Inakuwaje Doctor kumfungulisha mwanamke?

Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2008
Messages
326
Points
195
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2008
326 195
Katika kukaa na kufikiria zaidi kuna baadhi ya mambo kwa nchi ya Tanzania yananisumbua na nadhani hayo mambo hawajayatilia maanani zaidi na kujua wafanye nini ili kila kitu kiweze kuwa sawa kama wanavofanya nchi za wenzetu.....Hivi sasa bongo kuna kitu kama hospital mfano mke amepata dharula ya kujifungua inabidi akimbizwe hospital sasa akishafika hospital unakuta anapokelewa na doctor ndio anakwenda kumfungulisha mwanamke sasa jamani kweli hii ni sa hiii??Au doctor ana ruksa za kuweza kuona naniihii za wake wa watu hata kama yeye amepitishwa kuwa doctor??Na pia ma nurse wanakazi gani zaidi hospital au hamna manurse wasomi ambao wanaweza kumfungulisha mwanamke mwenye mimba???Maana huku wenzetu kuna manurse ndio kazi zao hizo,,Sasa kwa kwetu bongo nashindwa kuelewa ndio elimu yetu tulipofikia au ndio mpangilio ambao umepangwa???
 
Pundit

Pundit

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2007
Messages
3,741
Points
1,225
Pundit

Pundit

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2007
3,741 1,225
Mtoto kuzaliwa salama na mwanamke kuonwa nanihii kipi muhimu zaidi?
 
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2008
Messages
326
Points
195
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2008
326 195
Mtoto kuzaliwa salama na mwanamke kuonwa nanihii kipi muhimu zaidi?

Sawa mkuu lakini sasa hatuna manurse ambao wamesomeshwa kwa ajili hiyo maana kama nurse na yeye akisoma anaweza kuwa na elimu kama ya doctor.....Ina maana doctor anaelimu zaidi kuliko nurse pia nurse haweza kumfungulisha mama na kutoka salama???
 
Nkamangi

Nkamangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
642
Points
0
Nkamangi

Nkamangi

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
642 0
Yassin, nesi wapo wanaume na wanawake kama madaktari walivyo wanawake na wanaume. Hao madaktari wanaume unafikiri wanaweka kumbukumbu za kila mwanamke na sehemu zake za siri walizoziona? Nafikiri wana mambo ya munimu zaidi ya kuweka kumbukumbu. Wasiwasi kama wako upo sana afghanistan...
 
M

Mama

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2008
Messages
2,858
Points
0
M

Mama

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2008
2,858 0
Hao madoc wa kiume wanapenda sana kutia vidole na kushikashika matiti! unabaki kushangaa tu huyu jamaa vipi, wa wapi huyu?
 
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2008
Messages
326
Points
195
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2008
326 195
Hao madoc wa kiume wanapenda sana kutia vidole na kushikashika matiti! unabaki kushangaa tu huyu jamaa vipi, wa wapi huyu?

Mama kumbe unajuwa hilo maana wasiwasi wangu ni hapo mke anapigwa sindano ya usingizi unadhani doctor atabakia kuangalia tu???Kuna mambo mengine unajuwa ukifikiria zaidi na kiundani zaidi nadhani majibu yapo mengi tu.......
 
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2008
Messages
326
Points
195
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2008
326 195
Yassin, nesi wapo wanaume na wanawake kama madaktari walivyo wanawake na wanaume. Hao madaktari wanaume unafikiri wanaweka kumbukumbu za kila mwanamke na sehemu zake za siri walizoziona? Nafikiri wana mambo ya munimu zaidi ya kuweka kumbukumbu. Wasiwasi kama wako upo sana afghanistan...

Ok sawa sawa nimeelewa
ndugu yangu lakini sasa hapo mimi sisemei kwamba sipendi madoctor wananye hivyo lakini niachosema ni amani ya mke au sio maana mwanamke akiwa kule anakuwa peke yake na doctor sidhani kama anahaki zaidi kwa mwanamke nadhani bora mwanamke akiingizwa kufungulishwa afungulishwe na mwanamke mwenzake ndio inakuwa vizuri zaidi au inakuwaje hapo????
 
M

Mama

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2008
Messages
2,858
Points
0
M

Mama

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2008
2,858 0
hadi apigwe sindano ya usingizi, lazima kutakuwa na serious case na hivyo Dr hatakuwa peke yake.

Wasi wasi unakuja pale unapokuwa umeenda tu kwa consultation...., hivyo usijidanganye uko busy sana na schedule unamwacha mkeo anaenda mwenyewe mara zote, msindikize.

BTW sio madr wanaume wote wako hivyo.
 
Pundit

Pundit

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2007
Messages
3,741
Points
1,225
Pundit

Pundit

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2007
3,741 1,225
Hao madoc wa kiume wanapenda sana kutia vidole na kushikashika matiti! unabaki kushangaa tu huyu jamaa vipi, wa wapi huyu?
Mama hao inabidi kama kuna ushahidi wafanyiwe ethical block kwenye practices zao.

Alternative ni kuwa na ma-gynaecologist wa kike tu, lakini hata hao wa kike kuna wengine ma butch, sasa ukikutana na daktari wa kike msagaji akakushika shika si tunarudi pale pale?

Kama kuna daktari anafanya huo ushenzi anafanya ushenzi kwa sababu ni mshenzi, sio kwa sababu ni mwanamme.Hata mwanamke anaweza kufanya ushenzi.

Therefore tuwaondoe madaktari washenzi bila kujali gender zao, kwani kusema tuwe na madaktari wanawake tu hakutasaidia kitu.
 
Nkamangi

Nkamangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
642
Points
0
Nkamangi

Nkamangi

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
642 0
Cha muhimu ni ujuzi wa kumwezesha kumsaidia mama kujifungua salama sio jinsia. Hao mnaosema wana "take advantage of the situation" ni wachache wasiojua maadili ya kazi zao. Kumpima mama njia kabla ya kujifungua ni muhimu kujua maendeleo ya uchungu na mtoto alipofikia, mtu mwenye akili nzuri hawezi kufanya hivyo kwa manufaa yake mengine binafsi. Tanzania hatujafikia hatua ya kuchagua msaidizi wa kujifungua kny hospitali za serikali....safari ni ndefu
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
95,876
Points
2,000
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
95,876 2,000
Hao madoc wa kiume wanapenda sana kutia vidole na kushikashika matiti! unabaki kushangaa tu huyu jamaa vipi, wa wapi huyu?
LOL! Mama umenichekesha kweli kweli...Ukiona anatomasatomasa zaidi matiti basi ujue kayapenda :). Hilo tatizo lipo sana. Nimeona hata wazungu wengi katika vipindi mbali mbali vya TV wanalalamika hivyo wengine huhakikisha wanakuwa na magynecologist (I am not sure about the spelling) wanawake. Wengine hukasirika sana kitendo cha kuamriwa wavue nguo apande kitandani huku ameacha nyeti zote wazi kabisa halafu daktari anaendelea na shughuli zake kwa dakika 10 hata zaidi.
 
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2008
Messages
326
Points
195
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2008
326 195
LOL! Mama umenichekesha kweli kweli...Ukiona anatomasatomasa zaidi matiti basi ujue kayapenda :). Hilo tatizo lipo sana. Nimeona hata wazungu wengi katika vipindi mbali mbali vya TV wanalalamika hivyo wengine huhakikisha wanakuwa na magynecologist (I am not sure about the spelling) wanawake. Wengine hukasirika sana kitendo cha kuamriwa wavue nguo apande kitandani huku ameacha nyeti zote wazi kabisa halafu daktari anaendelea na shughuli zake kwa dakika 10 hata zaidi.

Kabisa maana hata tukiangalia kwamba yeye mwanamke mwenyewe anaambiwa avue nguo apande kitandani unadhani huwa anajisikia vipi hapo au anakuwa katika hali gani????Maana pia anakuwa anajisikia vibaya sana bora angekuwa mwanamke wenzake lakini sio doctor ws kiume ndio anamwambia afanye hivyo naona kama haijatulia kabisa.........
 
M

Mama

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2008
Messages
2,858
Points
0
M

Mama

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2008
2,858 0
Mama hao inabidi kama kuna ushahidi wafanyiwe ethical block kwenye practices zao.

Alternative ni kuwa na ma-gynaecologist wa kike tu, lakini hata hao wa kike kuna wengine ma butch, sasa ukikutana na daktari wa kike msagaji akakushika shika si tunarudi pale pale?

Kama kuna daktari anafanya huo ushenzi anafanya ushenzi kwa sababu ni mshenzi, sio kwa sababu ni mwanamme.Hata mwanamke anaweza kufanya ushenzi.

Therefore tuwaondoe madaktari washenzi bila kujali gender zao, kwani kusema tuwe na madaktari wanawake tu hakutasaidia kitu.
Ulo sema ni kweli.

Kuna tofauti sana msagaji akakushika shika na ambavyo mwanaume atakushika shika. Kwanza si hadi ujue kwamba mwanamke anayekushika shika hapo ni msagaji! mara nyingi ukimuona mwanamke mwenzio hata akushike wapi, huwezi kumdhania vinginevyo.

Ila kama ni mwanaume, na unajua kabisa kwa hali uliyonayo hapo huhitaji kushikwa wala kuguswa na dr; pengine ni routine visit tu (halafu anaanza kukushikashika manyonyo), hapo lazima uhisi huyu anataka kujiridhisha inturn wewe ndio umlipe kwa yeye kujiridhisha. Unaumwa mguu halafu unapimwa ........?!
 
M

Mama

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2008
Messages
2,858
Points
0
M

Mama

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2008
2,858 0
LOL! Mama umenichekesha kweli kweli...Ukiona anatomasatomasa zaidi matiti basi ujue kayapenda :). Hilo tatizo lipo sana. Nimeona hata wazungu wengi katika vipindi mbali mbali vya TV wanalalamika hivyo wengine huhakikisha wanakuwa na magynecologist (I am not sure about the spelling) wanawake. Wengine hukasirika sana kitendo cha kuamriwa wavue nguo apande kitandani huku ameacha nyeti zote wazi kabisa halafu daktari anaendelea na shughuli zake kwa dakika 10 hata zaidi.

Halafu hicho kitendo kinakuudhi na huwezi kumuambia mwenzio ulofanyiwa maana anaweza kwenda muua dr bure. Unabaki na mahasira yako tu, mwenzio anajaji kuwa una mood swings za mimba! kumbe yaliyokupata Mungu ndio anajua.
 
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2008
Messages
326
Points
195
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2008
326 195
Ulo sema ni kweli.

Kuna tofauti sana msagaji akakushika shika na ambavyo mwanaume atakushika shika. Kwanza si hadi ujue kwamba mwanamke anayekushika shika hapo ni msagaji! mara nyingi ukimuona mwanamke mwenzio hata akushike wapi, huwezi kumdhania vinginevyo.

Ila kama ni mwanaume, na unajua kabisa kwa hali uliyonayo hapo huhitaji kushikwa wala kuguswa na dr: pengine ni routine visit tu (halafu anaanza kukushikashika manyonyo), hapo lazima uhisi huyu anataka kujiridhisha inturn wewe ndio umlipe kwa yeye kujiridhisha. Unaumwa mguu halafu unapimwa ........?!

Nadhani hapo hata mimi nimekuelewa vizuri zaidi,,,,,Hiyo hipo bora hata awe mwanamke mwenzako lakini mpaka uje ugundue inakuwa vigumu sana yaani...Sasa mbona wenzetu wanasheria maalum ambayo nurse au doctor wa kike ndiye anayemfungulisha mwanamke......Hiyo ndio haki sawa kabisa lakini doctor wa kiume kumfungulisha mwanamke naona kama sio sawa kabisa
 
M

Mama

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2008
Messages
2,858
Points
0
M

Mama

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2008
2,858 0
Nadhani hapo hata mimi nimekuelewa vizuri zaidi,,,,,Hiyo hipo bora hata awe mwanamke mwenzako lakini mpaka uje ugundue inakuwa vigumu sana yaani...Sasa mbona wenzetu wanasheria maalum ambayo nurse au doctor wa kike ndiye anayemfungulisha mwanamke......Hiyo ndio haki sawa kabisa lakini doctor wa kiume kumfungulisha mwanamke naona kama sio sawa kabisa

Kumbuka madr wa kike tulionao ni wachache sana. Hivyo wakati mwingine unakuwa huna jinsi....inabidi tu uende kwa huyo mwanaume. Au pengine una tatizo na dr bingwa wa tatizo lako ni mwanaume. Basi tu kina mama wanapitia majaribu lukuki.
 
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2008
Messages
326
Points
195
Y

Yassin

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2008
326 195
Kumbuka madr wa kike tulionao ni wachache sana. Hivyo wakati mwingine unakuwa huna jinsi....inabidi tu uende kwa huyo mwanaume. Au pengine una tatizo na dr bingwa wa tatizo lako ni mwanaume. Basi tu kina mama wanapitia majaribu lukuki.

Sasa ndio hapo ni kwamba tupo chini kielimu na kimaendeleo sasa inabidi tufahamu hilo zaidi maana kuwepo kwa madoctor wa kiume ambao wataalam zaidi naona kama bado tupo nyuma kidogo lakini ndio muendeleo wa nchi yetu ilivyo hatuwezi kulaumu.
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
95,876
Points
2,000
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
95,876 2,000
Ulo sema ni kweli.

Kuna tofauti sana msagaji akakushika shika na ambavyo mwanaume atakushika shika. Kwanza si hadi ujue kwamba mwanamke anayekushika shika hapo ni msagaji! mara nyingi ukimuona mwanamke mwenzio hata akushike wapi, huwezi kumdhania vinginevyo.

Ila kama ni mwanaume, na unajua kabisa kwa hali uliyonayo hapo huhitaji kushikwa wala kuguswa na dr; pengine ni routine visit tu (halafu anaanza kukushikashika manyonyo), hapo lazima uhisi huyu anataka kujiridhisha inturn wewe ndio umlipe kwa yeye kujiridhisha. Unaumwa mguu halafu unapimwa ........?!
Hapo umesema mama. Akina mama wengi ambao wana madaktari wanawake katika vipindi hivyo nilivyoviona walisema kuna tofauti kubwa kati ya madaktari wa kike na wa kiume. Madaktari wa kike hata siku moja hawatakuacha umeweka nyeti zote nje kwa zaidi ya dakika 2 kabla ya kuja kukushughulikia na hata tomasa tomasa yao ya matiti walidai ina tofauti kubwa ukilinganisha na madaktari wa kiume.
 
Buswelu

Buswelu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2007
Messages
2,007
Points
1,225
Buswelu

Buswelu

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2007
2,007 1,225
Kwanini tusichukue juhudi za msingi kabisa...kuhimiza wanawake walioko kwenye masomo ya udaktari wa binadamu...wasomee hasa hasa magojwa yanayo wahusu wao.Ila kupunguza....huu utata wa kifikra ambao mgojwa wa kike akienda kwa hospital wasiwe na wasi wasi na udaktari wa kiume katika miili yao.
 
Mpita Njia

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
7,008
Points
1,225
Mpita Njia

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
7,008 1,225
Mimi nadhani tutofautishe kati ya daktari anayefanya kazi yake kwa mujibu wa misingi ya kazi yake na daktari ambaye anaitumia taaluma yake kufanya ukware huo. Siamini kuwa kuilaumu taaluma ya udaktari kwa kosa linalofanywa na daktari mkware, ni kuitendea haki taaluma hiyo.
Wapo madaktari wengi ambao wanazalisha akina mama vizuri tu, je mbona hatutoi sifa kwa taaluma ya udaktari kuwa ni nzuri?
 
Forum statistics

Threads 1,325,004
Members 508,910
Posts 32,180,471
Top