Ipi ni siku ya kwanza ya juma? nimeambiwa ni Monday kwetu tunaita Jumatatu. Ukweli ni upi?

Vito Corleone

JF-Expert Member
Apr 4, 2023
2,233
4,783
Tumekuwa na kawaida Kila Jumalipi tunaenda kanisani kusali Kwa sisi Wakristo na tukisisitizwa kuwa ni siku ya Bwana; kuwa alipumzika siku ya Saba.

Je lugha yetu inanichanganya maana nafahamu juma mosi ndio mwanzo wa wiki, jumapili ni siku ya pili and so on. Nimegoogle ipi ni siku ya kwanza ya juma nimeambiwa ni Monday kwetu tunaita jumatatu.

Na hii google inasema ni according to ISO 8601 inayosimamiwa na shirika la kimataifa la Muda? Na kwamba wali toa chapisho la la kwanza 1988?

Yaani nimedata hapa naomba msaada.
 
Siku zote ni sawa, wewe tenga siku unayoona ni njema kwako ifanye iwe ndiyo sabato yako.

Kila siku ukimuomba/kumuabudu MUNGU unapata matokeo chanya.

Kol 2:16-17​

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
 
Tumekuwa na kawaida Kila J2 tunaenda kanisani kusali Kwa ss Wakristo na tukisisitizwa kuwa ni siku ya Bwana; kuwa alipumzika siku ya Saba.Je lugha yetu inanichanganya maana nafahamu juma mosi ndio mwanzo wa wiki,jumapili ni siku ya pili and so on.Nimegoogle ipi ni siku ya kwanza ya juma nimeambiwa ni Monday kwetu tunaita jumatatu.Na hii google inasema ni according to ISO 8601 inayosimamiwa na shirika la kimataifa la Muda??what the Fack.Na kwamba wali toa chapisho la la kwanza 1988????Yaani nimedata hapa naomba msaada.
Indeed, WTF!
 
Hayo mambo ya siku za Ibada wamekuletea Wazungu na Waarabu, Babu zako hawakua na siku maalum za kwenda kutambika jaribu kufuatilia Dini zako za asili utaelewa jambo, enzi hizo walikua wanaishi kusogeza siku hakukua na jumamosi wala jumapili hizo jumamosi na jumapili ameleta Mzungu anaitwa Gregory ndio unayotumia kwa hio unaishi kile Gregory alichosema ukichunguza kwa makini kwenye hio Biblia kwa mfano hakuna sehemu imekwambia ukafanye Ibada Jumapili haipo mwandishi wa biblia ameandika biblia kwa code anakwambia siku ya kwanza ya Juma hio ni code name
 
Tumekuwa na kawaida Kila Jumalipi tunaenda kanisani kusali Kwa sisi Wakristo na tukisisitizwa kuwa ni siku ya Bwana; kuwa alipumzika siku ya Saba.

Je lugha yetu inanichanganya maana nafahamu juma mosi ndio mwanzo wa wiki, jumapili ni siku ya pili and so on. Nimegoogle ipi ni siku ya kwanza ya juma nimeambiwa ni Monday kwetu tunaita jumatatu.

Na hii google inasema ni according to ISO 8601 inayosimamiwa na shirika la kimataifa la Muda? Na kwamba wali toa chapisho la la kwanza 1988?

Yaani nimedata hapa naomba msaada.
Siku ya kwanza ya juma ni jumapili, ndo siku alifufuka Yesu
Ndo maana kuna pasaka ya jumapili kuadhimisha ufufuo wa Yesu
Alisulubiwa Ijumaa ambayo hadi leo tunaiita ni ijumaa kuu
Siku ya saba Yesu alibaki kaburini kupumzika sababu ilikuwa ni sabato, yaani siku ya saba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom