Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,089
- 9,259
Uongozi umeshatowa "ultimatum", mkishindwa kujiendesha, tunauza. Kazi kwenu.
Unauza wewe na Nani?
manamuuzia nani?
si useme tu MNAJIUZIA!
Uongozi umeshatowa "ultimatum", mkishindwa kujiendesha, tunauza. Kazi kwenu.
Toka awamu ya Alli Hassan Mwiny iliamuliwa kuwa shirika la umma lisiloweza kujiendesha lenyewe halitopewa ruzuku.
Wizi, Uzembe, Uvivu, Uongo ndiyo unayapeekea mashirika yote ya umma kufa.
Ukiona lipo ujuwe hilo amma linajiendesha lenyewe au linapewa ruzuku kwa kuwa hakuna mbadala wa mashirika binafsi, mfano TANESCO, kama si kusaidiwa na Serikali lingeshakufilia mbali zamani sana.
Sishangai.
Mmiliki ni nani?
Mkuu take it from me. TTCL haijafilisika na sasa wako kwenye mkakati kuanzia April kuvamia soko la GSM badala la hili la sasa la CDMA. Tuliza ball endelea kuwa na imani na Kamu.Haya mengine mbona hakuna jipya? Kwani kufilisika kwa TTCL kumeanza kutajwa leo? Juzi juzi hapa wakati Zitto ana mgogoro na chama chake walienda kina Filikunjombe. Nao wakaja na porojo hizi hizi. Hatujui walienda kuiambia nini serikali. Zitto nae anakuja na yake....TTCL is there to stay. Misukosuko iliyoipata ni mizito ingeshakuwa marehemu kitambo.Dr. Kazaura alileta matumaini hapa mwishomwisho, lakini naona kuna maradhi ya kimsingi hapo ambayo hayawezi kubadilishwa na mtu mmoja hata awe na ujuzi gani.
Bahati mbaya hili litakuwa kwenye rekodi yake kama CEO aliyeipitisha TTCL kwenye kuwa mufilisi.
Mkuu labda tukodishe na viongozi wa serikari pia maana wote wanahusika kwa uzembe uliopo.Katika nchi yetu kuna matatizo ya utendaji na utaalamu binafsi wa watendaji,
Si vibaya kwa mashirika yetu kama haya tukatafuta wataalam wazoefu toka nje ili kuyainua na kusimamia kwa kipindi maalum, rais Moi wa kenya aliweza fanikiwa kwa kuifufua benki ya taifa ya biashshara (KCB) illiyokuwa imependekezwa kufirisiwa kwa kumkabidhi mtendaji mkuu aliyemnunua toka barclays jukumu hilo na sasa kcb hiko kila mahali ndani ya east africa.
Tatizo kuu hapo ni mikataba tu, hawa wahuni walifanya ujanja wa kununua hisa TTCL ili kutumia miundombinu yake kwa kuikuza Celtel.
Fikiria walitumia minara ya TCCL na kuwafanya wapatikane nchi nzima, na ofisi zao zikawekwa kwenye kiwanja cha TTCL.
Sasa wameshakuza Simu zao za mkononi na wanajitegemea hawataki tena TCCL ifufuke kwa sababu wanajua itakuwa mshindani wao mkubwa kibiashara.
Inasikitisha sana kuona mali za umma zinafanywa ni shamba la bibi na hawa raia wa kigeni kwa kuwatumia viongozi tuliowapa dhamana ya nchi yetu.
Ova
Reli liko hai wakati usafirishaji wa mizigo umeshuka toka tani zaidi ya milioni moja miaka kabla ya 2007 hadi tani 150,000 sasa??!!
Hebu tuambie ni kazi gani zinaendelea?!
Dr. Kazaura alileta matumaini hapa mwishomwisho, lakini naona kuna maradhi ya kimsingi hapo ambayo hayawezi kubadilishwa na mtu mmoja hata awe na ujuzi gani.
Bahati mbaya hili litakuwa kwenye rekodi yake kama CEO aliyeipitisha TTCL kwenye kuwa mufilisi.