Lusungo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 29,514
- 42,649
Akibisha na hapa, basi ni mchochezi.
Hawezi kujibu achilia mbali kubisha.....
Sijui Kama ni MTU mzima kweli na exposure anayojidai anayo ilhali tunaona kabisa thinking yake ni too low .....
Akibisha na hapa, basi ni mchochezi.
Mkuu pale yupo MWANAMBOKA S.A.SALIM
sijui na shirika la IKULU nalo ataliuwa lini?Kwa hiyo hili ni shirika la tatu linakufa chini ya mikono ya Kikwete.
Air Tanzania
Railway
TTCL
Acha upunguani wewe usipende kuchangia vitu usivyovijua utaumbuka....
Huwa nakukanya Sana mambo ya kitaalamu huyawezi we imba taarabu zako za kumsifia shemejiyo mwenye tezi dume....
Hiyo kampuni ya airtel imeinunua Zain ambayo nayo walinunua celtel international ambao nao walinunua Celtel Tz.....
So Bhahti Airtel walinunua kampuni pamoja na Mali zake ikiwemo hisa na madeni so Airtel Tanzania bado ni sehemu ya wamiliki Wa TTCL ndio maana wanadai PESA ya hisa sasa unakurupuka nini kuchangia ujinga??
Kwani PAP alivyolipwa madeni ya kuanzia 2006 alianza kazi 2006??
Kaa kimya kuliko kudhihirisha ujinga na upunguani wako na inaonekana uwezo wako Wa reasoning na thinking ni duni Sana Kama huyo shemeji yako....
Omari Issa alikuwa Celtel sio? Ndiye atakuwa ame-engineer haya mambo. Na sasa anasimamia BRN.
Dada yake January Makamba akiwa Vodacom alipata kuchangisha fedha za kampeni za ubunge wa January kutoka kwa wenye makampuni ya mawasiliano (Barua iliyoandikwa na dada yake January kwenda kwa haya makampuni iliwekwa hapa jamvini) kwa ahadi kwamba akishinda ubunge, atakuwa Waziri wa Mawasiliano na mambo yao yataenda vizuri. Ni kweli sasa January ni Naibu Waziri wa Mawasiliano. Yuko pale kuhakikisha maslahi ya wafanyabiashara yanalindwa, kwa kuliingiza taifa kwenye hasara kubwa. Na kwa mambo yalivyokaa, inaonekana kazi ya January ilikuwa ni kuhakikisha TTCL inauzwa kwa wawekezaji (kama vile Airtel au Vodacom) kwa njia za mizengwe. Another plausible theory ni kwamba walitaka kuvuna kwa kuiingiza serikali mkenge wa kununua hisa za Airtel. Haiwezekani Kampuni ina hali mbaya kiasi hicho na hakuna jitihada zozote zilizofanyika kuiokoa. Wanataka kujenga mazingira ya kuiuza TTCL. Katika hili, Zitto ni wa kumtizama kwa jicho la tatu. Ni mjanja sana huyu kijana.
Unauhakika ni shemeji yake? asijekuwa mchepuko.
Kikwete si alipokea kijiti kwa bashasha, amefanya nini kulifufua? Ten years now.
Ukuwadi wa Kina Makamba ni kitu kilichowazi hata kipofu anaweza kukiona.
Hawa amanyang'au wa CCM ndio janja yao, Wanayafilisi mashirika ya Umma yaonekane ya hovyo kabla hawajajiuzia wao kwa bei za kutupwa. Typical Russian Oligarch moves of the 90's. Ndio kina Abramovich walivyoweza kuwa mabilionea.Leo hii tunawaona hawa kina Mohammed Enterprises waliouziwa mashamba na maghala na makarakana ya serikali kwa bei za nyanya, wakijitapa kuwa ni mabilionea, while in essence wameshiriki ku-embezzle mali za watanzania kwa bei za kutupwa.
Wasichojua, sio watanzania wote ni mazuzu. Tunaona yanayotokea, na tutayasema ili siku ya kuchukua hatua ikifia wasiseme hatukuwaambia haya.
Alijisemea Kuli."yana mwisho haya" Kiko wapi?
mbona mashirika yote yamekufa mengi sana toka enzi ya nyerere, mwinyim, mkapa na kikwete? Na mwinyi ndiyo kabisa aliamuwa shirika lolote lisiloweza kuijinedesha lenyewe halitopewa ruzuku tena na serikali, matokeo si unayajuwa au mpaka tuchambuwe?
Haya yaliyobaki mpaka hii leo yamejitahidi sana.
Huo uongozi wa ttcl ni mbovu kabisa si shirika la kufa lile kwa miuondombinu waliokuwa nayo, tazama attakaelinunuwa utaona linavyoshamiri.
Lakini ndiyo mashirika uya umma yalivyo kama halina ruzuku hayawezi kujiendesha, watu wanaiba tu mtindo mmoja.
Nilikuwa tukuyu juzi, nikapita kwenye mashamba makubwa kwelikweli y chai, yanamilikiwa na METL, na sehemu kubwa ya hayo mashamba jamaa kaitelekeza.
Toka awamu ya Alli Hassan Mwiny iliamuliwa kuwa shirika la umma lisiloweza kujiendesha lenyewe halitopewa ruzuku.
Wizi, Uzembe, Uvivu, Uongo ndiyo unayapeekea mashirika yote ya umma kufa.
Ukiona lipo ujuwe hilo amma linajiendesha lenyewe au linapewa ruzuku kwa kuwa hakuna mbadala wa mashirika binafsi, mfano TANESCO, kama si kusaidiwa na Serikali lingeshakufilia mbali zamani sana.
Sishangai.
Lakini jamani tujiulize kama kweli serekali haingegawa zile hela za escrow kwa watu binafsi, na ikaamua kuikopesha TTCL bilioni 100 tu ingekuwaje?
Ikaikopesha ATCL biloini 200 siingenunua hata boin 2 ambazo zingetosha kabisa kulifufua shirika.
Watanzania tuamke, jibu mnalo!