Imetokea loliondo

Imetokea loliondo

subiri kusikia mwingine kusema kaoteshwa na Mtume Muhamad,mwingine Mussa hadi mitume waishe.baada ya hapo hawakawii kuja waliooteshwa na Yuda iskarioti na mwisho kabisa watasema shetani katubun na karudi kundini na kaanza kuotesha watu dawa.
nadhani funga kazi atakuja ataesema katokewa na kinjekitile ngwale anatibu kwa kunywa mkojo wake.
 
Sitak kuamin kwamba maggid uwezo wa kufikiri ni mdogo. BABU ameoteshwa mia tano kwa kuwa ni hela ya Kitanzania ambayo kila mtz anaiweza kuipata awe maskin au tajiri. na khs 1USD hiyo ni currency maarufu dunian kote na inajulikana kila mahali. Tatizo lako ulitaka BABU aoteshwe Currency za kutoka UARABUNI ndo ungerizika na kuamin kama hutak kuamin kaa kimya waache wenye iman wakatibiwe, SHEIKH YAHYA YUPO KUWATIBU WATU KAMA NINYI BABU HANA MAJIN MAIMUNA.

babu a.k.a kalumanzila,
 
Majid, nadhani unakosea sana pale unapoingilia imani za watu, hebu unapokuwa ukisini na wake za watu ile siyo dhambi? Unapokuwa ukiwatenga wakristo na imani yako ile siyo dhambi! Leo unamfindisha nani kuhusu kuhusu huyu babu!
 
Chanzo cha habari cha kuaminika kinasema kuwa jana Waziri Lukuvi alitoa agizo kwenye Mamlaka ya Usalama wa Usafiri wa Anga, tawi la Arusha akitaka Safari zote za Ndege kuelekea Loliondo zisimamishwe, na Uwanja wa ndege wa Loliondo ufungwe mara moja.

Lakini pia aliagiza helikopta zote zinazotua Samunge nyumbani kwa babu zikome mara moja hadi itakapotangazwa tena.

Najiuliza sijui kama kwa suala hili Lukuvi amepata baraka za wakubwa wenzie!

Maana kwasasa Arusha imegubikwa na kelele za ndege na helikopta zisizovumilika, zote zikielekea kwa babu Loliondo, na wanaotumia vyombo hivyo ni Vogogo wa serikali na Matajiri.

Lets be patient &wait tuone kama watamsikiliza!
 
So why bother mkuu??

why dont you shut up! and do your things!

Hii ni imani na mpaka sasa umeishavuna aibu nyingi tu, you cvan not question Imani, after all wewe ni mwislamu na yule ni mkristo hauoni kwa akili ndogo kabisa mko dunia mbili tofauti?

Leo hii mtu akisikia mtume alioa wake 22, aliua, akaoa na kulala na mtoto wa miaka 9, alilala na wanawake wenye edhi, alichukua Quran toka kwenye pango, n.k haviingii akilini! Yet we have mosques kila kona na tunaenda misikitini na kurudi kwetu,...maisha yanaendelea...

Issues za Imani ni nzito sana na next time try your level best kukaa mbali navyo maana utapata aibu, nilifikiri ulipopost ile ya kwanza nilijua umepata somo, unarudia tena??

Kuwa najua mabaya ua islamu then niseme ili iwe nini?? eti babu hajaku-convince! Sheikh yahya nimsemsikia kwa masikio yangu akisema mimi naenda nyie kufeni!!!

Ni swala la mtu na ndio maana wengi wako kule na wa dini na mataifa mbalimbali HATA HIZO ARV kuna wengine hawazitaki, kuna wengine hawatumii panadol bali hedex...list of preferances goes on

sasa wewe kwa nini USEME?? ili iwe nini??


Mkuu imani yako imani gani? mpaka unasema ni masuala ya kiimani? maana mie ninavyojua kwa imani zote hakuna ambapo hapajaelezea kutokea vituko kama vya babu. Manabii wa uwongo unajua vitimbwi vyao? Unajua some times soma bible on your own usi depend sana kwa maaskofu wako, kwani wamesha haralisha mengi ambayo hayapo katika bible kama kula nguruwe, watu wa jinsia moja kuoana, kulewa, kuvaa uchi kwahiyo nakushauri kuisoma imani yako ili unapo support babu ujue unasupport imani gani. Kuna mungu asingejua kama watu watakuja kwa wingi pale? mbona hakumuotesha nalo hilo, maana mie siamini kama mungu eti angetakaa watu waje wafie pale.
 
magid huyu babu wa liliondo ana nini na wewe?...maana unamsakama sana huyu mzee wa watu.....mi nikushauri tu kama unaweza we nenda kule arusha hadi pale mto wa mbu.....na uwazuie wale wote wanaokwenda kule ....maana babu hajaita watu waende kule.
 
Maggid anakataa kuwa babu kaoteshwa na Mungu kwa kuwa Biblia inasema "Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake Yohana 5:37" Maggid anathibitisha kuwa Biblia inasema kuwa sisi pamoja na "babu" hatujapata kamwe kusikia sauti ya Mungu wala kuuona uso wake!Nadhani babu ana zaidi ya majini Maimuna Tafakari!
Unajua, mnapoquote Biblia kwa juhudi za kudiscredit mtu hapo ndipo mnapofanya makosa. Martin Luther King Jr, alipokuwa anapigania harakati za kuwakomboa Wamarekani weusi aliamini kabisa kuwa alitumwa na mwenyezi Mungu. Na hata katika hotuba yake ya mwisho alisema hivyo hivyo kama vile alikuwa nabii. Na matunda ya juhudi zake leo tunayaona. Hakuna aliyewahi kumwuliza huyo Mungu kakutumaje, umeongea naye saa ngapi. Noah aliagizwa na Mungu ajenge ark. Kwani alimwona Mungu? Mbona wakati huo hakuulizwa Mungu anafananaje? Moses aliamriwa ajenge sanamu la joka ambalo wana wa Israeli wakiliangalia watapona na adha za kuumwa na majoka msituni. Hakuna mtu aliwahi kumwuliza Moses umeisikia wapi hiyo sauti ya Mungu. Kuna mifano chungu nzima kwenye Biblia ambako Mungu anawamuru binadamu wafanye hiki na kile.
 
Majid, nadhani unakosea sana pale unapoingilia imani za watu, hebu unapokuwa ukisini na wake za watu ile siyo dhambi? Unapokuwa ukiwatenga wakristo na imani yako ile siyo dhambi! Leo unamfindisha nani kuhusu kuhusu huyu babu!

Maggid kama mwandishi wa habari anao wajibu huo. na wewe kama msomaji una wajibu wa kufuatilia alichokiandika maggid kina ukweli kiasi gani. wewe usiishie kufikiria kuwa tayari dawa ya magonjwa sugu imepatikana, fikiria zaidi ya hapo, tena kupitia imani yako wewe unayoiamini.Shetani ana vitimbi vingi sana vya kuweza kumtoa mtu katika imani yake, huo ni mfano mdogo katika vitimbi vya shetani. Jibu swali kuna mungu anayebagua watu wake katika kuwaponya? katika dawa zinazojulikana za kienyeji na hata za kitaalamu ni dawa gani ambayo ukihama nayo kutoka sehem moja kwenda sehemu nyingine haiwi dawa? hayo ni masheriti ya nguvu za giza.
 
Wewe ndo unatuchekesha! Wanaoponywa huwa hawafi? Wanaishi milele hapa duniani? Kufa ni lazima. Hata wale walioponywa na Bwana Yesu baadae walikufa. Kufa hakuzuiliki.

silly ideas!,

nakumbuka imani iliyopelekea ile vita ikaitwa ya "majimaji"
napita tu,
 
evidence plz! Vngnevyo ndo zile, zile, story za kusadkika! Mm mpk sshv nna ndg mwny sukar na presha alienda kupata kkombe bt up 2 nw bdo anaumw na amerudia dawa zake.

Jamani mimi nadhani suala la imani nalo lina umuhimu wake hapa. Inawezekana watu wanaokwenda kwa imani thabiti ya kuponywa ndiyo wanaofanikiwa. Lakini nakubaliana na hoja kwamba evidence nayo ni muhimu ili nasi angalau tushuhudie hayo maajabu ya babu.
 
Majid, nadhani unakosea sana pale unapoingilia imani za watu, hebu unapokuwa ukisini na wake za watu ile siyo dhambi? Unapokuwa ukiwatenga wakristo na imani yako ile siyo dhambi! Leo unamfindisha nani kuhusu kuhusu huyu babu!

Sio kuwa anakosea ni upumbavu tu anaoufanya, anajua kabisa pint yake ya mwanzo ilikataliwa , anachofanya ni ubishi wa kisaikolojia, ambao unazidi kumuumbua na anajiridhisha tu.

waacheni waende, furaha yao ya kupona au tu kuwa na matumaini inahitajika sana na mwingine hawezi kuwapa isipokuwa babu! let them live!
 
Ishu ya Babu wa Loliondo inaumiza kichwa kusema ukweli na kiasi fulani inakuja kwenye imani ya mtu. Binafsi niko so skeptical na huduma itolewayo huko, lakini kuna dada mmoja nilmwona kwenye CNN alisema kitu kimoja ambacho kinafanana Tna hii kesi ya huko Arusha. Kuna jamaa mmoja huko Brazil anajiita John of God, anawatibu wagonjwa kwa imani tuu na pia anafanya surgery bila ya kutumia anesthisia na wala wagonjwa hawalalamiki. Huyo dada alikuwa kwenye kipindi cha Sanjay Gupta, ambaye ni neurosurgeon by profession na alimwambia Sunjay ya kuwa simply because we can't explain or rationalize what is happening in Brazil it doesn't mean it is not HAPPENING . Wakati huo, mtu mwingine aliyekwenda huko Brazil ni Harvard doctor ambaye hata yeye alichanganyikiwa na mwisho wa siku alisema.. "THE WORLD IS MORE MYSTERIOUS THAN HE HAD UNDERSTOOD."


YouTube - CNN Investigates 'John of God' - Faith Healer Popularized by Oprah
 
Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kama ufisadi au ujanjaujanja waliokunao viongozi wetu kuna jambo la kihuni linalotokea wakati wa kunywa kikombe cha babu.
Kuna taarifa ya kuwa viongozi kabla ya kufika loliondo huwa wanatuma taarifa inayoambatana na list ya majina ya ndugu zao ambao hawatakaa foleni ya kusubiri kikombe.
Yaani fisadi ni fisadi tu hata kwenye mambo ya ki-imani!?!

Hivi babu si alisema mtu atakayeleta ufisadi hatapona!
 
Ndugu Zangu,

JANA usiku muda mfupi kabla ya taarifa ya habari, TBC1, kulikuwa na mahojiano ya mwandishi wa TBC na Babu wa Loliondo.

Kati ya aliyoyaongea, Babu anasema, kuwa Mungu ndiye aliyepanga bei ya tiba ya kikombe iwe shilingi mia tano. Kuwa alimwonyesha mia tano! Na Mungu akamwambia wageni walipe dola moja!

Tafsiri yangu;

Pamoja na kuwa mwandishi hakumuuliza Babu maswali magumu, bado Babu wa Loliondo hakunisogeza hata hatua moja kutoka kwenye msimamo wangu. Kuwa tiba ya Babu ni Abrakadabra.

Tujiulize swali moja tu; hivi Mungu huyo ni Mungu gani anayebagua waja wake. Kuwa wengine walipe mia tano na wengine dola moja?

Jamani, hivi Mungu huyu wa Babu wa Loliondo naye anafuatilia exchange rate kila siku? Itakuwaje basi, shilingi ikipanda au kushuka thamani dhidi ya dola ya Marekani? Babu itabidi aoteshwe haraka ndoto nyingine ili abadilishe bei ya kikombe!

Na kwenye taarifa ya habari iliyofuatia ikaripotiwa, kuwa Serikali imeshindwa kutoa tamko jana juu ya tiba ya Babu kwa vile Babu amesema kamati iliyoundwa iende kwanza Loliondo!

Mnajua tena mambo haya ya imani! Alitamka mwanakamati mmoja kwenye TBC1. Na leo imeandikwa kwenye gazeti moja, kuwa Serikali itatoa tamko leo juu ya tiba ya ' Babu'.

Naam. Tamko hili liharakishwe kutolewa kabla ' Babu' hajaoteshwa ndoto, kuwa ' Tamko Lisitishwe hadi itakapotamkwa tena!'. Na nani? Fikiri mwenyewe.

Si ilipata kusemwa, kuwa kila kukicha, kuna kioja kinazuka kutoka Afrika!


Maggid
Iringa,
Jumapili, Machi 27, 2011

Maggid,

Inawezekana mawazo yako ni sahihi lakini hoja yangu ipo palepale kwamba kwa mtu anayesumbuliwa na maradhi miaka na miaka lazima hatakuwa na simile ya kumwona Babu. Lazima nae ataenda akapate kikombe cha Babu ili ajaribu bahati yake. Wewe usiyeumwa huwezi kujua ni kwa nini watu wanasafiri kutoka Namtumbo mpaka Loliondo. Na sasa tunaambiwa watu wanatoka Zambia, Kenya, Uganda, n.k hadi Loliondo.
 
babu a.k.a kalumanzila,

Ha Ha Ha Haaaa!!
Acha tu nicheke maskin mpe mvinyo asahau shida zake, sijui ndugu zetu wa mataifa aka watoto wa mama mdogo wa ISAKA sijui tuwape nini msahau matatizo yenu. Miaka ya 90 Alikuja bwana mdogo aliyeongozwa na majin(yatakuwa yametoka kwa SHEIKH YAHYA) alijiita mtume katoka kwa mungu na kupachikwa jina la SHEIKH SHARRIF alisumbua sana imani za watu akipita huku na huko kuitangaza dini yake huku akitumia maandiko kutoka ktk QURAN sasa
 
jamani hii ishu ni ya kiiman zaidi, wenye matatizo ya magonjwa na ambao wamehangaika nayo bila mafanikio kama ukimwi,kisukari,na mengineo kwa iman waende tu wakajaribu bahat yao,
wewe ukiona ni chezo tu linachezwa na kalumanzila achana nalo,
mi sioni tatizo liko wapi
 
"imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana"

Kiguu na njia, I can rate your comment as the best of all and Maggid's thread the worst of all as it has NO any meaning in spiritual world but in simple mind's man
 
jamani hii ishu ni ya kiiman zaidi, wenye matatizo ya magonjwa na ambao wamehangaika nayo bila mafanikio kama ukimwi,kisukari,na mengineo kwa iman waende tu wakajaribu bahat yao,
wewe ukiona ni chezo tu linachezwa na kalumanzila achana nalo,
mi sioni tatizo liko wapi

mbona huelewek kama mufti wako uko upande upi ambao ni sahihi kwako.
 
.... Hili suala ni gumu sana kuna interest za watu wazito na linasemekana hili jambo lina mkono wa kifreemasons ndio maana babu anataka mia tano ile namba ina maana kubwa! Hili la dola moja nimelisikia hivi punde limenifanya nianze kuamini kuwa fremasons wanamkono ukiitazama ile dola moja utaona alama zao iangalie kwa makini kuna picha ya piramid juu yake kuna kama jicho! .

Shossi,

This is too low from you. Hata kama unataka kutushawishi kuwa tiba ya babu sio ya kutoka kwa Mungu, hoja nyepesi kama hizi zinavuruga jitihada hizo. Unless unasema nikienda kwa babu na coins tano za sh 100 hapokei!

Hata kama kuna mambo ya msingi 'mnayatetea', hii itafanya jitihada hizo kuonekana kama wivu tu!.

Btw, nimeona soda siku za karibuni zimewekwa bei kwenye kifuniko sh 500/=!
 
Ni iman lazima, nnachoongea ni ukwel,
hapa kazin kwetu kuna mama alienda ila bado ajapona,
ila kuna dada alimpeleka mama yke ambae amemtoa kijjn kwa mda wa miaka miwil hawez kutoka ndan kwa kuumwa, ila alipogonga kombe la babu yule maza kapona na karud nyumban kwake kijjini..
Na huyu ambae ajapona mi nna hakika na sababu maana ni mshirikina, na watu wote tunajua
 
Back
Top Bottom