Dar, Mlimani City: Yaliyojiri Mkutano Mkuu wa CHADEMA leo tarehe 04/08/2020

Roving Journalist

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
596
1,000
Salaam Wakuu,

Leo Vikao vya Chanma cha CHADEMA vinaendelea Jijini Dar es Salaam. Na leo ni mkutano Mkuu wa CHADEMA.

Tutawalea Updates ya kile kitakachojiri kutoka Mlimani City.

Leo Tarehe 4, Agosti 2020, Mkutano Mkuu wa Chama una kazi ya kutekeleza kazi zake, ikiwemo “kuteua mgombea wa Urais na mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar,” inavyoelekezwa kwenye ibara ya 7.7.10 (c). Halikadhalika, Mkutano Mkuu wa Chama utainidhinisha Ilani (manifesto) ya Chama kwa Uchaguzi Mkuu, kwa mujibu wa ibara ya 7.7.10 (h).


1596527465562.png

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chadema unaofanyika leo Agosti 4, 2020 katika ukumbi wa Mlimani City.

UPDTAES:
= > Viongozi (Wajumbe) wa Mkutano Mkuu wa Chadema wameanza kuingia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kushiriki Mkutano huo, leo Jumanne 4 Agosti 2020.

= > Shughuli rasmi inatarajia kuanza hivi punde
Ratiba nzima ya mkutano wa leo
 • Viongozi wataingia
 • wimbo wa taifa na dua ya ufunguzi
 • Utambulisho wa wajumbe​
 • Utambulisho wa wageni waalikwa​
 • Salamu kutoka kwa wageni waalikwa​
 • Hotuba ya ufunguzi​
 • Kuthibitisha Ajenda​
 • Kuidhinisha ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama​
 • Kuzindua Chadema Digital​
 • Wenyekiti na Makatibu wa kanda kueleza walivyojiandaa na Uchaguzi​
 • Uteuzi wa ugombea Urais wa Zanzibar, makamu wa wa Rais na Rais ya Muungano​
 • Hotuba ya Makamu wa rais​
 • Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano​
= > Burudani zinaendelea kwa sasa wasanii mbalimbali wakitumbuza na kuimba nyimbo za chama.

=> Viongozi mbalimbali waliotia nia pamoja na viongozi Wakuu wa Chama wameshaingia ukumbini kwa wimbo rasmi tayari kwa ajili ya kuanza shughuli hii ya leo.

= > Wimbo wa taifa unaimbwa

= > Viongozi wa dini wa kiislamu na Wakristo wamepewa nafasi ya kufanya dua kwa ajili ya kufungua Mkutano huu.

Utoaji wa Akidi
Katibu Mkuu (John Mnyika) amekaribishwa kwa ajili ya kutoa akidi ya Mkutano huu:
Katika hatua ya sasa nifanye kazi mbili tu. Mosi, kuwatangazia kwamba mpaka sasa ndani ya ukumbi huu kuna jumla ya wajumbe1001 ya mkutano mkuu wa chama kati ya wajumbe 1080 sawa na asilimia 92.6 kwa hiyo akidi ya mkutano huu imetimia ni halali kwa M/ kiti kuendelea na hotuba.

Jambo la pili, Mkutano huu unakutano huu umekutana kwa mujibu wa ibara ya 7.7.10 cha katiba ya chama. Ni mkutano maalumu ambao baraza la jana limekubaliana kuwa na ajenda kuu mbili.

Ajenda za Mkutano
 • Kuidhinisha ilani ya Uchaguzi Mkuu ya 2020 ya chama cha Chadema
 • Kuteua Mgombea wa Urais na Mgombea Mwenza kwa JMT na Mgombea Urais wa Zanzibar
Mkutano huu wa chama utahusisha vilevile kuzindua wa Chadema Digital Arm ambayo itatumika kwa kutumia teknolojia ya kisasa kuongoza mapambano ya kidemokrasia ya kuhakikisha tunashinda kwa kuwa na rasilimali za kutosha, kuwa na uwezo wa kuwasiliana na mambo mengine ambayo mtano chama kimejiandaaje kushinda uchaguzi.

Mnyika ameeleza kuhusu suala la Uhujumu wa Wagombea unaofanya na Tume ya Uchaguzi katika ngazi mbalimbali. Katika kukabiliana na jambo hili kama chama Mnyika amesema "Kwakuwa sasa basi ni muhimu nguvu ya umma ianze kuonekana kuanzia kwenye hatua ya kuchukua fomu mambo yote yafanyike hadharani.

Kwahiyo naomba kutangaza katika Mkutano huu, Mnamo tarehe Agost, 8 saa tano kamili Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema atakwenda kuchukua fomu, tukio hili litafanyika Dodoma.

Lakini naomba kutangaza vilevile tarehe 12 Agost ambayo ni siku ya kwanza ya uchukuaji fomu za Ubunge na Udiwani nchini Wagombea wa Chadema na viongozi wa Mkutano Mkuu mjiandae kuhakikisha tunakuwa wa kwanza kabisa kuchukua fomu nchi nzima kwa nguvu ya umma.

= > Baada ya kutolewa kwa akidi kwa sasa ni utambulisho wa Kanda mbalimbali, ikiwamo Kanda Maalum, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyasa, Kanda ya Pemba, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Unguja, Kanda ya Kati na Kanda ya Viktoria.

= > Utambulisho wa Wajumbe wa kamati Kuu

= > Utambulisho wa Wajumbe wa Bodi

= > Utambulisho wa baadhi ya wageni waliohudhuria, wamo Viongozi kutoka Chama cha CCK wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Nabu katibu Mkuu wa Chama cha Chauma Ndugu Kabendera, Viongozi wa Chama cha UMD wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu, Viongozi wa Chama cha Sauti ya Umma, Wawakilishi kutoka shirika la Waldafu, Wawakilishi kutoka Taula, Wawakilishi wa Shirika la KYO, Uwakilishi wa Diaspora, Msajili wa Msaidizi wa Vyama vya Siasa Ndugu Nyahoza, Joseph Butiku, Mjumbe wa Kamati kuu wa ACT Wazalendo Maalimu Seif Hamad.

Salamu zilizotolewa na Baadhi ya Wawakilishi wa Wageni Waalikwa
Muwakilishi kutoka TAMWA

- ametoa salamu, amesisitiza kuwa wao kama wanawake wanaweza kwa hivyo wasiogope.

Muwakilishi kutoka WiLDAF
- Ametoa salamu kwa kushukuru kupewa nafasi na kuwapa moyo wanawake. Amesisitiza kuwa anataka aone ilani ya Chadema ipoje na namna gani ilani hiyo inawapa nafasi wanawake katika kugombea nafasi mbalimbali.

Muwakilishi kutoka TLS
- Jebra Kambole ametoa salamu kwa niaba ya wanasheria. amewatakia heri Chadema na maamuzi mema.

Muwakilishi kutoka Taasisi ya Mwalimu Nyerere
- Mzee Butiku amepeta nafasi ya kutoa salamu kwa kutoa shukrani kwa kupata nafasi ya kukaribishwa hapo. Amesisitiza misingi ya taasisi yao na malengo ya taasisi hiyo tangu ilipoanzishwa.

- zaidi ya hayo Mzee Butiku amesema Uchaguzi wa mwaka 2020 ukiwa wa Uhuru, Uwazi na Haki utatupatia viongozi bora

Muwakilishi wa Vyama vya Siasa ametoka Chama cha ACT Wazalendo
- Maalim Seif Hamad ametoa salamu kwa kuwapongeza Chadema kwa kuandaa Mkutano mkubwa wenye viwango pamoja na kumpa pole Tundu Lissu kwa matatizo yaliyomkumba. Amesisitiza kuwa Tanzania mpaka sasa hakuna Tume Huru.

- Ametoa wito kwa Chadema tusitegemee kama tume itafanya haki isipokuwa wajipange kuwa endapo watashinda asiwepo wa kuzuia ushindi huo. Asisitiza Wapinzani kuungana ili wawe wamoja ili wapate ushindi.

Hotuba ya Ufunguzi
Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amekaribishwa kwa ajili ya kutoa hotuba ya ufunguzi.

Ameanza kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwakutanisha katika Mkutano huo sambamba na kuwapongeza Wanachama wote na Viongozi wa Chama kwa harakati walizozifanya kukipigania chama licha ya magumu na maumivu waliyopitia.

Akiongea na Muwakilishi wa Tume Huru ya Uchaguzi Mbowe amesema "Na ndugu yangu Sisti amesema mara kwa mara yeye ni mwenyeji katika vikao vyetu tunakukaribisha sana. Lakini tunapenda kurudia kwamba tunafanya wajibu huu kwa maumivu makubwa sana, hawa watu kwa niaba ya Mamilioni ya watu wanalia rohoni na unajua hilo.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ipo 'biased' ina upendeleo wa wazi ambao haujifichi. Tunaitaka ofisi ya Msajili isiipendelee Chadema, ipendelee haki katika taifa letu. Nyinyi kama regulators muone haki ya Vyama vyote vilivyo na dola na visivyo na dola inapatikana.

Tunalitamani taifa lenye upendo na mshikamano. Siku zote Chadema tumekuwa tunatanguliza jani la Mzaituni, ili kwamba pamoja kwa taifa hili iwe ni nchi yenye furaha. Nchi hii ina maumivi, nchi hii ina msiba. Robo tatu ya viongozi walio katika mkutano huu wana kesi mahakamani. Navyozungumza Binti katibu Mkuu wa Baraza la chama chetu Chadema Rusnat Anji na mwenezi wa Baraza wa Taifa na viongozi wengine tisa katika mkoa wa Singida wako mahabusu kwa zaidi ya mwezi mmoja hawapewi dhamana.

Napenda niwaambie viongozi wa Serikali, amani ya nchi hii haipo kwa sababu tuna Majeshi, amani ya nchi hii imekuwepo kwa sababu tumekuwa wavumilivu. Matendo mbalimbali tunayofanyiwa na Taasisi ambayo tulizitegemea zitumike kuijenga amani ya nchi yetu, kuanziba Bunge, wakati mwingine hata Mahakama, Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, wasiojulikana. Tunapitia madhila mbalimbali sana tunakwenda kwenye uchaguzi tunashindwa kujiandaa na uchaguzi kwa sababu tunajiuliza tutafikaje kwenye uchaguzi. Nchi ipo kwenye state of fear.

Watanzania wanalazimishwa kuwa na mapenzi kwa Watawala, mapenzi bandia. Chadema tunakubaliana kabisa na kauli aliyoitoa Mzee Butiku aliyezungumza (amani, umoja na maendeleo ya watu) na nakubaliana na maneno ya Maalim Sharif Hamad.

Msajili anazungumza habari ya sisi kuheshimu sheria wakati anajua tunatunga sherias katika nchi hii ambazo ni sheria mbovu kwa makusudi. Kuendelea kuheshimu sheria za ukandamizaji ni Injustice to our People.

= > Mbowe amkaribisha Odela mbele tena

Akimfafanulia Odela Mbowe amesema "Chadema tunataka kuliunganisha taifa, ulipokuwa unazungumza walipokwambia sasa basi ukafikili wamekuzuia kuzungumza. Tunakupenda sana na tunaheshimu kazi yenu.

Azma ya kuitafuta dola ya nchi hii sio kwenda kulipiza kisasi. Azma ya kuitafuta dola ya nchiyetu ni kwenda kutengeneza mfumo mbadala wa kiutawala utakaotoa haki kwa Watanzania wote wakiwemo Wanachama wa Chama cha Mapinduzi. Hatuna azma wala muda wa kulipiza visasi. Na asiwepo Mwanachadema yoyote ambaye anafikiri kuwa chama hiki tumekipigania ili kulipiza visasi.

Sisi tumechagua wajibu wa kusema, wapo wengi wanaogopa kusema. Tumeamua kuchukua wajibu wa kusema hadharani na kuzikubali risasi kwa sababu tunafikiri tusiposema mawe yatasema.

Ndugu Viongozi wa Mkutano MKuu Tumekutana hapa leo kwa sababu ya mambo makubwa matatu. Kwanza mkutano huu una wajibu wa kufanya uamuzi wa mwisho kwa ajili ya chama ni nani wanakwenda kupeperusha bendera ya chama chetu katika wajibu mkubwa ulio mbele yetu. Pili, kuwatuma viongozi wetu wakaitambue ilani ya chama chetu. Tatu, kuzindua rasmi platform wa Chadema Digital ambao utakiongoza chama hicho ndani na nje.

Maalim Seif amezungumza kuhusu ushirikiano. Tutapa taarifa ya Kanda zetu kumi za Chama, tutapata vilevile taarifa za Mabaraza ya Chama, ni namna gani Mabaraza yamejiandaa kwenda kwenye ushindi. Na tunawaambia tena Serikali kama wamezoea kufanya utani kwenye masuala ya haki za watu sasa basi.

Wale wenye roho nyepesi wamekwishaondoka, kuna watu mkiki huu uliwashinda. Kwahiyo sio kweli kwamba Magufuli ni hatari wakati wote wakati mwingine Magufuli amekuwa fursa kwetu. Ametusaidia kutuondolea upupuupupi uliokuwa unatamalaki kwenye chama sasa we are solid like never before. Nimesema tunakwenda kushiriki uchaguzi with confidence, hatuendi kushiriki tunakwenda kushinda. Tunatambua mikakati mbalimbali inayofanywa na vyombo vya Dola dhidi ya ushindi wa Wapinzani, this is so sad.

Taasisi za Umma ambazo zina wajibu wa kusimamia haki kwa watu wote ndizo taasisi zinazotumika kuandaa uchakachuzi wa Uchaguzi. Tutaheshimu Sheria lakini tutaheshimu zaidi sheria bora. Mkakati wowote wa kunyima ushindi wetu sasa basi.

Hatuna ugomvi na msajili, msaidizi wake na msajili wake. Hatuna ugomvi tunayajua mazingira magumu mnayofanyia kazi japo hamuwezi kukiri. Lakini nchi hii inastahili kufika hatua ambayo Viongozi watakuwa na courage ya kukataa kutumika kama agent wa oppression. Useme kama shida ni kazi hii kazi sasa basi. Tufike mahali Watumishi wa Umma katika nchi hii wawe na hiyo Courage

Jaji wa Mahakama kuu unapewa mamlaka ya kumuumiza mtu unaumiza. Polisi mnapewa amri ya kuzuia mikutano ya nchi nzima mnazuia.
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,041
2,000
Mungu aliyemtoa Daniel kutoka kwenye Pango La Simba, Mungu aliyemponya Shedrack, Mesack na Abdnego, Mungu aliyeponya Lissu, Huyu Ndio Mungu wa kumtumikia na chama hicho nitakua chama chenye Baraka na Kubali kutoka kwake. Salamu kutoka Chattle.

Elli
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
34,322
2,000
Salaam Wakuu,

Leo Vikao vya Chanma cha CHADEMA vinaendelea Jijini Dar es Salaam. Na leo ni mkutano Mkuu wa CHADEMA.

Tutawalea Updates ya kile kitakachojiri kutoka Mlimani City.

Leo Tarehe 4, Agosti 2020, Mkutano Mkuu wa Chama una kazi ya kutekeleza kazi zake, ikiwemo “kuteua mgombea wa Urais na mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar,” inavyoelekezwa kwenye ibara ya 7.7.10 (c). Halikadhalika, Mkutano Mkuu wa Chama utainidhinisha Ilani (manifesto) ya Chama kwa Uchaguzi Mkuu, kwa mujibu wa ibara ya 7.7.10 (h).

=====

UPDTAES:
View attachment 1526675
View attachment 1526676
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chadema unaofanyika leo Agosti 4, 2020 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam
Wazee wa mbwembwe.........ila kwa pamba mnajitahidi!
 

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,235
2,000
Lisu anatosha ameonesha dhahiri kuwa anaweza kurejesha matumaini amepigwa risasi zaidi ya 16 lakini bado amekuwa imara na yuko tayari kwa mapambano watu wa aina hii ni wachache sana duniani wengi wao ni mitume na wanafalsafa
Dah, CCM wakisikia tu TL amepitishwa kuwa mgombea wanajisikia kuhara. Ni jambo ambalo hawakulitegemea kabisa!
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,965
2,000
Niwapongeze kwa utaratibu wa kisasa kabisa wa uendeshaji wa mkutano wa Baraza Kuu na Leo mkutano Mkuu.
Hakika Chadema ni Chama cha kisasa kabisa, na kumbe CCM huwa wanabebwa tuu na mkusanyiko wa Wasanii ndio maana hata hotuba za viongozi wao sehemu kubwa ni kuwasifia na kujikomba kwa wasanii hadi unaona Wasanii ndio nguvu ya Chama.
Nimefuatilia mkutano Mkuu unaoendelea sasa hivi na ikitolewa ilani ya Chama 2020-2025 na hakika inagusa nyanja zote kwa ufanisi bora sana.
Sio wanafunzi, watumishi, wastaafu na wazee, kinamama na watoto, vijana wote watanufaika sana na ilani hiyo.
Sasa ni wajibu wetu kuwapa nafasi waitekeleze baada ya wenzetu wa CCM kuanzia enzi za TANU kutupiga kabobo ya maneno kila kwenye uchaguzi.
Chadema ya sasa sio kwa wanachadema tuu bali ni ya Watanzania kwa maendeleo ya Tanzania.
chadematzofficial-___CDdma1PAwAE___-.jpg
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
5,034
2,000
Ilete hapa watu waisome acha kukaa na material kama form One unajifungia nayo chumbani paper ikija inakuchomoa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom