Inauma sana kuachwa sababu hauna pesa

Inauma sana kuachwa sababu hauna pesa

Status
Not open for further replies.

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,383
Reaction score
7,976
Ni wiki kadhaa tangu mpenzi wangu aniache. Nilikuwa nimempenda kweli na nilimpata kipindi ambacho nilikuwa nimetoka kuachwa na mwanamke wangu aliyepita sababu kuu ikiwa ni pesa na kuniambia anataka watu wenye wadhifa.

Sasa baada ya kumpata huyu kutokana na hali yangu bado sijakaa vizuri lakini nikaapa huyu sitaki kumpoteza. Kwakweli nilijitahidi sana kumpa pesa ili kumuonesha love. Kila pesa aliyokuwa akiomba nilikuwa nikimpa ikafika time nikaona mizinga inakuwa inazidi hadi muda mwingine nikawa nashindwa kula mimi vizuri sababu ya mahitaji yake.

Sasa ameniacha na chanzo cha kuniacha ni pesa. Aliniomba nauli ya kurudia alikuwa mkoa mwingine kwa dada yake kusalimia nikamtumia 60 tena siku ya pili akaanza kuniomba tena 50 anasema ana shida nayo nikamwambia leo sina subiri siku nne nikutafutie nikaona kakasirika. Siku ya pili akanitumia SMS "sikutaki haunithamini".

Tangu hapo akatoa na line niliyomsajilia mimi mpaka leo hajapatikana tena nimebaki na maumivu tu makali sana nikimkumbuka sana. Kweli kupenda ni kitu kingine!
 
Nakupa pole sana ndugu yangu..najua maumivu ya mapenzi yalivyo, lakini nikupe tu ushauri ktk kipindi cha hivi karibuni vijana wengi tunapitia kwenye fkake love bila kujua kwa sababu hatuchunguzi watu tunaokuwa nao.. kumjua mwanamke ambaye hana future na wewe ni rahisi sana kama hautaingia kwenye mahusiano kwa pupa..next time mchunguze na dont pretend ili kumuonyesha una pesa...anapaswa akupende jinsi ulivyo mwanzoni tu. Pole sana
 
HAWA nwalimu wao hajulikani
ukiwa na pesa na unacho kibamia bado atakuacha
iko siku utakuwa na kuoa utulie
subira yavuta heri
 
Sawa mkuu inawezekana japo kwa mjini hapa kuna ku straggle sana kumpata mtu huyo ndo mana tunalazimika kuonekan tunaweza kugharamia
 
HAWA nwalimu wao hajulikani
ukiwa na pesa na unacho kibamia bado atakuacha
iko siku utakuwa na kuoa utulie
subira yavuta heri
Ni bora kuachwa unahela unawez ukaenda zako nchi yoyote kutuliza mawazo ukaendelea kuwa na marafiki wakutosha sio kipindi ambacho upo vibaya mda mwingi nipo geto tu alone
 
Ni bora kuachwa unahela unawez ukaenda zako nchi yoyote kutuliza mawazo ukaendelea kuwa na marafiki wakutosha sio kipindi ambacho upo vibaya mda mwingi nipo geto tu alone
toka humo ndani utakufa bure Dogo
fanya mazoezi ya jogging, unaweza kukutana na mchumba wa ukweli
nenda kwenye social activities km mipira ngoma hata vigodoro utasahau
 
Fujitsu kama ukiebdekea nae ndoa yenu itakuwaje? Yaani kama nyumbani hukulete kuku, beef filet au samaki unaambiwa humthamini. Si ndiyo mwanza wa kuleteana pressure hayo! Mshukuru Mungu wako, mwache aende.
Umeandika nini hiyo lugha kama ngeni
 
Hawa viumbe ni balaa hata maandiko yanasema tuishi nao kwa akili,tatizo ulinjengea mazingira ya kipesa tafuta mwanamke anayeendanavna mazingira yako achana na warembo wa mjini ni pasua kichwa
 
Daah napoona ishu kama hz huwa natamani initokee, yaani nimpende mwanamke ambaye atanifanya niweze kusend pesa everytime anapohitaji.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom