Ipi tofauti ya maneno haya: Fedha, Hela, Pesa?

Kiraka Kikuu

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,904
1,976
Jamani,kama kuna mwana jamii anajua tofauti ya maneno haya: FEDHA,HELA na PESA, tusaidiane.
Cc Kiranga FaizaFoxy Madame B.

===========

Huitwa ‘Fedha’ wakati mwingine huitwa ‘Pesa’ na wengine huita ‘Hela’. Ushajiuliza kwa nini majina haya tofauti na nini asili yake?

Fedha ni Kiswahili cha madini ya ‘silver’, ambayo miaka ya nyuma yalitumika kama njia ya kubadilishana huduma na bidhaa.

Hivyo ikapelekea kitu kinachotumika kubadilishiana bidhaa na huduma kuitwa fedha hadi leo hii.

Hela imetokana na ‘Heller’ ni kipimo cha sarafu ya Kijerumani kilichotumiwa walipokuwa wanaitawala Tanganyika.

Pesa imetokana na 'Paisa' ambayo ilikuwa ni kipimo cha sarafu ya Kihindi kilichotumika miaka nyuma walipokuwa wakifanya biashara Afrika Mashariki.
 
Last edited by a moderator:
Jamani,kama kuna mwana jamii anajua tofauti ya maneno haya: FEDHA,HELA na PESA,tusaidiane.
Cc Kiranga FaizaFoxy Madame B.

Mimi ninavyojua ni hivi. Wakuu msisite kunisahihisha.

Fedha = Silver
(kwa hiyo sarafu za silver ziliitwa fedha. Kwa kuwa enzi hizo wazee wetu kikubwa alichoweza kulipwa ni siver coins, hence fedha ikawa sawa na money)

Hela ni unit ya kijerumani ambayo alipokuja Muingereza ilikuwa sawa na Senti 2
Kwa hiyo wale watu wa Tanga tuliokulia wakati wa mkoloni, ukisema "mkate huu bei yake ni hela 10", tulimaanisha "bei yake ni senti 20". Enzi zangu Tanga watu walinunua maji ya manispaa kwa debe senti 1 au nusu hela. I am dating myself here.

Pesa au Peso ni unit ya kispaniola na sisi tukaitumia kama unit ya MONEY.

Nyongeza:

Ngawira = mali uliyo ipata kwa ufisadi. Hili neno saa nyingine linatumiwa kwenye lugha za mitaani kumaanisha MONEY
 
Hela = Kijerumani "heller" hii ilitokana na wajeruma walipotutawala.

Pesa = Paisa, Kihindi, pesa za kihindi zilikuwa dominant enzi hizo za Biashara ya Bahari ya hindi na zikitumika ufuko wote wa Bahari ya Hindi na Wajerumani walipotutawala wakaendeleza, kuna wakati tulikuwa na Paisa ya Kijerumani.

Kulikuwa pia kuna Rupia ya kihindi na Kijerumani (German Rupee). Na ndipo fumbo "penye udhia tia rupia" lilipotokea. Rupia (rupee) na Paisa mpaka leo ni pesa halali za India na au Pakistan na kwingineko kuchache.

Jee, unajuwa kuwa hapa kwetu tulikuwa na sarafu aa dhahabu kabla ya Ulaya (Europe)? za kwanza kabisa zilikuwa zikifyatuliwa Kilwa na baadae Tabora. Soma.

Majina mengine yaliyokwisha wahi kutumika kwetu na kwingine; Riali, Dirham (Darahim), njuluku, mkuraba (mkuraba haujazi kibaba).
 
Mimi ninavyojua ni hivi. Wakuu msisite kunisahihisha.

Fedha = Silver
(kwa hiyo sarafu za silver ziliitwa fedha. Kwa kuwa enzi hizo wazee wetu kikubwa alichoweza kulipwa ni siver coins, hence fedha ikawa sawa na money)

Hela ni unit ya kijerumani ambayo alipokuja Muingereza ilikuwa sawa na Senti 2
Kwa hiyo wale watu wa Tanga tuliokulia wakati wa mkoloni, ukisema "mkate huu bei yake ni hela 10", tulimaanisha "bei yake ni senti 20". Enzi zangu Tanga watu walinunua maji ya manispaa kwa debe senti 1 au nusu hela. I am dating myself here.

Pesa au Peso ni unit ya kispaniola na sisi tukaitumia kama unit ya MONEY.

Nyongeza:

Ngawira = mali uliyo ipata kwa ufisadi. Hili neno saa nyingine linatumiwa kwenye lugha za mitaani kumaanisha MONEY

Uongo! Ngawira ni mali iliyotekwa kwenye vita na inayogawanywa kwa walioiteka.

Mlungula ndio mali inayoshabihiana na ya ufisadi, aka Hongo, Rushwa, mlungula hautolewi haupokelewi kwenye uhalali.

Kuhonga ni kuliwaza/kuhadaa kwa kutoa mali au pesa ili upate unayotarajia kwa aliye honga / hongwa. Unaweza kuhonga kiharamu au kihalali.
 
Uongo! Ngawira ni mali iliyotekwa kwenye vita na inayogawanywa kwa walioiteka.

Mlungula ndio mali inayoshabihiana na ya ufisadi, aka Hongo, Rushwa, mlungula hautolewi haupoklewi kwenye uhalali.

Kuhonga ni kuliwaza kwa kutoa mali au pesa ili upate unayotarajia kwa aliye honga. Unaweza kuhonga kiharamu au kihalali.
Asante kwa sahihisho bibie.
 
Fedha = Silver
Hela = Kijerumani "heller" hii ilitokana na wajeruma walipotutawala.
Pesa = Paisa, Kihindi, pesa za kihindi zilikuwa dominant enzi hizo za Biashara ya Bahari ya hindi na zikitumika ufuko wote wa Bahari ya Hindi na Wajerumani walipotutawala wakaendeleza, kuna wakati tulikuwa na Paisa ya Kijerumani.
Kulikuwa pia kuna Rupia ya kihindi na Kijerumani (German Rupee). Na ndipo fumbo "penye udhia tia rupia" lilipotokea. Rupia (rupee) na Paisa mpaka leo ni pesa halali za India na au Pakistan na kwingineko kuchache.

Je, unajuwa kuwa hapa kwetu tulikuwa na sarafu aa dhahabu kabla ya Ulaya (Europe)? za kwanza kabisa zilikuwa zikifyatuliwa Kilwa na baadae Tabora. Soma.

Majina mengine yaliyokwisha wahi kutumika kwetu na kwingine; Riali, Dirham (Darahim), njuluku, mkuraba (mkuraba haujazi kibaba).

Ahsante Madam FaizaFoxy, umenipa elimu kubwa sanaa!
Sasa,naona majina hayo matatu{hela, fedha na pesa yanatumika kutambulisha currency Tz.

Unaweza kunisaidia, ni wakati upi sahihi wa kutumia jina husika?
Mimi ninavyojua ni hivi. Wakuu msisite kunisahihisha.

Fedha = Silver
(kwa hiyo sarafu za silver ziliitwa fedha. Kwa kuwa enzi hizo wazee wetu kikubwa alichoweza kulipwa ni siver coins, hence fedha ikawa sawa na money)

Hela ni unit ya kijerumani ambayo alipokuja Muingereza ilikuwa sawa na Senti 2
Kwa hiyo wale watu wa Tanga tuliokulia wakati wa mkoloni, ukisema "mkate huu bei yake ni hela 10", tulimaanisha "bei yake ni senti 20". Enzi zangu Tanga watu walinunua maji ya manispaa kwa debe senti 1 au nusu hela. I am dating myself here.

Pesa au Peso ni unit ya kispaniola na sisi tukaitumia kama unit ya MONEY.

Nyongeza:

Ngawira = mali uliyo ipata kwa ufisadi. Hili neno saa nyingine linatumiwa kwenye lugha za mitaani kumaanisha MONEY

Ahsante Kifyatu [though sijui kwanini umejiita hivyo,lol!]
Jaribu kunielezea bs wakati upi ni sahihi kutumia jina lipi.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante Madam FaizaFoxy,umenipa elimu kubwa sanaa!
Sasa,naona majina hayo matatu{hela,fedha na pesa yanatumika kutambulisha currency Tz.
Unaweza kunisaidia,ni wakati upi sahihi wa kutumia jina husika?

Ahsante Kifyatu [though sijui kwanini umejiita hivyo,lol!]
Jaribu kunielezea bs wakati upi ni sahihi kutumia jina lipi.

Lugha hukuwa inapokuwa na maneno mengi. Sina utaalamu zaidi wa wapi uyatumie, binafsi nimekuwa nikiyatumia yote bila kufikiria na nnauhakika mara zote nimeeleweka.

Mlipe pesa zake,
Nadai fedha zangu nyingi,
Ana hela nyingi,
Sina hata senti tano na kadhalika.
 
Ahsante Madam FaizaFoxy,umenipa elimu kubwa sanaa!
Sasa,naona majina hayo matatu{hela,fedha na pesa yanatumika kutambulisha currency Tz.
Unaweza kunisaidia,ni wakati upi sahihi wa kutumia jina husika?

Ahsante Kifyatu [though sijui kwanini umejiita hivyo,lol!]
Jaribu kunielezea bs wakati upi ni sahihi kutumia jina lipi.

Mkuu jina la Kifyatu ni la utani nililopewa na babu yangu.

Kama mkuu FaizaFoxy alivyosema, mimi pia huyatumia hayo maneno interchangeably nikimaanisha money.
 
Naomba ufafanuzi utofauti iliopa kati ya fedha na pesa ili nijue kama ni katika mazingira yapi huwa nakosea kutamka

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Pesa

17cf71c8e83b346f76ae414b9e60daf3.jpg

Fedha

873bf18f53bedafb84acc7c8208d7f8a.jpg
 
naomba ufafanuzi utofauti iliopa kati ya fedha na pesa ili nijue kama ni katika mazingira yapi huwa nakosea kutamka

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
Pesa ni alizonazo Jay Z
Fedha ni alizonazo Bill Gates

Sijui Umenielewa??

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
naomba ufafanuzi utofauti iliopa kati ya fedha na pesa ili nijue kama ni katika mazingira yapi huwa nakosea kutamka

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app

Fedha ni Madini ambayo kwa kiingereza yanaitwa Silver, Pesa ni thamani iliyokubaliwa kwenye kununulia vitu mbalimbali, Pesa inaweza kutengenezwa na Fedha(Silver), dhahabu (gold), Shaba (Copper) au Makaratasi
 
Pesa ni ile unaweza kuihesabu moja moja. Unafikia mahali unaanzakuzihesabu kwa mafungu yaani laki, milioni, bilioni na kundelea.

Hapa wanatumia hayo mafungu kuhesabia.
Sisiwengi tunazo pesa na huwa tunatumia pesa sana kilasiku. Wenye nazo hutumia fedha yao kufanyia shopping.
 
Pesa - kwa kiingereza ni Money
Fedha - kwa kiingereza ni Finance
Feza - Kwa kiingereza ni Silver.

Maelezo ya kina yatakuaja bdae nikimaliza shuguli flani hapa kwa ofisi...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom