Ina maana kweli, kwa mjibu wa ibara 144(1) ya Katiba kama CAG akateuliwa wa umri wa miaka 20 atadumu miaka 40?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
Wapo watu ambao wanaamini kwamba mahakamani huwa hakuna haki bali kuna sheria pekee. Kwa kiasi kikubwa huwa ninakubaliana nao.

Kazi za mahakama ni kutafisiri sheria. Katiba ndiyo sheria mama au kwa jina jingine sheria kiongozi. Ni dhahiri kuwa kama sheria (na Katiba) tulizozitunga wenyewe kupitia wawakilishi wetu bungeni zina ubovu, tusitegemee sana kupata haki mahakamani. Kazi ya mahakama ni kuhakikisha sheria hazikiukwi au kuvunjwa.

Haki kupatikana mahakamani inategemea tu na busara ya mahakimu au majaji wanavyotafisiri hizo sheria na Katiba tulizozitunga hususani lengo lake hasa lilikuwa nini. Kwa mfano ibara ya 144(1) ya Katiba yetu inaeleza kuwa CAG akishateuliwa na rais atatumikia wadhifa huo mpaka umri wake wa kustaafu, yaani miaka 60 kikatiba. Kifungu cha 62(a) cha sheria ya utumishi serikalini kimeuongeza umri huo kuwa miaka 65. Hakuna ibara yo yote ya katiba inayoelezea umri wa mtu kuteuliwa kuwa CAG. Kwa hivyo mtu hata mwenye umri wa miaka 20 anaweza kuteuliwa kuwa CAG kama ana hizo sifa zingine zilizotajwa kwenye Katiba na sheria zetu. Ikitokea hivyo, ina maana kweli kwamba mtu huyo Katiba yetu ililenga aendelee kuwa CAG kwa miaka 40 mfululizo? Yaani kazi ya CAG ni milele kama vile mfalume?

Nadhani ndiyo maana kwa kuona ufa huo kwenye ibara ya 144(1) ya Katiba, kifungu cha 6(1) cha sheria ya Ukaguzi wa Umma Na 11 ya mwaka 2008 kiliweka mihura isiyozidi miwili ya miaka mitano kwa CAG kama ilivyo kwa maraisi. Akimaliza miaka 5 ya kwanza siyo lazima ateuliwe tena kwa mara ya pili kama ilivyo kwa raisi na wabunge. Bahati mbaya bunge letu baada ya kutunga hiki kifungu cha sheria ya ukaguzi wa umma, ilisahau kufanya marekebisho ya ibara ya 144(1) ya Katiba. Hiki ndicho akina Zitto na Assadi wameona ni kete. Wanajidanganya tu kwani sana sana kitakachofanyika ni bunge letu kwenda kurekebesha hiyo ibara ya Katiba. Tuliona jinsi mahaka ya katiba ilipo amuru kuhusu kuzuia wagombea binafsi kwenye uchaguzi mkuu kuwa ni kinyume cha Katiba yetu. Hadi leo maamuzi hayo ya mahakama hayakutekelezwa na baadaye mahakama ya rufaa kusema kuwa hayo ni mambo ya wanasiasa na hivyo kulachia wanasiasa. Hata hili la Zitto na Assadi ni la wanasiasa tu na litaachiwa wanasiasa.
 
Ile.kesi ya. Zito ilikuwa. Yaa. Kisiasa.
Ndiyo, na mahakama ya rufaa ya kikatiba ilishasema haishughuliki nazo. Zinatakiwa wakamalizane nazo kisiasa, hususani hilo la wagombea binafsi. Zitto na Assadi hawakupaswa kulipeleka suala hili mahakamani labda tu kama lengo lao ni kuonekana kisiasa ie kick ya kisiasa. Assadi atakuwa kapoteza hela yake bure kugharimia kick ya kisiasa ya Zitto
 
Back
Top Bottom