Jeshi la Polisi linapokosa weledi linageuka kuwa chanzo cha taharuki

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,063
Tungekuwa tupo katika nchi zilizostaarabika, wakati huu, uongozi wote wa Jeshi la Polisi ungekuwa umeshaondolewa kwa mambo ya ajabu yanayofanywa na jeshi hili yanayoashiria kukosekana kwa weledi ndani ya chombo hiki.

Jeshi la Polisi linapofanya kazi ya kuwatengenezea watu kesi za kubumba ili kuwatesa na kuwaumiza, linakuwa halina tofauti na kikundi cha kigaidi. Jeshi la Polisi, kinyume na matakwa ya sheria iliyoanzisha jeshi hili, limegeuka na kuwa kikundi cha kuwatisha watu wasikemee uovu au makosa yanayofanywa na dola dhidi ya umma.

Inawezekana vipi ndani ya jeshi zima wakosekana watu ambao wanaelewa hata tafsiri tu au vitendo na mazingira ya mtu kuweza kufanya ugaidi?

Huko siku za nyuma, wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi, mchungaji Mtikila, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, akiwa anapinga muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya watu kwenye viwanja vya Jangwani, aliwahi kunena.

"Huyu Rais Mwinyi ambaye ni tx, tunamwambia aende kwao. Hivi hajui nini hutokea watu wanapokataa kutawaliwa? Watanzania ni watu wa amani, tunataka Mwinyi arudi mwenyewe, hatutaki arudi akiwa kwenye jeneza. Watanganyika hawataki kutawaliwa na Tx. Wanasema kuwa sisi ni wa damu moja, wamasai wa Kenya na Tanzania, siyo wa damu moja? Wakurya wa Tarime na wa Kenya, siyo wa damu moja? Kwa ninj hatujawa nchi moja?"

Lakini kauli yake wala haikuwahi kutafsiriwa kuwa ni uhaini. Sababu ni moja, kwa sababu hakukuwa na vitendo wala mazingira yalioshiria kuna nia ya kumwondoa Mwinyi madarakani kwa mapinduzi au kuundoa uhai wake kwa njia yoyote ile ya kupangwa. Na hatukuwahi kusikia mtu yeyote akishtakiwa kwa makosa ya ugaidi au uhaini, nadhani ni kwa sababu wakati huo ndani ya jeshi la Polisi kulikuwa na viongozi waliokuwa na weledi, tofauti na sasa.

Mtu kutamka, "matendo haya ya uuzwaji wa rasilimali za nchi, yakifanyika katika nchi nyingine, Serikali au Rais anaweza kupinduliwa", haiwezi kuwa ni uhaini. Hii ni kauli ya tahadhari. Lazima uwe mjinga sana kuamini kuwa kauli ya tahadhari ni uhaini. Kauli ya tahadhari inawezaje kumwondoa Rais madarakani?

Hivi mtu akikuambia kuwa ukinywa sumu unaweza kufa, maana yake anataka kukuua?

Chini ya katiba mbaya tuliyo nayo, tumeona jinsi utendaji wa Jeshi la Polisi ulivyo mbaya. Tupiganie katiba mpya. Kwa uzoefu wa utendaji mbaya wa Jeshi la Polisi ambao tunaushuhudia, katiba mpya iangalie namna nchi itakavyoweza kuwa na Jeshi la Polisi lenye weledi na litakalofanya kazi kwa kuzingatia sheria zote za ndani ya nchi na za kimataifa. Tukiendelea na jeshi la namna tuliyo nayo, kuna wakati wananchi watashindwa kuvumilia, hivyo watachukua hatua dhidi ya chombo hiki kisichotambua majukumu yake na kinachofanya kazi bila kuzingatia sheria, bali kwa utashi na matakwa ya watawala.
 
Mna propaganda za kijinga sana. Aliyewanyika wa Tz elimu alikosea sana. Temebaki na elimu za kukariri tu!
 
NCHI YETU ni masikini mno .
" Hakuna UMASIKINI MBAYA kama umasikini wa FIKRA".
JK NYERERE.

KIBAYA ZAIDI NCHI NYINGI AFRIKA ZILIPATA UHURU WAAKE MAPEMA BILA YA KUWA NA UWEZO WA KUJITAWALA.

Tumeishia kuwa.
Masikini.
RUSHWA.
UFISADI.
Vita.
Migogoro nk.

POLE SANA AFRIKA
POLE MNO MAMA TANZANIA.

#ngozi ya Ttako.
 
Ukitazama vizuri utaona kabisa, wanachokifanya polisi kwa sasa, ni kujaribu kutafuta njia nyingine ya kumnasua Samia na balaa alilosababisha mwenyewe.

Walianza kuwatumia chawa, wengine wakapewa nauli, wakaenda Dubai kufanya ziara kwenye kampuni, wakaipamba walivyotaka, lakini watanganyika wakagoma kuwaelewa.

Wakafuata UVCCM na matamko yao, wataandamana nchi nzima kumuunga mkono Samia kwa usaliti wake kwa watanganyika, wakajua wakifanya hivyo, ndio wataamsha hasira zaidi kwa watanganyika, wakaacha igizo lao.

Wakaja kuzunguka huko mikoani wakina Kinana na Chongolo, nao kujaribu kuuzima moto uliowashwa na Samia, mpaka mmoja akakiri mkataba ule unahitaji marekebisho, lakini bado watanganyika wamegoma kuwaelewa.

Baada ya njia zote hizo kufeli, sasa ndio wameamua kulitumia jeshi la polisi, wakaenda studio kutengeneza kipande toka kwenye maneno aliyowahi kuzungumza Dr. Slaa kwenye interviews zake, ili kuhalalisha madai yao dhidi yake.

Kwa hili nina hakika, napo wamefeli, huu moto utaendelea kuwaka mpaka pale yule aliyeuwasha kwa ujinga wake mwenyewe, atakapoamua kuuzima kwa mikono yake, kwa kuuvunja ule mkataba wa kishetani alioingia na waarabu.
 
Kauli zozote zinazohatarisha usalama na amani ya nchi hazitavumiliwa.
Tatizo mnakosa uelewa hata wa kutambua ni ninj kinahatarisha usalama wa nchi.

Hata siku moja anayekosoa wizi, rushwa, mikataba ya hovyo na ufisadi, hawezi kuwa ndiye anayehatarisha usalama wa nchi. Anayehatarisha usalama wa nchi ni anayeiingiza nchi kwenye mikataba ya hovyo kutokana na kurubuniwa.
 
NCHI YETU ni masikini mno .
" Hakuna UMASIKINI MBAYA kama umasikini wa FIKRA".
JK NYERERE.

KIBAYA ZAIDI NCHI NYINGI AFRIKA ZILIPATA UHURU WAAKE MAPEMA BILA YA KUWA NA UWEZO WA KUJITAWALA.

Tumeishia kuwa.
Masikini.
RUSHWA.
UFISADI.
Vita.
Migogoro nk.

POLE SANA AFRIKA
POLE MNO MAMA TANZANIA.

#ngozi ya Ttako.
Pia machaww
 
Mna propaganda za kijinga sana. Aliyewanyika wa Tz elimu alikosea sana. Temebaki na elimu za kukariri tu!
Ni kweli, wengi mmekosa elimu na akili. Mmekaririshwa kuwa Rais hakosei, hakosolewi na yupo juu ya sheria. Nanyi mmebakia kasuku wa kuziimba nyimbo hizo.
 
Back
Top Bottom