Interview TPB: Naombeni mnisaidie aptitude test

Interview TPB: Naombeni mnisaidie aptitude test

Wakuu poleni na majukumu ya kila siku!

Lengo la kuandika hapa nikuwaombeni mnisaidie aptitude test ya bank ya TPB huwa inakuaje?

Au maswali yake huwa vipi?

Maana nimeitwa kwenye interview, naombeni msaada
Mkuu usipoteze mda. Wale huwa Wana watu wao tayari wanazugaga. Hakuna ambaye huwa anaitwa na paper hazisahihishwi. Ukimaliza kufanya na wakakusanya wanaenda moja kwa moja kuzichoma Moto.
 
Mi ninafanya kazi tpb. Nina watu wangu wawili nimewaambia waende kwenye aptitude test kuzuga ila tayari nimeshafanya mipango
 
Watu nendeni mkafanye test, Kwan sh ngapi? Maswali yenyewe kuchagua tu waweza ukaotea yote. Msiogope! Mimi ndo nimetoka uko.
 
Huu uzi wa tpb...utakua una trend sana mpaka hao 58 wakipatikana.

Inaonekana 57% ya waliofanya aptitude wako hapa jf .
 
Haya mambo wangeweza tu kuyafanya online basi mchezo unaisha
Naaam na uwingi ule wa raia umewakatisha tamaa vijana wengi hakuna namna mitaala yetu ibadilishwe tu ili kuwajenga vijana wajitambue, watambue talanta zao na uwezo wao ili watafute knowledge sahihi ili wabaini skills sahihi wanazoendana nazo mapema wakiwa shuleni ili kama kujiandaa na fani wenye passion nazo waweze kujiajiri ili kukabiliana na hali ya maisha. Dunia Ya sasa maarifa sahihi, skills sahihi, taarifa sahihi ndio injini kuu za kumsaidia kijana kujiingiza kipato.
 
Huu uzi wa tpb...utakua una trend sana mpaka hao 58 wakipatikana.

Inaonekana 57% ya waliofanya aptitude wako hapa jf .
Kabisaaaa ndio maana kadri interview inavyoelekea ukingoni ndio na uzi unavyozidi kusinzia kwa kuwa walengwa wamekata matumaini kwa hesabu za std 7 zilizowekwa kwa kiingereza.
 
Kabisaaaa ndio maana kadri interview inavyoelekea ukingoni ndio na uzi unavyozidi kusinzia kwa kuwa walengwa wamekata matumaini kwa hesabu za std 7 zilizowekwa kwa kiingereza.

Vipi we ushafanya
 
Ulitaka uitwe peke yako?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Inshu sio kuitwa pekee yake!!bali ni uwiano sawia kati ya nafasi za kazi na wanaoitwa kwenye usaili!!we unakuta nafasi 20, wanaoitwa kwenye usaili ni watu 600?!!hata kama ajira ni ngumu lakini sio kuwafanyia watu hivyo, ita uwiano mzuri ili kila mtu, aone ana nafasi ya kupata!!hata kama anakopa nauli huko alipoko, angalau, wewe unajaza watu uwanja kwa nafasi 200!???
 
Hongereni wote mliofanya interview! Sasa tusubiri matokeo! Kila rakheri kwa wataofaulu kwa hatua ya oral nk, Na ambao hatutofanikiwa mapambano yaendelee hadi kieleweke 🤞💪
 
Back
Top Bottom