Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,448
- 16,313
Kwa mujibu wa gazeti la nipashe la leo, limeripoti kwamba japokuwa makaburi ya Kisutu, Kinondoni, Magomeni na Sinza kutangazwa na serikali kuwa yamejaa toka mwaka 2018, lakini yameendelea kutumika mpaka sasa.
Kinachofanyika ni unawapa tenda vijana maalumu wanaohusika kuchimba makaburi kwenye hayo maeneo tajwa, na wao watakutafutia eneo la kuzika kwa njia wanazozijua wao.
Kwenye mchakato wa kutengeneza kaburi, ndugu hawaruhusiwi kuhusika, bali mtaenda kuangalia pindi wanapomaliza kazi ya kuandaa kaburi lenu.
Kwa mujibu wa mtangazaji Zembwela wa Wasafi FM, amesema wanachofanya wale vijana wanatengeneza makaburi juu ya makaburi mengine, hasa yale ambayo hayajajengewa, ila kwenye kufukua hawaendi mpaka zile futi 6 zinazotakiwa ili wasije kuwafikia wale marehemu wengine kule chini, wanaishia futi 5 au 4.