iPhone na matatizo yake: Ushauri, maujanja, matengenezo na mengineyo

iPhone na matatizo yake: Ushauri, maujanja, matengenezo na mengineyo

Ahsante sana rafiki ila Nina tatizo jingine tena but ktk Simu yangu ya pili iPhone 4s yenye line ya Voda
Hii Simu mwanzo ilikuwa sawa but ikaja kupata tatizo la touch
hivyo Jana nikabadili
huwa zinauzwa complete display + touch
Sasa tangu niweke iwekewe hichi kioo
Niliweka Line yangu kama kawaida but tangu Jana hadi leo ina
b787f0d22ea1ea6e3f8182eb670c5fe0.jpg

Inaandika SEARCHING
961927f2e53f573c1fa6cad707b7f06e.jpg

Upande wa carrier inatambua kuwa ni Vodacom
Mtu akiipiga hii line atasikia Simu ikiita but Mimi Simu wala haioneshi kitu chochote wala hata missed call sioni
ipo tu kawaida
Hili tatizo nimemsolvia jana usiku mtu ana iphone 4s pia aliwahi badili display lakini ameitumia miez zaidi ya mitatu jumamosi aliiconect na itunes ikaanza hilo tatizo.
Nilichokifanya niliondoa cydia maana ilikuwa jailbroken then nikaenda settings, general, reset nika reset network settings ikawa sawa kabisa.
Hebu jaribu uone
 
Oh okay nikienda hadi setting na nikafanya hivyo ktk upande wa Network
Sasa baada ya kumaliza imeandika
No Service
Duh!
953057048337fc9412db61e5d9d6dee9.jpg
Irestart kwa kubonyeza home button na button ya power ikizma thn ukaskia ina vibrate ziachie uone kama ikiwaka itasoma
 
Nimefanya hivyo ulivyonielekeza but imewaka kawaida bila ku-vibrates
Na sasa imerudi pale pale pa awali
SEARCHING
1805731250bde3906d21cf9d8d6bfd98.jpg
Tarehe yake iko sawa? Kama haiko sawa iset manually.
Halafu fanya kuzima kwa kuhold home button na power button mpaka ikiwaka ikaleta apple logo ndo u release.
Ilizingua chomoa sim kadi ukiwa umeiwasha then chomeka isiposoma zima simu chomoa sim card washa ikishawaka chomeka.
Kati ya hizi moja ita work out hilo ni tatizo la kawaida la iphone 4s after lcd replacement
 
Katika maisha yangu hata siku moja sijawahi kumsifu mzungu
coz kuna vitu vinafanywa japo ni Ulaya but ni mwafrika mwenzetu kumbe ndiye kavifanya
Hakika ELMAGNIFICO umekuwa msaada mkubwa sana kwangu
Kweli ni Tar haikuwa sawa baada ya kuiweka sawa manually then nikaizima as you asked me to
Then imekuwa SAWA 100%
Kutoka moyoni mwangu nasema AHSANTE SANA Na ubarikiwe
Nimetambua na kuthamini msaada wako kwangu
coz hiyo inaonesha ni tabia yako
Kupenda kuwasaidia watu
Nikuombe tu usichoke rafiki
Hili jukwaa lifike mbaaali mnooo coz linatusaidia mambo mengi mno
Kweli huu ni uwanja wa iPhone
4de980606fd3581326c90d201ef27545.jpg
Nashukuru sana mkuu na mimi nimefurahi kuona mchango wangu umeweza kukusaidia na ukaleta feedback maana wengine uwa hawaleti mrejesho.
Asante sana mkuu
 
Hiyo ya kutokurejesha feedback huwa ni hulka ya sisi binadamu
Shida ikiisha tu au tatizo likiishapata ufumbuzi tu
Unaona kumbe hata mimi mwenyewe ningeweza tu sema ni vile sijatuliza akili
Ila kiukweli ukipewa msaada inabidi uuthamini haijalishi ni mkubwa au kidogo kiasi gani
coz huyo mtu aliyekusaidia amechukua nguvu zake, muda wake (kitu ambacho ni cha thamani) kukusaidia tu wewe huenda alikuwa na shaghuli zake Ila ameamua kuziweka pembeni ili tu akausaidie
Guys tuweni na tabia ya kuleta mrejesho na kushukuru tunapopewa msaada
coz leo ukijiona mjanja kuna kesho pia hujui litakupata lipi
 
Hii MacBook Pro ni ya Mwaka 2008
Sasa nilikuwa natumia upande wa Mac kama Mac na part nyingine nilikuwa nimeweka Windows
Sasa nikiiwasha inaanza processes za kuwaka but inaishia ktkt then display inakuwa WHITE
alafu tena inaanza upya
Inaleta LOGO ya APPLE kisha kale kamstari ka chini kanatembea kakifika katkati
Display inakuwa white alafu kama sekunde hivi display inakuwa Black hapo inakuwa imezima
Ila tena inaanza kuwaka upya kama hapo awali
Sasa mchezo ni huu huu tu hakuna kinachoendelea zaidi ya hapo
Mkuu anza na hii izime kisha washa na uwahi ubonyeze option key, ishikilie mpaka itakapoleta start up manager.
Kisha tumia arrow keys kuteremka mpaka kwenyae primary hd ambayo itakuwa inasomeka akama macmtosh hd ukiifikia ponye R then computer ita reboot.
Nipe mrejesho
 
Msaada jinsi wa kujua IPhone original au fake
Simple angalia kama inasupport icloud mkuu.
Au ingia app store download app yoyote ya benchmark irun itakuwa specifcs za sim husika na kama fake utajua
 
Okay wakati ikiendelea na hiyo process imeniuliza Kama natumia English as a main Language nibonyeze RETURN key
Nami nimebonyeza japo bado inaendelea na hiyo process
Kama ikiishia vile vile mkuu iwashie kwenye safe mode uone kama itafika mwisho maana through safe mode uwa ikiwa inawaka ina repair some errors.
Zima then washa na wahu bonyeza shift key itawakia kwenye safe mode then niambie kama imewaka mpaka mwisho mkuu
 
Rafiki Mbona imezima ghafla hata huo mstari haujafika mwisho?
Ilipozima haijajirestart? Kama haijajirestart ili start mwenyewe ikiendelea fanya kama nlivyokwambia iwashie kwenye safe mode.
Au kwa msaada zaidi ndugu unaweza nitupia namba yako pm maana soon ntakuwa off jf so naweza nikakuchek hata asubuh nkakuelekeza vzuri zaid
 
Haijaji-restart na nimei-restart mwenyewe but naona it’s like ndani inafanya though display ni nyeusi haijawaka
Alright wacha nikutumie namba pia
Sawa nitakuchek kesho mkuu mida ya saa tatu nne nitumie namba sasa hivi nalala
 
wajuzi wa mambo msaada tafadhali,,nina iphone 6+ ina shida ya ku-touch screen na sometimes inajiandika,,yani inajifungua app zilizoko kwenye screen bila mimi kuzigusa,,
 
Back
Top Bottom