Kiraka Kikuu
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 5,904
- 1,976
Jamani,kama kuna mwana jamii anajua tofauti ya maneno haya: FEDHA,HELA na PESA, tusaidiane.
Cc Kiranga FaizaFoxy Madame B.
===========
Huitwa ‘Fedha’ wakati mwingine huitwa ‘Pesa’ na wengine huita ‘Hela’. Ushajiuliza kwa nini majina haya tofauti na nini asili yake?
Fedha ni Kiswahili cha madini ya ‘silver’, ambayo miaka ya nyuma yalitumika kama njia ya kubadilishana huduma na bidhaa.
Hivyo ikapelekea kitu kinachotumika kubadilishiana bidhaa na huduma kuitwa fedha hadi leo hii.
Hela imetokana na ‘Heller’ ni kipimo cha sarafu ya Kijerumani kilichotumiwa walipokuwa wanaitawala Tanganyika.
Pesa imetokana na 'Paisa' ambayo ilikuwa ni kipimo cha sarafu ya Kihindi kilichotumika miaka nyuma walipokuwa wakifanya biashara Afrika Mashariki.

Last edited by a moderator: