Ipi tofauti ya maneno haya: Fedha, Hela, Pesa?

mmmh.. anyway, usikute na wewe ni mwalimu tena unafundisha watoto wetu kabisa
 
Mimi nataka nitupe maneno mengine ya kiingereza ya kuongelea hela:

Kwa matumizi rasmi:
Money
Currency
Cash
Legal tender
Funds
Payment

Yaliyo misemo ya kimarekani:
Green
Dough
Cheddar
Lettuce
Moolah

Yako mengi mengine
 
Pesa - kwa kiingereza ni Money
Fedha - kwa kiingereza ni Finance
Feza - Kwa kiingereza ni Silver.

Maelezo ya kina yatakuaja bdae nikimaliza shuguli flani hapa kwa ofisi...
Ulichofanya umetafsiri lkn hujaeleza fasili hasa ya maneno hayo. Nijuavyo mm neno pesa ni neno lenye asili ya kihindi km sijakosea na hela(heller) lina asili ya kijerumani kwa ujumla wake maneno haya yana maana sawa na neno lingine la kiswahili tulilolizoea la fedha kuumanisha kitu chenye thamani ktk noti au sarafu kitumikacho kununulia bidhaa au kulipia huduma.

Sasa fedha/hela/pesa hupewa majina tofauti kulingana na nchi mbalimbali km vile dola, kwacha, shillingi, kwanza, rupia nk.

Ikumbukwe pia kuwa ktk lugha ya kiswahili kuna kitu kinaitwa istilahi yaan maneno maalum yanayotumika ktk taaluma au fani fulani. Mfano kwenye lugha kuna istilahi inaitwa nomino inayomaanisha jina lkn neno hilo nomino huwezi kulitumia ktk mazungumzo ya kila siku mfano ktk sentensi hii "hivi ww nomino yako ni nani" kumaniisha kuwa jina lako ni nani. Sentensi hiyo inakuwa si sahihi.
Hivyo basi hata maneno hayo hapo juu mengine ni istalahi yaani hutumika zaidi kitaaluma kuliko ktk matumizi ya kawaida mfano neno fedha(currency kwa kiingereza km sijakosea) wkt maneno km hela na pesa ni maneno(misamiati) ya kawaida lkn matumizi(maana) zake ni sawa au karibu sawa.

Hayo ni kwa uelewa au maoni yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom