Inadaiwa Polisi maarufu kama Tigo, huwabambikia makosa bodaboda na kuwalazimisha kutoa rushwa. Mamlaka iingilie kati

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Polisi wanaotembea na pikipiki maarufu kama (tigo), wanadaiwa kuwafanya bodaboda kama wahalifu kwa kuwakamata ovyo na kuwazungusha bila kuwapeleka kituoni wasipotoa pesa kwa lengo la kumalizana juu juu.
images (1).jpeg

Bodaboda wasiolipa pesa hupelekwa kituoni pasipo kujua hatma yao, pikipiki huchukuliwa ambapo inaweza kushikiliwa hata kwa mwezi mzima.

Inadaiwa kuwa baada ya kufikishwa kituoni, bodaboda hao hutoa kiasi cha pesa kisichopungua Tsh. 200,000/= kama sehemu ya malipo ya kurudishiwa pikipiki zao.

Pia, bodaboda wanaopeleka abiria katikati ya jiji wamesema hukamatwa pindi wanaposhusha abiria pasipo kuelezwa sababu maalamu kwa kuwa kilichokatazwa ni kupaki mjini na siyo kushusha abiria kwenye maeneo hayo. Pikipiki zao huchukuliwa wanapokamatwa wakiwa wanashusha abiria ambapo hupaswa kulipia Tsh. 100,000/= pasipo kupewa risiti yoyote.

Mamlaka zinazohusika zifuatilie kero hii pamoja na kuchukua hatua stahiki ili iweze kutatuliwa.
 
Back
Top Bottom