Inaweza kuwa kweli marehemu Hamza alikuwa gaidi, lakini ukweli utabaki kuwa kweli. Jeshi la polisi linafanya uonevu mkubwa kwa Watanzania

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Kwa namna jeshi la polisi linavyodili na watuhumiwa wa uhalifu hapa nchini basi ifikie hatua tusiwe na chombo kinachoitwa mahakama.

Maana mtu akituhumiwa kwa wizi wa aina yoyote kabla ya kufika mahakamani lazima apate kipigo na mateso makubwa akiwa chini ya jeshi la polisi.

Ni kweli kabisa taifa linatakiwa lisiwe na uhalifu wa kila namna. Lakini hii haiwezekani maana uhalifu ni kitu natural. Ndio maana kuna mtu anazaliwa kibaka tu. Sasa kama kazaliwa kibaka ndio apigwe na kuteswa ndani ya kituo cha polisi?

Achana na wanaoteswa na kupigwa. Je wanaodhurumiwa mali zao? Hao ndio wengi maana ukikamatwa na polisi wakijua una mali au pesa basi sahau.

Mbaya zaidi maovu ya askari polisi huwa yanafumbiwa macho na viongozi wa taifa hili.

Uhalifu ni suala lisilotakiwa hapa nchini. Lakini uhalifu utazuiwa kwa kuwa na jeshi la polisi linalodhulumu haki za raia wa kila namna? Maana kwa polisi wa Tanzania uwe na makosa au huna makosa basi wese ni mtu wa kudhulumiwa haki.

My take: Dhuluma ya polisi dhidi ya raia imetengeneza chuki kubwa sana dhidi ya IGP Sirro.
 
Ni majambazi ndio huwa wanachezea kipigo sio kila mwizi tu. Pili sio inawezekana ukweli ni kwamba Hamza ni gaidi sababu hata wakati anafanya lile tukio alisema anafanya kwa ajili ya dini.
 
Ni kweli jeshi la polisi Tanzania limejaa uonevu, hilo liko wazi.

Lakini hilo halihusiani na hamza kua gaidi, hamza alikua gaidi na hilo liko wazi wala halihitaji mabishano.
Wewe una hakika kuwa Hamza alikuwa gaidi??
 
Jeshi la Polisi la Tanzania ni mirror image ya Serikali ya CCM iliyopo madarakani kwa sababu jeshi hilo lipo chini ya Serikali hiyo.Serikali ya CCM haiwezi kujivua lawama kwa jeshi la Polisi Tanzania kuoza.
 
Kwa namna jeshi la polisi linavyodili na watuhumiwa wa uhalifu hapa nchini basi ifikie hatua tusiwe na chombo kinachoitwa mahakama.

Maana mtu akituhumiwa kwa wizi wa aina yoyote kabla ya kufika mahakamani lazima apate kipigo na mateso makubwa akiwa chini ya jeshi la polisi.

Ni kweli kabisa taifa linatakiwa lisiwe na uhalifu wa kila namna. Lakini hii haiwezekani maana uhalifu ni kitu natural. Ndio maana kuna mtu anazaliwa kibaka tu. Sasa kama kazalisa kibaka ndio apigwe na kuteswa ndani ya kituo cha polisi?

Achana na wanaoteswa na kupigwa. Je wanaodhurumiwa mali zao? Hao ndio wengi maana ukikamatwa na polisi wakijua una mali au pesa basi sahau.

Mbaya zaidi maovu ya askari polisi huwa yanafumbiwa macho na viongozi wa taifa hili.

Uhalifu ni suala lisilotakiwa hapa nchini. Lakini uhalifu utazuiwa kwa kuwa na jeshi la polisi linalodhulumu haki za raia wa kila namna? Maana kwa polisi wa Tanzania uwe na makosa au huna makosa basi wese ni mtu wa kudhulumiwa haki.

My take: Dhuluma ya polisi dhidi ya raia imetengeneza chuki kubwa sana dhidi ya Igp Sirro.
Tii sheria za nchi,heshimu mamlaka,utaishi kwa amani.
 
Wewe una hakika kuwa Hamza alikuwa gaidi??
Ndio.

Kwanza ameonekana kwenye video clip akitamka mwenyewe, hilo liko wazi.

Pili, kwa kua alitamka mwenyewe dakika chache kabla hajafa, huo ni ushahidi wa moja kwa moja na ushahidi mzito unaothibitisha hamza alikua gaidi.

Tatu, Matendo ya hamza yanathibitisha ugaidi wake.
 
Ni kweli jeshi la polisi Tanzania limejaa uonevu, hilo liko wazi.

Lakini hilo halihusiani na hamza kua gaidi, hamza alikua gaidi na hilo liko wazi wala halihitaji mabishano.
Tunaomba taarifa kamili ili kila mmoja wetu aweze kuujua ugaidi wake kikamilifu,vichocheo vilivyopelekea kuwa gaidi na mazingira vichocheo hivyo.
 
Tunaomba taarifa kamili ili kila mmoja wetu aweze kuujua ugaidi wake kikamilifu,vichocheo vilivyopelekea kuwa gaidi na mazingira vichocheo hivyo.
taarifa kamili subiri utaipata,kwa sasa chain inaunhwa kwanza.
 
na hapo ndipo huwa nawalaumu wanaharakati maandazi wa jf na twitter,wako uchi mno hawana lengo wala mission juu ya wananchokipambania.

hamza ameua askari,mbali na kwamba askari mara nyingi wamekua si watendaji wema bado hakuna uhalali wa hamza kufanya alichokifanya,maana si msimamo chama wala harakati zenu kuua polisi,alitakiwa akemewe kwa kulaani sana.kinyume chake mnafurahi,upuuzi mkubwa huu.

hakuna anayemjua hamza zaidi ya ccm wenzake kwa uchache,nduguze kiasi fulani na yeye mwenyewe kwa ujumla.kwanini muungane naye ktk vita ambayo yeye mwenyewe haamini katka mnachoamini yeye anaamini katika kumpigania allah!!!!upumbavu mwingine mkubwa.

ilifaa kulaani alichofanya at first stape,kisha kuomba uchunguzi huru kuujua undani wake,busara na utashi ungeonekana kati yenu hapa.kwenye hili hata ndugu wameonyesha tofauti kubwa sana na wanaharakati,maana wao wamekuwa wakikaririwa wakisema wanashangaa ndugu yao amekuwaje!!!

yote kwa yote ishara za ugaidi kwa hamza zina nguvu zaidi kuliko hoja ya kuporwa haki kabla.
 
Back
Top Bottom