ipo siku nitampiga makofi wife akiwa anasali

ipo siku nitampiga makofi wife akiwa anasali

et tukikosana anapofanya maombi ili alale anaanza kunitaja kwenye maombi yake mfano dk 5 zilizopita ndio narudi home nimechelewa anasali na mwanetu et mungu mponye na mme wangu pepo la kuchelewa home mbadilishe .ina niboa kila siku namwambia.ngoja

edward snowden unaugua no doubt.
 
Usimpige wife kwasababu ya kusali, siku unapokuwa na nafasi na hauna hasira jaribu kumshauri taratibu jinsi unavyojisikia, pia mwambie wakati mwingine akuombee kwa siri bila ya wewe kujua ili ukibadilika atajua kweli mungu kafanya kazi. Lakini sasa hata ukibadilika inawezakuwa ni kwasababu umejisikia vibaya kuombewa hivyo. Pia kwa kufanya hivyo mwambie unamtafasiri kama mafarisayo ambao huomba kwa sauti kubwa ili waonekane kama waombaji wazuri. Mwambie maombi yanafanya kazi hata kama anakuombea bila ya wewe kujua kuwa anakuombea (ingawa atakuuliza umejuaje wakati hauombagi? mwambie nimesikia toka JF). Pia jaribu kushiriki kwenye hayo maombi hata mara moja moja kuwatia moyo kuwa upo pamoja nao ili aone pia una m-support. Muonyeshe kuwa pamoja na kuwa hushiriki mara kwa mara lkn uko vizuri nao. Utashangaa badala ya kukuombea kwa kihivyo (yaani kukushitaki kwa mungu) badala yake ataanza kukuombea baraka, neema na mafanikio na hivyo italeta baraka zaidi ndani ya nyumba.

Huko unakotaka kuelekea kutakuletea matatizo. Wanawake nenda nao taratibu ukutumia nguvu utaumia mwenyewe. Hiyo tunaita WIFE MANAGEMENT METHODS.
 
Nionacho hapa ni mwanaume mhafidhina asiyejua nini maana ya kuwa mume...

Hakika unahitaji maombi zaidi...maana sina uhakika kama unaamini katika Mungu wewe...

huwa wananiita tusali wote ila kama kuna kosa hawa niiti
 
Hahahahahaaha Mwee huku ndani hadi raha lol 😀😀😀😀
 
Mkuu tafuta swala tano uoe uachane na huyo mlokole.
 
Mkuu kweli kabisa unataka kumchapa Mkeo kisa anakuombea kwa Mungu jambo jema!!! Ningepata Mke mwene tabia hizo naona ningelikuwa Tayari nilisha okoka kwa Jinsi navyo Muogopa Mungu afu Mtu anishitakie kwake sijui ningezimia hapo hapo
 
huwa wananiita tusali wote ila kama kuna kosa hawa niiti

Kumbe unajua kuwa huwa unafanya makosa eenh!!!

Hili weweseko ulifanyalo hapa naamini ni sehemu ya majibu ya maombi ya mkeo na mwanao...

Badilika bana unatudhalilisha wanaume kiasi unadiriki hata kutaka kutumia nguvu kumuadhibu mkeo...
 
et tukikosana anapofanya maombi ili alale anaanza kunitaja kwenye maombi yake mfano dk 5 zilizopita ndio narudi home nimechelewa anasali na mwanetu et mungu mponye na mme wangu pepo la kuchelewa home mbadilishe .ina niboa kila siku namwambia.ngoja

Ee Mungu mponye edward snowdern, pepo la kumpiga mkewe makofi.
 
Last edited by a moderator:
huwa wananiita tusali wote ila kama kuna kosa hawa niiti

MUNGU YEHOVA hakuyapokea maombi ya YESU kwa kuwa YESU aliomba kikombe kimuepuke huku akijua kuwa hatakubaliwa! sembuse mkeo anayejua kuwa huna helikopta ya kukuepusha na foleni!!! haya mahubiri ya kulegeza mioyo ili kutunisha mfuko wa sadaka utatupeleka pabaya.

Tafadhali print sehemu hii hapa chini umpelekee mkeo asome.

Mkiomba sawasawa na mapenzi yake mtapewa asema BWANA.
 
Hivi mbona leo kila kona nayokatiza ni vichekesho tu...nimechoka mbav zinauma!! Hahahahahaaa..jaman ndo umpige makofi! Lol
 
mkuu naamini mkeo anakupenda sana, nayaonekana ni tabia yako kuchelewa, sasa kaamua kukushitaki kwamungu na shahidi mwanao, naamini kesho hutachelewa
 
Before kuhukumu kuna mengi ya kuuliza..
Huwa ni tabia yako kuchelewa mara kwa mara?
Je huwa mna communicate either yeye kukuuliza sababu ya kuchelewa au wewe kujieleza pasipo kuulizwa?

Inawezekana ulikuwa unawahi ile miaka mitatu ya kwanza ya ndoa halafu ghafla mambo yamebadilika bila sababu za msingi....Ukiona hivyo ujue mwenzio anakumiss nyumbani...Mshukuru Mungu kwa hilo..

Ushauri...
Hakuna sababu ya kupigana makofi, wewe jitahidi uwahi nyumbani, usimamie majukumu yako ya father house na sala kama hizo zitakoma...
 
mkuu naamini mkeo anakupenda sana, nayaonekana ni tabia yako kuchelewa, sasa kaamua kukushitaki kwamungu na shahidi mwanao, naamini kesho hutachelewa

kwani kuchelewa ni kosa gani kwenye ndoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom