INASIKITISHA: Makaburi Kinondoni yanavunjwa makusudi ili ipatikane nafasi ya kuzikia

Sio kinondoni tu makaburi mengi hufanya hivyo..jiulize makuburi ya kisutu mbona kila siku wanazika watu na ukiangalia kasehemu kadogo.. makaburi huitaj ukarabati sasa wengi wakishizika harud rudi tena kwahiyo wazikaji wanatoa mifupa wanamwuZia mwengine maisha yanaendelea,ndo mana wachaga tunazika moshi kuepuka hii kadhia
 
Iwe mmakua je hauna Mashamba kwenu ili ukamstiri ndugu yako bila disturbance yoyote, Sisi kule Tanga huwa tuna makaburi mpaka ya mababu zetu wa zamani sana haya jengewi ila eneo lina julikana na hakuna kutoa mifupa uweke Mwingine ardhi ni kubwa sana na tume ya preserve Kwa kumbukumbu na mambo ya kimila nina Kaburi la Babu wa mababu mark yake ni pana mti mkubwa alikuwa mwamba kweli huyo Babu na alizikwa hapo na mkewe huwa tunatembelea walau once per year ntakuza wanangu kwa Kuwasimulia Matendo safi ya babu zao na sio upuuzi sijui wa kwenda Israel au Macca kuhiji wakitaka kwenda huko waende just for utalii tu
 
Kama kisha pata demu huko Kuzimu ama laa
huu uzi umenikumbusha kaburi fulani la ndugu yake Mobutu sese seko, waasi wa FDL walienda kutaka kulibomoa ili waibe dhahabu mana jamaa alizikwa na vitu vya thamani
walipofika wakaanza kwa kulifyatulia risasi lile kaburi lakini risasi ilienda ikakata kona ikamrudia aliyefyatua na kumpiga kifuani akaanguka na wenzie wakaamsha mbio,marehemu aliitwa Maboti nadhani
 
Mhm ningependa kufahamu zaidi kuhusu hili tafadhali
 
Mimi msinifanyie cremation, huo moto nikutane nao huko sio niuanzie hapa duniani.
 
Huyo mbona mdogo hata wale wakubwa kwa cheo na ubora kuzidi haifai kuwajengea makaburi.

Ndiyo maana kuna baadhi ya mitume hawajulikani au haijulikani makaburi yao yako wapi. Hii ni hekima kubwa sana.
Kwanini hatuchomwi kama wadosi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…