Online Aptitude Test - Ajira Aptitude Test

Online Aptitude Test - Ajira Aptitude Test

Attaboy

New Member
Joined
Jul 26, 2024
Posts
3
Reaction score
9
Salamu kwenu wadau, poleni na majukumu na mapambano ya kusaka ajira.

Sote tunajua jinsi ilivyo ngumu kufaulu usaili wa ajira za utumishi wa umma. Changamoto huwa ni pale unapofika kwenye chumba cha mtihani; unakutana na maswali 50/100, halafu muda ni mchache. Wengi wetu unakuta tunafeli sio kwa sababu hatujui majibu sahihi ila hofu ugeni wa aina hii ya usaili na kubanwa na muda mdogo kwa maswali mengi. Unakuta mtu anatoka na 48% kwa sababu alishindwa kumaliza maswali.

Binafsi, nashauri tuzoe kufanya mazoezi ya kujipima kwa hizi Online Aptitude Test mara kwa mara sio tu ukiskia umeitwa ndio uanze mazoezi, tujenge mazoea ya kujipima kabla ya kufanya usaili halisi.

Tofauti na zile PDF na ma-past papers tunayosomaga mitaani, ingewekwa mifumo maalum ya kufanya mazoezi online mifumo ya kitanzania yenye kuendana na soko letu la ajira. Mfumo kama Ajira Aptitude binafsi nimeona ni mizuri na imekuwa mkombozi sana kwetu vijana na wasomi tunaosaka ajira kila kukicha tunapokea "NOT SELECTED FOR ORAL INTERVIEW" .
 
Back
Top Bottom