Watu wote tunajua (hata makamanda wenzie wanajua) kuwa mdude hazimtoshi (kama lisu), sasa rais aanze kuparurana naye ili iweje?
Rais ana mambo mengi ya msingi ya kufanya, siyo kushughulika na vichaa. Hao watashughulikiwa na dada Ummy.
Dah
 
Wanasema mtu mpole akichukia ni hatari sana tena sana , huyu mama amekuwa mkimya japo aliwahi kuonya kuhusu kupapasa na kukuna kwa wabaya wake ,kama unabisha muulize Diwani Athumani na Mbowe .

Huyu mama siku akimchoka Mdude mjue ndio mwisho hatapiga Makele kama ya mwendazake itakuwa kimyakimya sana

USSR
Hacha kuingilia uhuru wa maoni ya mwenzio kunguni wewe!
 
Kwahiyo mnataka wote tuwe "machawa/Chawa" wa Bi kirembwe?. Ukisifia wewe inatosha hizi Mambo za kijinga kutaka watu wasema upande mmoja wa shilingi muasisi wake alaaniwa kabisa.
 
tatizo chawa hampendi mtu wenu asemwe

alivyokuwa anafanya awamu ya tano akachukuliwa hatua mlisema kaonewa,sasa anawaambia ukweli hamtaki kuusikia binafsi sijaona ubaya wowote alioandika hapo kasema UKWELI
CCM imefanikiwa kutengeneza kizazi Cha kijinga chenye nidhamu ya kujikomba na kijipendekeza na UKUDA.
 
Ww unatakaje labda?
Mie nimeuliza tu maana nilikuwa najua watu wanataka nguvu za hoja na watu washindane kwa nguvu za hoja sikujua kuwa kumbe kuna lugha ngumu pia.
 
Mimi siipendi ccm lakini nampenda mama pia namuombea msamaha mdude mbele ya mama na system pia namuomba mama na system wawe wavumilivu Kwa wakosoaji!!
Unamwombea msamaha kwa Kosa gani?
 
Acheni upumbavu wenu, nyie ndio wezi wa mali za umma, Mdude yuko sahihi kabisa na watanzania tunaojitambua tunahitaji Mama achukue hatua kali sana but akishindwa why asijiuzulu ili aje mtu anaeweza kusimamia na kulinda mali ya nchi?

Samia anaonyesha udhaifu kwakweli, kabla hajamchoka Mdude ajue watanzania tayari tumeshamchoka, hivi unakuaje Mkuu wa nchi usiyekuwa na maumivu makali pamoja na huruma kwa raia wako?

Mdude go go ahead tumekuruhusu make tumechoka Sasa, hawa debe tupu wanaopiga kelele humu kukuchongea kwa Mama hawa ndo wajinga majizi wasiojitambua wala rushwa wanaamini katika kutekana, kuua, na kupoteza kama alivyo kuwa akifanya baba yao
Wewe unamchochea Mdude kwa sababu unajua we huwezi kutekwa wala kuuwawa kwa kusema huo ukweli sababu umejificha nyuma ya keyboard.
 
Back
Top Bottom