Inauma: 'Alisema tusimpige picha'... Angesema mvue nguo!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inauma: 'Alisema tusimpige picha'... Angesema mvue nguo!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waberoya, Feb 24, 2011.

 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Ukiangalia media zetu zinamfanya kila mtu eti kama vile mjinga...walichukuzana wakaenda kumwona Al Adawi, Al Adawi akasema msinipige picha! nao wakakubali! wakamsikiliza hawakumpiga picha!

  Siku ya pili yake magazeti yote yakalalamika eti alisema tusimpige picha, yule Al Adawi wa uongo, sijui eti mtanzania, sijui eti feki na maneno kibao.. ili mradi wauze gazeti yes dowans si inalipa bana!

  Hawa walioingia mule sio watoto ni wanaume na wanawake watu wazima sio chekechea! KULIKUWA NA ULAZIMA gani kumsikiliza? kwa nini wasitoke nje basi baada ya kuona msimamo wa Adawi?

  Hivi inaingia akilini kweli? kwa nini watanzania wamechukuliwa ni wapenda umbea na wako tayari kununua habari zozote zile hata kama zinadhallilisha utashi na common sense ya watanzania..hivi is it a debate kuwa Adawi alisema asipigwe picha?, kweli haukumpiga na ukamsikiliza toka mwazo hadi mwisho, angesema lingine je?

  Angesema muingie uchi mngekubali tu! na kesho mngelalamika alisema tuvue nguo! Ndio angesema vueni nguo ili kuhakikisha wenye vinasa hawana...waandishi mmejidhalilisha sana! kesho atakuja mwingine na condition zake! hapa mlikamatwa

  Hawa ni waandishi wa habari eti, je hao viongozi wa serikali wakiambiwa yale ya asilimia 10% hamuoni huwa wanakubali tu, kama wale tunaowategemea wawe wakali kwa matendo ya uwazi sio wakali je wale tunaowategema kuwa wakali kwa matendo ya siri inakuwaje?

  Hivi kweli sivyo tulivyo??

  Nashukuru nimeipata hii katuni kutoka kwa (Safari ni Safari) naamini imetolewa na Majira ili kukazia hoja
  [​IMG]
   
 2. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #2
  Feb 24, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hoja yako haina maana.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Ulikuwemo? pole sana

  Ninachotaka hapa kuangalia ni jinsi gani inavyokuwa kukemea maovu ni vigumu kama sisi wenyewe hatuna misingi na itikadi zetu tunazoziamini, huwezi ukaambia usifanye hivi ukafanya halafu kesho ukaamka na kulaumu, alisema eti tusimpige picha, hauoni kichekesho hiki!
   
 4. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #4
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  upupu,tafuta lingine la kusema!mnakera na ma-thread ya kijinga!
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ana hoja ya msingi kama huna cha kuchangia chapa lapa, au ndo nyinyi mlilipwa na huyu fisadi
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Unaita upupu kwa sababu umeingizwa mkenge na waandishi wa habari na kuona walichofanya ni sahihi! sasa nani ana upupu, haunipi asante lau kidogo kukuonjesha ladha ya kufikiria nje ya box, hujalazimishwa kusoma hii thread nenda zingine nyingi tu zo 'dowans' zisome tu niachie upupu wangu, hujakuwasha wewe utawawasha wenzako wasiofikiria na kulialia kama vitoto.
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280

  Asante mkuu!
   
 8. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Umeukalia?
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Niaibu bwana kwa waandishi wa habari kuambiwa msipige pic na nyinyi mkatoka bila kupiga picha kweli huu ni upuuuzi kweli!
  Sjui nani yule alisema waandishi wahabari walifeli mitihani ya form four! mimi simtaji ila mnamfahamu,
  Ndo maana Sipika akasema magazeti yenu YASOMWE KAMA BARUA.:A S 13::A S 13:
  MNAENDA TUU KAMA MAZUZU BASI HIYO HABARI MSINGEITOA, NYINYI NDO MNALETA UGONVI NCHINI HAPA!:A S 13::A S 13:
   
 10. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tunazungumzia Uhuru wa habari, tunata serikari ihakishe inavipa uhuru viombo vya habari. Cha kushangaza watu wa habari wanakubali kunyimwa uhuru na mtu mmoja, Al Adawi? Je wangempiga picha angewafanya nini wakati serikali yetu inadhamini uhuru wa habari. Mngegoma kuhudhuri kikao chake mpaka andoe masharti, mlivyoiwakilisha habari ile kwenye media ni kama porojo tu. Shame of you.
   
 11. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  pia cha kushangaza zaidi hatujapata waliyomuuliza huko kwenye press meeting, sasa sijui pia aliwakataza kuuliza swali lolote...
   
 12. I

  Igembe Nsabo Member

  #12
  Feb 24, 2011
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Mkuu nakuunga Mkono kwa hilo! Hatuna Waandishi wa Habari walio makini most of them are Papetrator and Trator, some of them not all!! Mimi haingii akilini kuona mtu au chombo cha Habari kinalipoti taarifa hiyo na kuendelea kulalama tu! Andikeni habari zenye maslahi ya taifa bila kuwa na uoga na kutokusaliti nafsi zenu kwa tamaa ya pesa kidogo tu ambazo zinakufanya uonekane kama huna akili au umetumika kwa maslahi ya wachache!!!
   
 13. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,227
  Likes Received: 1,153
  Trophy Points: 280
  Nakupa Thanks zangu.
  Hapa pia kama kuna anayeweza kuleta list ya vyombo na waandishi waliohudhuria/ kusikiliza wakala wa mafisadi atatusaidia kutokupotezea vijisenti vyetu kununua alichokiita barua za wasomaji wakala mwingine wa mafisadi.
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mi nakubaliana na wewe Waberoya. Haiingii akilini eti waandishi wa habari, tena wengine ni wahariri, mnapewa mwaliko (na hapa inabidi tuulize mwaliko huo ulitolewa kwa akina nani na kufuata utaratibu gani na kwa nini vyombo vingine kama MwanaHalisi havikuhusishwa) then mnaambiwa msipige picha, mnakubali tu,halafu mnakuja kuamndika mmiliki wa Dowans amekataa kupigwa picha.........So what? kwa hiyo hicho ndo mlichoona cha kuwaambia wananchi, that is news to you. Shame on you.

  Integrity ya hawa waandishi wa habari (fake) walioalikwa ni lazima tui-question. Uzalendo wao upo wapi? je walimuuliza kwa nini hataki kupigwa picha? kama investor (hivi huyu nae ni investor? - generators, kweli?) kwa nini hataki watu wamfahamu kwa sura? anaogopa nini?
   
 15. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #15
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,592
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Umebadili avatar mara hii! kidonge hiki!!, unaweza kutema tu, maji ya uhai yanasaidia sana, juice za vijoti may help unajua Klorokwin tena!

  usirudie kosa la kukosoa tu thread huwa hatukurupuki, inabidi huwe shujaa sana kuzipinga

  swali; ni vingapi kama vya Al Adawi vinatokea kila siku kwenye media zetu kwa mafisadi na wenye uwezo mbalimbali, sio ndio dalili tosha kuwa hata habari za kila siku sio za kuaminika sana, unaweza kupika tu au kufuata matakwa ya matajiri..A.I.B.UUUUU
   
 16. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu upo sahihi kabisa.
  Wanaobeza basi ujue walikuwepo.
  Mimi najiuliza hivi hawa waandishi na wapiga picha wetu mahiri kweli walikubali ujinga ule? Walipewa nini? Halafu wakikaa kwenye tv wanauza sura na kujifanya kubwabwaja kumbe hamna kitu.
  Kama mtu amekuja nchini kwao, akawapa amri, wakatii. Je wakitumwa wakatafute habari za uchunguzi nje ya nchi wataweza?
  Wabadilike la sivyo hiyo kazi haiwafai.
   
 17. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  walikuwa waandishi wasaliti wala si wazalendo. Kwani wangemsikiliza na mwishoni mwa mambo wakampiga picha kibao-angefanya nini??? Ujuha huo...
   
 18. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Anaye mdhihaki Waberoya kwa thread hii basi hajui nguvu ya kalamu kwenye jamii

  Nakuunga mkono Waberoya,haiwezekani mtu awapangie kazi wahariri wa vyombo halali vya habari nini ca kufanya na hii ni aibu sana kwa media za TZ;Al-Adawi angekutana na wahariri wanaojua kazi zao wangeondoka kwenye chumba hicho maana kuwakataza kupiga picha ni sawa na kuwaingilia kwenye kazi zao;na habari zake za kuja zisingeripotiwa na chombo chochote kile cha habari!

  Kitendo hiki cha waandishi wetu kupangiwa cha kufanya na wenye mabilion kinafanana kabisa na katuni ile kutoka Kenya iliyo onyesha waaandishi wetu wakimpigia magoti bwana mkubwa!
   
 19. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hoja nzuri ila imeletwa na wrong person ambaye credibility yake inayoyoma. Na ungeendelea tu kidogo ungeishia kusema hao waandishi wa habari ni CDM! Poor Waberoya!
   
 20. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Ukombozi/uhuru utakamilika pale tu utumwa wa fikra utakapoisha!
  Safari bado inaendelelea kutoka utumwani.
   
Loading...