Inadaiwa hizi video ni za wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020

Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,870
2,000
Sisi tuliomba kwa Mungu atuaibishie wote watakaovuruga uchaguzi mkuu hakika alisikia maombi yetu
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,491
2,000
Nchi hii tumepitia kipindi kigumu Sana. Waliofanya haya wakatubu Sasa hata wakifa basi Mungu awe amewasamehe.

Kuna watu wako kwenye ofisi wasizostahili sababu ya huu uhuni. Unapofanya haya jua tu unawakomoa pia na Ndugu zako ambao wataongozwa na watu wasiostahili.

Sababu ya vihela vichache unaendekeza njaa zako na kuharibu tukio kubwa (uchaguzi) kama hili, hivi unajua ni gharama kiasi gani zimetumika kuandaa hili tukio? Unajua ni muda gani watu wameupoteza mpaka unakuja kuwaharibia maamuzi yao?

Hivi wanajua kua ushenzi huu unachelewesha demokrasia Kwa miaka kama mitano na pengine ikawa zaidi? Wanajua kua Demokrasia ni sehemu ya Maendeleo?

Ni Maji ya Bendera ya Aina gani uliyokunywa kiasi akili yako imekua mgando na kuwaza kua ni wale tu ndio wanastahili kukaa pale? Nini kikufanye uamini kua wengine hawastahili? Na kama mawazo yako wewe mmoja yanaamini wengine hawastahili, kwanini usiache basi uamuzi wa "Wengi Wape" uamue nani akae hapo? Kwanini utake yule unaemuona wewe kua anafaa ndo awe anafaa na Kwa wengine hata kama sio ridhaa yao?

Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,276
2,000
IMG_20210527_183902.jpg
 
kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
18,271
2,000
Wazalendo wameanza kuachia hadharani mambo machafu yaliyotendwa kwenye kile kilichoitwa uchaguzi mkuu wa 2020 .

Toleo la sasa ni video inayoonyesha wizi wa kishamba sana wa kura ulivyofanyika , tena chini ya watu walioaminiwa kulinda usalama .

Hebu jionee mwenyewe.

View attachment 1964679

Majina ya Wahusika wote yamepatikana , ila yanahifadhiwa kwa muda kwa sababu za kibinadamu
CCM B wakijipigia Kura,halafu mshahara ni uleule na madeni ya kutosha kwa mangi
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
7,244
2,000
Niuchelewashaji wa. Maendekeo kuwa na watunga Sera ambao hawajui matokeo hasi ama chanya ya Sera ama sheria wanazozitunha/zipitisha bungeni
 
Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,800
2,000
Mkuu umemsahau aliemuuwa Chacha Wangwe kwa sababu ya kutaka kugombea uenyekiti wa chama. Huyu naona Mungu kaanza kumhukumu hapa hapa duniani.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,762
2,000
Nchi hii tumepitia kipindi kigumu Sana. Waliofanya haya wakatubu Sasa hata wakifa basi Mungu awe amewasamehe.

Kuna watu wako kwenye ofisi wasizostahili sababu ya huu uhuni. Unapofanya haya jua tu unawakomoa pia na Ndugu zako ambao wataongozwa na watu wasiostahili.

Sababu ya vihela vichache unaendekeza njaa zako na kuharibu tukio kubwa (uchaguzi) kama hili, hivi unajua ni gharama kiasi gani zimetumika kuandaa hili tukio? Unajua ni muda gani watu wameupoteza mpaka unakuja kuwaharibia maamuzi yao?

Hivi wanajua kua ushenzi huu unachelewesha demokrasia Kwa miaka kama mitano na pengine ikawa zaidi? Wanajua kua Demokrasia ni sehemu ya Maendeleo?

Ni Maji ya Bendera ya Aina gani uliyokunywa kiasi akili yako imekua mgando na kuwaza kua ni wale tu ndio wanastahili kukaa pale? Nini kikufanye uamini kua wengine hawastahili? Na kama mawazo yako wewe mmoja yanaamini wengine hawastahili, kwanini usiache basi uamuzi wa "Wengi Wape" uamue nani akae hapo? Kwanini utake yule unaemuona wewe kua anafaa ndo awe anafaa na Kwa wengine hata kama sio ridhaa yao?
Sio hao tu. Lakini pia hawa wamesababisha laana shetani mkuu wao akatoweka kama upepo.

Nabii Suleimani ktk kitabu chake cha Mhubiri anasema Duniani pesa, mali na madaraka ni ubatiri mtupu.

Uuaji aliofanya na uporaji na uhujumu mwisho wa siku ukawa ubatili mtupu akazima mithiri ya mshumaa.
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,541
2,000
Nchi hii tumepitia kipindi kigumu Sana. Waliofanya haya wakatubu Sasa hata wakifa basi Mungu awe amewasamehe.

Kuna watu wako kwenye ofisi wasizostahili sababu ya huu uhuni. Unapofanya haya jua tu unawakomoa pia na Ndugu zako ambao wataongozwa na watu wasiostahili.

Sababu ya vihela vichache unaendekeza njaa zako na kuharibu tukio kubwa (uchaguzi) kama hili, hivi unajua ni gharama kiasi gani zimetumika kuandaa hili tukio? Unajua ni muda gani watu wameupoteza mpaka unakuja kuwaharibia maamuzi yao?

Hivi wanajua kua ushenzi huu unachelewesha demokrasia Kwa miaka kama mitano na pengine ikawa zaidi? Wanajua kua Demokrasia ni sehemu ya Maendeleo?

Ni Maji ya Bendera ya Aina gani uliyokunywa kiasi akili yako imekua mgando na kuwaza kua ni wale tu ndio wanastahili kukaa pale? Nini kikufanye uamini kua wengine hawastahili? Na kama mawazo yako wewe mmoja yanaamini wengine hawastahili, kwanini usiache basi uamuzi wa "Wengi Wape" uamue nani akae hapo? Kwanini utake yule unaemuona wewe kua anafaa ndo awe anafaa na Kwa wengine hata kama sio ridhaa yao?
Halafu wanakuaga na dhiki balaa, kuna Mtendaji mmoja juzi ananililia shida nikamtukana kimoyomoyo huku usoni najifanya kumuonea hurumma
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom