Intelligence heredity: Je, uwezo wa akili hurithiwa?

Intelligence heredity: Je, uwezo wa akili hurithiwa?

Habari za weekend wana JF, kuna swali nimekua nikijiuliza muda mrefu sana na kuna mada iliwekwa humu JF ambapo wachangiaji wengi kina Wick na Malcom Lumumba waliijadili hii issue ila kwa kugusia tu maana haikuwa kiini cha mada.

Ukweli mchungu: Pasipo anguko la Malaika (Sons of Gods/Watchers/Anunnakis/Aliens), Mwanadamu angeendelea kubaki kilaza. - JamiiForums

Humo ndani kuliibuka debate kama akili za binadamu ni hereditary/genetic au ni mazingira. Baada ya kusoma tafiti /makala kadhaa nikaona nilete mada humu ili tuweze kujadili suala hili kwa upana zaidi na niweze kupata conclusive answer kwa mjadala ule. Na source yangu kubwa ni study hii ya huyu neurosurgeon niliyeambatanisha pdf yake hapo chini.
View attachment 919915

UTANGULIZI
Akili kwa kifupi tu tunaweza kusema ni uwezo wa kufikiri au kuchanganua masuala mbalimbali yanayotuzunguka na kwa mingi wanasayansi wamejaribu kupima hiyo "akili" kati ya mtu na mtu ili kuweza kufahamu sababu halisi za kuwepo utofauti huo yaani mtu kuwa na akili ''ndogo'' au ''kubwa'' kuliko mwenzake.

Mnamo mwaka 1905 serikali ya ufaransa ilitaka kuanzisha mfumo wa "elimu kwa wote" hivyo ikataka kugundua watoto wenye ''akili ndogo'' ili wapewe elimu maalum kuwawezesha kusoma kwa spidi yao kuliko kuwabakisha nyumbani tu au kuitwa "wehu". Mtihani huu uliitwa stanford-simon test ambapo ulikuwa unapima vitu vikuu vitano ambako na sisi ningependa tutumie tunapoendelea na mjadala huu sababu hizi factors ndio zimeweka msingi wa IQ tests na mbinu karibu zote duniani za kupima akili ya mtu.

1.Maarifa (knowledge) ambapo hapa wanapima kama mtoto ana uwezo wa kuelewa mambo yanayomzunguka mfano mtoto aliulizwa kushiba au kuchoka ndio nini?

2. uchanganuzi wa hesabu (Quantitative reasoning) ; Hapa mtoto anaulizwa masuala ya hesabu ili kupima uwezo wa akili yake mfano kujumlisha,kutoa,kugawanya n.k

3. Working memory yaani Kumbukumbu ya muda mfupi ambapo hapa wanapima kama mtoto ana uwezo wa kutunza mambo aliyofundishwa au kuyashuhudia muda mfupi tu uliopita mfano kama unawaonyesha picha basi unawauliza picha ya kwanza kuwaonyesha ilikuwa ya nani.

4. Visual-spatial processing yaani utambuzi wa vitu kwa kuangalia mfano uhusiano baina ya picha na zaidi inayotumika ni puzzle ambapo mtoto alitakiwa kupanga vipande tofauti ili vitengeneze picha moja.
View attachment 919908
5.Ya mwisho ni uwezo wa kuchanganua (fluid reasoning) yaani uwezo wa kufikiri na kupata suluhisho kwa jambo ambalo halitegemei kitu ulichowahi fundishwa au kukutana nacho huko nyuma mfano kuunganisha dots za suala fulani fulani ili upate picha kamili mfano hapa chini ambapo mtoto ataulizwa umbo gani ndio sahihi kuwekwa kwenye alama ya kiulizo??
View attachment 919909
NADHARIA
Baada ya kujua baadhi ya vitu tunavyopima kwenye uwezo wa akili ya mtu.... Basi tuangalie nadharia mbalimbali zilizoletwa juu ya mjadala huu.

1. Akili hurithishwa /Heritability.
Kwenye nadharia hii baadhi ya wanasaikolojia wamejaribu kufanya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa akili ya mtu hurtishishwa kutoka kwa mzazi hivyo uwezo wa akili za wazazi ndio utaamua uwezo wa wanaye kwa kiasi kikubwa. Kwa mujibu wa tafiti nilioambatanisha hapo chini inaonyesha mapacha wakufanana wana wana akili (IQ) zinazofanana kuliko mapacha wasiofanana ikimaanisha jenetiki zina nafasi ya kucheza kwenye kuamua akili ya mtoto. Vilevile utafiti mwingine ukaonyesha ndugu waliokuzwa kwenye nyumba moja wana akili zinazofanana kuliko watoto wasio na undugu waliokuzwa eneo moja ikimaanisha genetics za kifamilia ndio huamua akili ya mtoto na sio makuzi/malezi n.k

Nadhari nyingine inayotumika humu ni wilson effect ambayo inasema mtu anapozidi kukua basi uwezo wa akili yake unakuwa umechangiwa na akili za kurithi kuliko sababu zingine zozote na alihitimisha kwa utafiti unaoonyesha 60% mpaka 80% ya akili ya mtu mzima huwa imerithiwa kutoka kwa kizazi chake na zilizobaki ndio sababu zingine kama elimu,makuzi,mazingira,uzoefu,afya n.k

2. Mazingira/makuzi
Nadharia ya pili inadai mtoto huzaliwa na uwezo wa akili wa kawaida ila mazingira au makuzi atayakayopata ndio yataamua akili yake hapa duniani. Tafiti mbalimbali zimefanyika mfano weinberg (1989) unaonyesha mapacha wanaofanana waliokuzwa mazingira tofauti kabisa uwezo wa akili zao haukufanana ikimaanisha uwezo wa akili huamuliwa na mazingira ambayo mtoto anakulia na sio kurithi akili za mzazi. Mfano mtoto ambaye baba na mama yake wana akili ila amekulia mazingira ya umaskini hivyo kula yake ni ya shida na hapati lishe bora hasa udogoni inaathiri size ya ubongo wake hasa ubongo wa mbele (frontal lobes) hivyo itasababisha uwezo wake wa akili kupungua sana. Ama mtoto mwenye uwezo mdogo wa akili akikulia mazingira ambayo wazazi wanamjengea uwezo wa kufikiri kama kumpa maarifa kadha wa kadha toka akiwa mdogo,kusoma vitabu,mitihani ya kimaisha ya kumfanya afikiri basi mtoto huyu akili yake (IQ) itapanuka muda unavyozidi kusogea.

View attachment 919916

Tabula rasa
Hii ni nadharia iliyoanzishwa na John locke (1690) inayodai mtoto akizaliwa huwa ni MWEUPE kichwani ila uwezo wake wa akili utaamuliwa na mazingira,uzoefu,maarifa atakayopata kwenye makuzi,mazingira au uzoefu anavyozidi kukua. Hivyo kwa kiujumla nadharia hii inasema haijalishi mtoto kazaliwa na akili gani ila makuzi yake ndio yataamuwa kama atakuwa na akili ''kubwa'' au ''ndogo''.

NB: tunapoongelea akili hatumaanishi za darasani na hatumaanishi jinsi mtu anavyozitumia bali tunamaanisha UWEZO wa juu zaidi ambao anaweza kutumia kufikiri hata kama bado hajaamua kuutumia ipasavyo. Kiufupi tunaangalia brain CAPACITY sio PERFORMANCE. Maana kuna wengine wana akili kubwa ila hawajawekewa mazingira ya kuzitumia kwa ukamilifu wake so tunapojadili tuwe nalo hili kichwani.

Naomba kuwasilisha
Cc
Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Wick Dukeson lifecoded Daimler monde arabe mtu watu
Daaaah...umenitag mkuu...!! aya bana ..

But hongera kwa maada fikilishi...

lakini nataka nichangia mada hii katika analysis ambayo inaweza isiwe imebase na jinsi wengine wanavyoweza kuchangia kwa facts za lishe bora pamoja na genetic influence kutoka kwa wazazi hasa mama...

Mpaka sasa bado jopo la madakatri hasa Neural scietists pamoja na psychiatrists ambao kazi yao kubwa ni kucheza na cognitive brain function ambayo inahusisha eneo moja pekee la ubongo lijulikanalo kama Prefrontal cotex ....

Wanasema kuwa Cognitive function ya ubongo( sehemu inayohusika na uelewa katika ubongo wa mwanadamu) ipo under neural circuit guided na Neural transmitter nyingi sana including Dopamine,Noradrenaline,Adrenaline yenyewe,serotonin,melatonin,GABA, pamoja na zinginr kibaoa ambayo utendaji kazi wake upo Antagost au agonizing zaid kutegemea na hitaji la ubongo au akili katika kutenda...

Kuna neurol transmitter hapo zinahusika na mambo ya firing au kuruhusu transimssion ya impulse kwa speed kubwa sana na zingine zinahusika na kudhibiti high neural firing rate hence zinazuia impulse rate changes katika specific part ya ubongo ...

Ukisoma mambo ya Dopaminergic pathways hapa unaweza ukaelewa ninachoongelea...

Twende kwenye mada yenyew what guides intelligence to a singular person ..??

Kuna kitu kinaitwa CPH4 ( 6-carboxytetrahydropterin synthase) hii ni enzymes ambayo mara nyingi inahusika na conversion snyingi sana ambazo huwa zinagive out Queuosine, ambayo ni component muhimu sana katika kuincrease neural firing ratio ya chemical maalumu ambazo zinahusika na prefrontal cotex capacity inayohusika na mambo ya cognitive function ya brain hasa maeneo ya limbic system ,amygdala na mengine ambayo yanahusika na memory pamoja na Intelligence brain centre...

Ili mtu tuseme kuwa ana akili nyingi sana au ana Intelligence kubwa ni lazima eneo flani la ubongo lazima liwe busy sana anapokuwa anafikilia au kufanya mazungumzo juu ya swali aliloulizwa...

Madaktari kutoka Armstadam ,Netherland walifanya jaribio moja kwa kutumia Electroencephalogram (EEG) kupima brain hyperactivity wakati mtu anapokuwa kwenye maswali magumu yanayomfanya mtu afikilie sana ila wakaja kugundua kuwa ni eneo moja tu la prefrontal cotex ndo lilionekana kuwa busy snaa wakati wa kufikilia...pia eneo hili ndilo linalohusika na mambo ya kuactivate brain function hasa mtu akiwa bado mdogo sana,,,consider about Mutism spectrum disorders kwa watoto wadogo ambao ni moj wapo ya mental disorder amabyo inawapata watoto wanapozaliwa na mara nyingi huathiri cognitive behavioral pattern ya mtoto husika.

Hivyo iliwafanya waanze kuchunguza zaidi why eneo lile ..Ila cha kushangaza walikuja kugundua kuwa eneo hilo ndo lilikuww na high neural firing rate za neural transimtter ambazo zinahusika zaidi na mambo ya cognitive function...siyo kila neural transmitter( vichocheo katika ubongo) inahusika na cognitive function...

Unaweza ukawa na high level ya dopamine( katika manic episodes) lakini ukawa na low cognitive function na mwingine akawa na high dopamine neural firing rate lakini akawa na cognitive function kubwa snaa zaidi kuliko mwingine despite wote wapo manic episode au Bipolar conditioned state...

Ukitaka kuelewa zaidi hapa nenda magaereza ya wafungwa ambao ni wagonjwa ndo utaelewa ninachozungumza hapa kuwa kuna vichaaa utakuta uwezo wake upo juu sana yani kawa geniuz mpaka karun mental disability ila ana high IQ score na mwingine ni mgonjwa wa vile vile bipolar lakini ni mbumbumbu wa kutupa though wote wana high level za dopamine...

Kwa hiyo dopamine sio kigezo sana za kujudge intelligence ...we need something else...

Sas kuna hiyo chemical substance ambayo inaitwa CPH4 ambayo mara nyingi watu wa Neural molecular science hawataki kuweka wazi na wanasema kazi yake bado haijagundukika lakini sio kweli kazi yake inafahamika na ndio chemical wanayoitumia hasa kupima ya Intelligence ya mwanadamu kuanzia akiwa tumboni kwa mama( Embryology) mpaka anapofikisha miaka 25 ...

Inasemekana kuwa japo ni kweli kuwa mama mjamzito akiwa na umri wa mimba ndani ya week 6 ndipo hormone hiyo au chemical hiyo huzalishwa kwa lengo la kwenda kuhimiza utengenezaji wa capacity ya kutosha ya neural circuit receptors kwa ajili ya high firing rate ya imuplse katika specific cognitive brain centre...

Ifahamike kuwa ubongo wa mwanadamu hutengenezwa mtoto akiwa na umri wa week 4 tumboni kwa mama yake kwa hiyo ubongo ukianza kutengenezwa tayari mwili wa mama unasense kuwa tayari ubongo wa mtoto umeanza kutengenezwa na tayari mwili wa mama unaamliwa kuanza kutoa hizo chemicali aina ya CPH4 ambazo zinaenda moja kwa moja kwa mtoto kwa ajili ya kuenhece cerebral formation hasa cognitive area ambalo kazi yake kubwa ni kujenga neural firing receptor za kutosha ili ubongo uwe na high receptors za hizo neural transmitter kwa ajili ya kuprocess information za kutosha katika eneo husika kwenye ubongo kila unapogundua kuwa hilo wazo linatakiwa lifanyiwe kazi katika eneo flani la ubongo basi taarifa muhimu inapelekwa kule kwa speed kubwa sana ambao ni millsecond ndani ya millsecond na tayari cognitive centre inainterprete kuwa hicho kitu jawabu lake ni hili...

The difference in Intelligence between us ni kwa sababu tunazidiana neural firing rate ya taarifa kufika eneo husika kwa muda mfupi sana na kufanyiwa interpretation yake..

Mtu ambaye ni Genius ana high neural firing rate kuliko mtu wa kawaida...manake nini...??

Kuna kitu kinaitwa processor,hiki ndo kifaaa kinachospeed up rate ya taarifa kusafili kwa haraka zaidi kwenye electronic component yoyote..ndo mana hata ubora wa komputer ni processor pamoja na RAM....manake nini kama Laptop au computer yako ina processor ndogo lets say 1.7 GHZ manake utakuwa kila ukiclick file lifunguke linachukua sekunde 4 ndo linafunguka lakini mwenye processor ya 2.7 GHZ akiclik inafunguka ndani ya fraction of second...processor ndo kila kitu ...

Same applied kwenye ubongo wa mwanadamu kinachomfanya mtu aww na upeo mkubwa wa kufikri na kupata jawabu lililo sahihi ni uwezo wa taarifa kufika eneo husika kwa haraka zaidi kisha kufanyiwa interpretation iliyosahihi ndani ya muda ule ule na taarifa zake kupelekwa kwenye cognitive centre kwa ajili ya kumfahamisha mwanadamu kuwa anachowaza au kuhisi ni hiki hapa ...

So kila mwanadamu ana ubongo ule ule the difference is the CPH4 level ambayo inahusika na kutengeneza more brain circuit kwa ajili ya impulse transduction na hapo ndipo hata anatomy(umbo katika physical morphology) ya ubongo huwa ina ratio tofauti za Gyrus na sulcus ambazo ndo zinazoupa ubongo folding morphology kuincrease surface area ya neural firing rate ...

So the level of CPH4 Itaendelea kuwa maintained mpaka pale ubongo utakapokuwa umekamilika...kwa hiyo kama productiom ya hormone hizo ikiwa ndogo basi hata uwezo wa akili wa mtoto unakuwa hafifu ..ndo mana tunasema mama ndo mtu pekeee anayechangia Intelligence ya mtoto na sio baba( hapa katika percent ratio mama anakuwa na nafasi kubwa)..

So kama ukitaka kumaintain high brain au cerebral capacity ya mtoto inabidi mama aproduce high level ya CPH4 during pregnacy kulikoa wakati akiwa ananyonyesha japo huwa ipo kwa kiwango kidogo snaa kwenye colostrum( maziwa ya mwazo kabsa ambayo mtoto hatakiwi kukosa)..

Lakina kuna study zilifanyika miaka ya nyuma na kugundua kuwa mwanadamu wa sasa ( tulio wengi) tunatumia only 10% ya cerebral capacity kisha 90% ya ubongo wetu haufanyi kazi na ikasemekana kuwa laiti binadamu angelitambua hilo kuwa yeye ni infirnity and Immortal basi angeweza kuraise energy na anaweza kuexpand cerebral capacity mpsaka hata 40% kisha anaweza akadevelop some features kama Telekinepathy, psychopathy abilities ambapo anaweza akafungua mambo mazito yaliyo nyuma ya ulimwengu huu na kisha kumfanya aanze kuiview universe katika 8 dimension state....kadri anavyoascend kwenye 100% ndipo uwezo wake unabdilika kwa kasi kubwa sana na anaweza akawa na nguvu ambazo ni uncontrolled =====pengine ndo mana serikali hazitaki kufundisha elimu ya kuraise CPH4 hasa kwa binadamu wa kawaida kwa sababu madhara yake ni makubwa sana.

Nchi za wenzetu wameweza atleast kujua namna ya kummonitor mama mjamzito hasa kuepuka stress wakati wa ujauzito kwani stress ni factor moja kubwa sana inayozuia production ya CPH4 na kumfanya mtoto anakuwa tumboni katika low level ya cerebral capacity formation hence anakuja kuwa na low IQ japo vyakula na lishe bora zinaweza kuboost lakini kwa kiwango kidogo sana....

Lakini pia kama wewe ni mdau wa kufuatilia mambo ya human cloning hasa kupitia project yake ya Maffin project and human cloning kupitia process za somatic-cell nuclear transfer au pluripotent stem cell induction basi hutumia normalizimg ratio ya CPH4 .Lakini pia kisha ukasoma hizo documentaries na scientific writtings zinazoelezea jinsi mradi huo wa siri wa kutengeneza exactly copy wa kiumbe unaemtaka bila kubadili chochote utagundua kuwa wanatumia technolojia under the help ya hizo chemicals hasa during blastula formation wanainduce the same ratio ya CPH4 kwenye morula ya yule clone kwa kufuatisha ratio alizonazo yule recipient wake...

Kabla ya kufanyiwa clone wake unapimwa kwanza cerebral capacity in relation ta CPH4 level kisha ndo anatengenezwa clone wako ambayo atakuja kuwa na Intelligence ile ile uliyokuwa nayo before ..

Forget about human cloning now make sio mada husika...ina nafasi yake..japo ipo siku nitaidondosha hapa rasmi...

kwa mara ya kwanza maabara ya The Thomas J. Watson Research Center. ambayo ilipata kashikashi kwa kuuza taarifa za kimolecular za CPH4 katika maabara kuu tatu ambazo ni ni Argonne National Laboratory,Oak Ridge National Laboratory pamoja na The Center for Integrated Nanotechnologies (CINT) kisha taarifa hizo kuuzwa wa badhi ya director mmoja ambapo kulipelekea kuelezea kazi ya chemical hiyo kwenye movie ya Lucy( 2010) japo usiri umeendelea kutawala zaidi juu ya uwezo au Intelligence ya mwanadamu...

kuna study nyingi zimefanyika kupima kiwango cha CPH4 kwa kina mama tofauti wakiwa wajawazito na kupima Intelligence outcome ya watoto wao na kukuta kuwa kulikuwa na utofauti mkubwa snaa depending na blood chemical level...

Nahitimisha kwa kusema kuwa Intelligence ya mwanadamu imekuwa ni swala gumu sana kulielewa kwani mambo mengi yanakuwa siri nzito sana....

wachache wanatuendesha watakavyo na huenda Nanotechnology ikaja kusolve hiyo paradoxy...

Asanteni...huo ndo mchango wangu kwa mwenye kung'amua machache unaweza fuatilia zaidi hasa kwa kusoma mambo ya Neural science in relatiom to neurotransmitter receptors that govern human Intelligence nadhani utajifunza mengi kuliko hata niliyoelezea .
PhotoGrid_1541284145239.jpg
PhotoGrid_1541284280399.jpg
 
Tuna kusubili mzee wa msata
Karibu sana mkuu utupe maoni yako
Kuna uhusiano mkubwa sana wa akili/ kukosa akili na kizalia (genes) au vinasaba.... Familia ya ma genius always hutoa ma genius na familia za wapumbavu always hutoa wapumbavu
Zamani wafalme na watawala walkuwa watu wa kaliba fulani (royal families) na hawakupenda kabisa kuchanganya damu ili kuepuka contamination... Familia ya uingereza ya malkia na Princess Diana ni mfano mmojawapo wa wazi
Zile familia za wapumbavu.... Mifano rahisi kabisa tunayo hapa nchini... Familia nzima hakuna aliyevuka std 7 au form four na maisha yao ni dhiki tupu... Hawa hutamani mno wachanganye damu ili walau kuwe na unafuu
 
kwamba familia tulionayo hapa ....nimecheka sana...

Lakini mkuu Ukiongelea familia ya Princes Diana ni familia yenye utata kidogo hasa genetic configuration zao...

Genetic configuration zao ipo tofauti kabisa na wengine na source ya ile familia ni kutokana na uzao fichwa wa Royal family...

Lakini swali jingine nashindwa kuelewa kwanini sasa aliachana na mume wake Charles, Prince of Wales kama kweli walikuwa ni selected royal family members na lengo lao ni kutunza geneology yao...??

Swala hili la Intelligence inheritance linaleta maswali mengi sama hasa namna passage ya intelligence genes na kuna baadhi ya jamiii( mfano taifa la Israel linasakika na kuwa na passage tata ya geneology yake kupitia mataifa mengine...hapa napo bado sijapata source ya kueleweka kuwa kwanini hybrid pure ya Jewish inakuwa ngumu kuwa passed into other mataifa ...!!
 
Labda niendelee kuuliza, hizo CPH4 zinazalishwa kutokana na nini ndani ya ubongo?
hiyo ni outomatic gene switch inayompa taarifa mama kuwa mwili wake sasa uanze kutengeneza CPH4 pale tu ubongo unapokuwa unaanza kutengenezwa kuanzia week ya 4 ya embryology...
 
Unakumbuka nyoka alimpata Adam kupitia Eva? Mwanamke ni kiumbe dhaifu kiroho kwa mtazamo wa kushawishiwa lakini pia ni kiumbe chenye nguvu kwa mtazamo wa kushawishi
 
Unakumbuka nyoka alimpata Adam kupitia Eva? Mwanamke ni kiumbe dhaifu kiroho kwa mtazamo wa kushawishiwa lakini pia ni kiumbe chenye nguvu kwa mtazamo wa kushawishi
ndo mana mwanamke anatumika kama weapon ya kila aina ya mission assigned kufanyika mahala...

Ni kiumbe anayehamisha attention ya mind ya masculine energy....

Lakini ndo kusema kwamba feminine energy ina nguvu zaidi kuzidi masculine energy au utendaji kazi unakuwaje hapa...??

kuna kitabu kimoja sikumbuki jina niliwahi kusoma ilikuwa inaelezea at what occassion feminine energy ina mask masculine energy japo masculine energy ina strength kubwa sana....

Natamani kujua kwa undani zaidi kwanini mwanamke ni kiumbe dhaifu lakini feminine inamuweka sehemu( rank ya juu sana) katika mindset shift kwa mwanaume..
 
Hapa kwenye power of energy inategemea anatumikaje kuna situation mbili hapa... Kutoka... Kwenda....! Na kwenda... Kutoka... Kuna mahali anakuwa weak...na kuna mahali anakuwa superior... To convince and to be convinced!
 
sawa kabisa...
 
hiyo ni outomatic gene switch inayompa taarifa mama kuwa mwili wake sasa uanze kutengeneza CPH4 pale tu ubongo unapokuwa unaanza kutengenezwa kuanzia week ya 4 ya embryology...
Mkuu kulingana na maelezo yako naona yanajenga picha kuwa urithi unahusika pia kwa asilimia kubwa

Nikiwa na maana kama mama ndiye mtoaji wa hiyo vichocheo/kemikali ya CPH4 na kwamba kuna wakati anaweza kuwa na upungufu juu yazo na kupelekea kusababisha madhara kwa kiini tete_basi ni wazi yeye ndiye Mungu wa akili

Na kama ni hivyo Tunapaswa kuangalia wapi unapanda mbegu mashamba mengine siyo

Ila bado ina ukakasi wa utengefu wa kijamii

Lakini vilevile kama hiyo CPH4 ni kakompaundi basi fulani basi lishe pia naona kama inahusika vilevile Mkuu_ si unajua Mwili ni kama nyumba lazima kuwe na kaupem uzi ka matilio husika kwa kazi maalumu

Maoni yangu sijui kama nimekuelewa vizuri....
 
ni kweli mkuu....Lishe inaplay part kiasi hasa knowledge activation lakini swala la Intelligence linabaki kuwa lina factor control kubwa...

Kumbuka kuwa tunaposema Intelligence ,we speak about something inborn ability to solve the circumstances surrounding human being..

Unapozungumzia Knowledge ,we speak about Acquired ability rather than inborn ability....

Kuna mchango mkubwa sana wa Lishe bora hasa miezi mitatu (3) ya kwanza ya mama akiwa mjamzito( First trimester) kuliko mchango wa lishe bora kuanzia 2rd na 3rd trimesters...

Hata study nyingi zimefanyika na zimebaini hilo kuwa miezi ambayo ubongo unatengenezwa kumeonekana impacts kubwa ya lishe kuathiri au ku alter Intelligence ya mtoto kwani zile amino acids muhimu zinazohusika na brain formation huwa zinakuja kuplay part kubwa sana mama atakapoanza kutoa CPH4 katika 4 weeks of gestation...

Pengine lishe bora huongeza gene switch za kutosha na kuruhusu production ya hizo hormones zinazohusika na utengenezahi wa maeneo muhimu kwa ajili ya cognition ya human being...

Kuna study ilifanyika pia ya kucompare mtoto anayezaliwa katika familia yeneye Intelligence kubwa na mtoto anayezaliwa kwenye familia yenye Intelligence ndogo ila wakamsubject mama ambaye anakadiliwa kuwa na Intelligence ndogo na lishe bora ili waangalie effects ya lishe bora kwenye low intelligence continuum lakini walikja kuona kuwa mtoto alizaliwa akiwa na improved Intelligence compared na mama yake au ndugu zake wengine lakini hakuweza kumfika yule ambaye kaziliwa na mama ambaye Intelligence continuum ipo kubwa snaa...

Na conclusion iliyofikiwa ni kwamba Intelligence is the Inborn ability and is more dependent on pre existance genetic trait ya wazazi wenu though Lishe bore inakuja kuplay part kwenye knowlege capacity ya mtu ...

Manake nini ...lishe bora inafavour zaid mtu kupata uwezo wa ku master knowlege zaidi kuliko kuenhence Intelligence yake...

we can say that Diet affects knowlege by 75% but it affects Intelligence by 25% .

Sijui kama utakuwa umenielewa nilichokiongelea mheshimiwa...

Unajua utofauti kati ya knowledge na Intelligence ni mkubwa sana na watu ni ngumu kutofautisha...mtu ambaye ana Intelligenxe kubwa ku master knowlege ya kitu ni rahisi sana...kwa hiyo lishe inamfanya mtu awe mwepesi wa kupata knowledge outside his mind ndo anaelewa....ndo mana hata darasana mwalimu anafundisha topic flani kuna wanaomwelewa pale pale na hawawezi kusahau tena juu ya kile kitu ambacho walikuwa hawakifahamu na hao ndo tunasema wana knowledge kubwa ...ila kuna wengine ambao anachokifundisha mwalimu wao tayari washakijua hata atakachosema mwalimu meaning that they have more intelligence compared to others. ...

Lakini mule mule darasani kuna watakaoelekezwa kitu kipya na bado watashindwa kumaster uelewa ule kwa muda mrefu,yani wao kusahau ni rahisi zaidi...na hawa ndo tunasema wana knowledge ndogo..same applies kwenye intelligence yao ni ndogo pia..

Sijui kama unanipata mkuu
 
ni kweli mkuu....Lishe inaplay part kiasi hasa knowledge activation lakini swala la Intelligence linabaki kuwa lina factor control kubwa...

Kumbuka kuwa tunaposema Intelligence ,we speak about something inborn ability to solve the circumstances surrounding human being..

Unapozungumzia Knowledge ,we speak about Acquired ability rather than inborn ability....

Kuna mchango mkubwa sana wa Lishe bora hasa miezi mitatu (3) ya kwanza ya mama akiwa mjamzito( First trimester) kuliko mchango wa lishe bora kuanzia 2rd na 3rd trimesters...

Hata study nyingi zimefanyika na zimebaini hilo kuwa miezi ambayo ubongo unatengenezwa kumeonekana impacts kubwa ya lishe kuathiri au ku alter Intelligence ya mtoto kwani zile amino acids muhimu zinazohusika na brain formation huwa zinakuja kuplay part kubwa sana mama atakapoanza kutoa CPH4 katika 4 weeks of gestation...

Pengine lishe bora huongeza gene switch za kutosha na kuruhusu production ya hizo hormones zinazohusika na utengenezahi wa maeneo muhimu kwa ajili ya cognition ya human being...

Kuna study ilifanyika pia ya kucompare mtoto anayezaliwa katika familia yeneye Intelligence kubwa na mtoto anayezaliwa kwenye familia yenye Intelligence ndogo ila wakamsubject mama ambaye anakadiliwa kuwa na Intelligence ndogo na lishe bora ili waangalie effects ya lishe bora kwenye low intelligence continuum lakini walikja kuona kuwa mtoto alizaliwa akiwa na improved Intelligence compared na mama yake au ndugu zake wengine lakini hakuweza kumfika yule ambaye kaziliwa na mama ambaye Intelligence continuum ipo kubwa snaa...

Na conclusion iliyofikiwa ni kwamba Intelligence is the Inborn ability and is more dependent on pre existance genetic trait ya wazazi wenu though Lishe bore inakuja kuplay part kwenye knowlege capacity ya mtu ...

Manake nini ...lishe bora inafavour zaid mtu kupata knowlege zaidi kuliko kuenhence Intelligence yake...

we can say that Diet affects knowlege by 75% but affects Intelligence by 25% .

Sijui kama utakuwa umenielewa nilichokiongelea mheshimiwa...

Unajua utofauti kati ya knowledge na Intelligence ni mkubwa sana na watu ni ngumu kutofautisha...mtu ambaye ana Intelligenxe kubwa kumastee knowlege ya kitu ni rahisi sana...kwa hiyo lishe inamfanya mtu awe mwepesi wa kupata knowledge outside his mind ndo anaelewa....ndo mana hata darasana mwalimu anafundisha topic flani kuna wanaomwelewa pale pale na hawawezi kusahau tena juu ya kile kitu ambacho walikuwa hawakifahamu na hao ndo tunasema wana knowledge kubwa ...ila kuna wengine ambao anachokifundisha mwalimu wao tayari washakijua hata atakachosema mwalimu meaning that they have more intelligence compared to others. ...

Lakini mule mule darasani kuna watakaoelekezwa kitu kipya na bado watashindwa kumaster uelewa ule kwa muda mrefu,yani wao kusahau ni rahisi zaidi...na hawa ndo tunasema wana knowledge ndogo..same applies kwenye intelligence yao ni ndogo pia..

Sijui kama unanipata mkuu
Nimekupata mkuu usijali

Nilishindwa kutofautisha kati ya knowledge na intelligence

Unajua katika imani yetu ya kibudha tunaamini katika milango nane ya ufahamu So haijanipa tabu

Basi nitaiweka knowledge katika sehemu ya mlango wa Sita unaohusikana na ufahamu (mental)

Na intelligence nitaiweka kwenye sehemu ya mlango wa saba (Manas) the general

Halafu mambo yanaenda

Ila mkuu nimeona juu umegusia kidogo kuhusiana hisi za mama mjamzito kwamba anapokuwa disponted na jambo fulani inaweza ikazuia uzalishaji wa hicho kichocheo cha CPH4

Ikiwa na maana kama Baba hajui kupetipeti inaweza kuleta shida_ si ndio...?

Je Huoni kwamba hii inaweza kuingilia utendaji wote na kumpa mama mamlaka ya ugawi wa ufahamu kuliko inavyohusika baba

Kiasi kwamba tunaweza kubadili defnition ya intelligence na kuipa maana ya tabasamu la mama ndio kuwa kila kitu ...unaonaje hii.?
 
ha ha ha kabsaa mkuu....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom