Kuna namna sahihi ya kucheza siasa za Tanzania, lakini si kwa njia ya Gwajima.
SIasa za Tanzania hazihitaji mbwembwe. Hii nchi sio tajiri lakini walau ina dira.
Kuna namna kwa nini baada ya Nyerere Mwinyi alikuwa rais, akafatiwa na Mkapa, akafatiwa na Kikwete, akafatiwa na Magufuli, na sasa tu mtu anaitwa Samia.
Hawa watu wanatofautiana sana. Lakini, I think, ninaweza kupata theme.
Hii nchi inahitahi iongozwe na mtu ana akili, ana humility na ana moyo.
Ukimsoma tu Gwajima, huyu mtu hana akili, hana humility na hana moyo.
Its just quite perplexing kwamba ni kiongozi kwenye dini niipendayo sana, ninayoiamini sana, ya kiKristo, but no, Gwajima is not my guy.
Kila kiftu anasema kiko transparent, so obvious kwamba anatafuta dili lake. Mfano anavyosema wakuu wa vyombo vya usalama wanahitaji kulindwa maana yake nini? Yaani mkuu wa majeshi au wa Polisi alindwe? Aongezewe maslahi zaidi ya anayopewa sasa? HOW? WHY?
Ni upuuzi, ni kujigonga, mtu yeyote anaona what Gwajima is up to. Ni akili ndogo. Ni aina ya ukristo ambao watu wa nchi za kiafrika wa miaka ya hivi karibuni wamejikuta wakikumbana nayo. Ukristo maslahi ulio mbali sana Kristo mwenyewe.
Mi siyo fan wa CCM. But nitamkataa Samia kwa mambo mengine lakini sio kwa tuhuma za Gwajima. So far kwangu baada ya Magufuli Samia hajaharibu sana. Kuna namna ambavyo mambo ningependa yawe tofauti (mfano, kuna namna rushwa na uzemve umeongezeka serikalini) lakini so far mambo yanavumilika.