Mkuu wala usiendekeze upuuzi wa kumpa mwanamke hata mia yako.
Mimi nimewahi kukumbwa na kadhia kama hiyo, kila siku mizinga mara sijala mara nauli mara sikukuu n.k.. Mwisho wa siku ukimtumia kiasi alichoomba anakuuliza "mbona hujatuma na yakutolea?"
Nimekuja ku realize kuwa ni upumbavu mkubwa tunafanya sisi wanaume. Kuliko umtumie shilingi 50,000/- mwanamke asiekuwa na shukrani wala upendo wowote, ni heri utoe hapo 20,000/- utume kwa wazee wako wanunue hata sukari na chumvi wakukumbuke katika maombi yao na upate kubarikiwa katika mishe zako. Hiyo iliyobaki 10,000/- toa sadaka masjid/kanisani. 20,000/- kula maisha..
Hapo utakuwa umejitendea haki mwenyewe, wazee wako umewathamini na watakuombea mafanikio na Mungu pia umemkumbuka. Sio kuwapa hela hawa viumbe zandiki.