Ipi ni CCM 'B' ACT Wazalendo au CHAUMMA?

Ipi ni CCM 'B' ACT Wazalendo au CHAUMMA?

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
15,894
Reaction score
36,382
Wana chadema tuliamini CCM B ni ACT Wazalendo Sasa Leo baada ya CHAUMA ya Hashim Rungwe Mzee wa Ubwabwa kupokwa waasi wa chadema na kuwapa madaraka, hii inatuchanganya

Awali upinzani wa ACT Wazalendo ulitiliwa shaka yaani ulikuwa upinzani wa zuga tu, binafsi naona hii kasi ya CHAUMA Kuna nguvu wanayo kutoka CCM na serikalini ili kuibomoa chadema

CHAUMA angekuwa mpinzani WA kweli angeibomoa CCM ili kuimarisha Chama chake ila kuibomoa Chadema hapa napata mashaka na aina ya upinzani wake

Adui wa maendeleo na Watanganyika ni CCM ilitakiwa vyama vya upinzani view na sera kama za chadema ili kuiondoa CCM madarakani

Nasema wazi Chadema kazi tunayo, maadui wanajiinua Kwa namna tofauti hapa tupambane na CCM na wapinzani wenzetu akina ACT Wazalendo na CHAUMA
 
ACT haina uwezo wa kuivuruga chadema ndyo mana wameongezewa nguvu na ccm kwakuleta chauma.kumbuka act na chauma ni vibrka wa ccm waliotoka chadema na motive yao ni kubomoa upinzani usiwe na nguvu
 
Ni hakika ktk hili.Muonekano wake imepikwa na CCM ili kupunguza au kuivuruga CHADEMA.chauma halisi haipo ipo CHAUMA feki ili kutimiza malengo waliyopewa na CCM kufanikisha mambo yao ya kimkakati na kupiga pesa za ccm.
Mwisho Kitakuwa chama pendwa kikitunzwa na CCM na kitakosa hoja na wananchi wamekistukia ujaji wake tofauti na vyama vingine hii ya trip hii imetushtua haiko kimapambano halisi.
 
wekeni focus kwenye chama chenu, acheni viherehere kila wakati kujadili vyama visivyov yenu
 
Hivi vyama toka Kigoma mbona vinachanganya? Wapinzani wakianza kuonyesha mkakati wa kuing'oa CCM, wao wanatoka kivyao.

Je mbali na kuwa CCM B, hivi siyo vyama vya mfukono ambavyo wanaovimilki hutumia kupiga pesa na kusaliti umma?
 
Back
Top Bottom