Imetokea loliondo

Imetokea loliondo

je na vipi wanaokufa kwa maelfu baada ya kunywa hiko kikombe cha loliondo? Mungu akiponya kaponya!! Tafuteni kitabu kinaitwa PAMBANO KUU
 
Kwani ww Magid usipobadli msimamo wako kuhusu Babu nani anajali? Who do u think you are btw. It seems unajikweza kwamba una attention saaana kumbe we
only read your trash to laugh out loudly.

Nimekuwa nikisoma criticisms zako kuhusu huyu mzee nikashangaa . For your info. there is no more news from Babu because everybody has succumbed
to his cup including scientist. Halafu eti nawe uko mbele against udini. Funny.

Wa Mbeya na Tarakea vp nao....?
 
Mtu mzima mwandishi wa habari anachallenge babu kuchagi mia tano na dola I . Hivi ww unataka aishi vipi na hao wanaofanyakazi nae wale mawe? Kwani si sera kuwa wageni walipie huduma in dollers.? Hata huko misikitini kwako mashehe huomba sadaka maana hawafanyi kazi nyingine. I hate such poor way of writting to publoc. Crazzy
 
Tumeona wengine "wakitumwa" na Dokta wa kanono Silaa, kwenda kujiangamiza kwa kuwa watapatiwa Simenti ya elfu tano na maisha bora kwa kufumba na kufumbuwa.

Hata hawatazami huyo anaewaambia ana maisha yepi? Na yana ubora upi?

1) Mwenyekiti anadaiwa, kapata mwanya kidogo kaanza kuchota mali ya umma hataki kuirudisha, jee akipewa nchi? Hatuyaoni haya.

2) Mgombea aliebobea (Daktari) mwenye kuzijuwa sheria za kanoni anaenda kinyume kabisa na hizo sheria: a) kwa kuoa akiwa padiri b) kwa kuongeza mke c) ambae hajaachika kwa mume wa kwanza na anaishi nae kama kimada kwa sheria za kanoni. Hatuyaoni haya.
Hivi hawa wakipewa waendeshe nchi, itakuwaje? Jibu: chota mali za umma na kula sheria za "kanono".

Hivyo ndivyo tulivyo. "Wajinga ndio waliwao".

"Reality" huwa hawaioni, hawaisikii wala hawataki kuiona wala kuisikia. Inashangaza kwa wenye kuona.

kweli slaa anawapa jambajamba sana ccm... Kila kitu kinachozungumziwa hapa nchini sasa anatajwa slaa,,, huyu ndie mpinzani wa kweli,,, hakuna mfano
 
Maggid, itakuwa vizuri kwa waandishii wafatilie hali halisi ya mahospitali ili muweze kulinganisha na kabla maswala ya babu yalivyokuwa. Kuna habari za kuaminika kuwa KCMC imefurika watu wanaotoka kupata kikombe cha babu! Hospital za Arusha na Moshi yaani KCMC na Mount Meru kumekuwa na taarifa za kupokea maiti zilizokwisha kuharibika. Waandishi waisaidie jamii kujua hii hali wasitumie jina la babu kujipatia mia tano na wao kwa kuuza magazeti tu!
 
je na vipi wanaokufa kwa maelfu baada ya kunywa hiko kikombe cha loliondo? Mungu akiponya kaponya!! Tafuteni kitabu kinaitwa PAMBANO KUU

Wewe ndo unatuchekesha! Wanaoponywa huwa hawafi? Wanaishi milele hapa duniani? Kufa ni lazima. Hata wale walioponywa na Bwana Yesu baadae walikufa. Kufa hakuzuiliki.
 
Median man ni Mwizi mkubwa na inawezekiana ni mkenya sio mtanzania
 
je na vipi wanaokufa kwa maelfu baada ya kunywa hiko kikombe cha loliondo? Mungu akiponya kaponya!! Tafuteni kitabu kinaitwa PAMBANO KUU

aagh nani akitafute hicho kitabu bana!! kama unacho we kimwage hapa.....kama hauna tupe dondoo..we si ushakisoma
 
Mtabishana weee na kukabana koo bure!
Kwani imani hulazimishiwa jamani?
Nadhani kama mna mengine ya kufanya, kafanyeni yatawasaidia zaidi kuliko kuendelea kumchambua babu.
 
Maggid,

Utakufa kwa wivu, husuda na kijiba cha roho. Ulianza na CHADEMA yakakushinda, umevagaa Babu pia...yatakushinda.

Mwaka huu lazima ujinyonge tu.

By the way kwa nini usiandike historia ya chama chetu kikkongwe na biograph ya mtabiri wetu mkuu na mtoa ulinzi usioonekana kwa kingozi wetu mkuu?
 
kweli slaa anawapa jambajamba sana ccm... Kila kitu kinachozungumziwa hapa nchini sasa anatajwa slaa,,, huyu ndie mpinzani wa kweli,,, hakuna mfano

Kweli kabisa na ni Daktari wa Kanoni au kanono? Asiyefata sheria alizosomea? Au huo ni uongo pia?
 
Majimshindo usiongee kama mtu aliyekunywa uji wa magimbi.....una post kitu ambacho hakina uhusiano na mada,au mkuu wakati unamaliza kidato cha nne ulitaga??? Hapana anaongelewa mganga kijana kutoka Mbeya,aliyeoteshwa na mama yake kuwa arithi mikoba ya uganga ya mama yake....Huyu naye ni mganga kama walivyo waganga wengine wa kienyeji,guvu za matibabu yake hazishabihihani naza Babu wa Loliondo...
 
Heshima yako Maggid, Hili suala ni gumu sana kuna interest za watu wazito na linasemekana hili jambo lina mkono wa kifreemasons ndio maana babu anataka mia tano ile namba ina maana kubwa! Hili la dola moja nimelisikia hivi punde limenifanya nianze kuamini kuwa fremasons wanamkono ukiitazama ile dola moja utaona alama zao iangalie kwa makini kuna picha ya piramid juu yake kuna kama jicho! Usihadaike na kuumiza kichwa kuhusu maswala ya exchange rates kwani Mungu wa Isaya na Yakobo ni mwenye mapenzi na wanaadamu hawezi kuwapeleka sehemu inayowadhalilisha na kuishi maisha ya wanyama! Si tunasikia watu wanajisaidia porini na wanateseka kisawasawa kungoja "kikombe"? Upo wapi utu hapo? Kuna wengine humu JF wana miradi yao ya kubeba wanaoenda Loliondo kwa babu kwahiyo tegemea upinzani mkubwa wa hoja zako.

plse acha kupotosha umma au kama ujui weka hoja zako kwenye format ya swali! Ukisema tsh500 au $1 ni nguvu za giza then binadamu dunia nzima tunatafuta, tunatembea na tunaishi na giza "get behind me you satan"
 
Panga la shaba, hakuongelewa babu wa loliondo pekee, rejea post ya kwanza.

Kama wameweza kuongelewa wengine wenye nguvu na mungu, wengine nguvu za maria bikira na nguvu za majinni na wameweza kukusanya watu wengi wakawaamini. Kwa nini iwe kioja kumuongelea Daktari wa kanoni (kwa mimi ni kanono) mwenye uwezo huo huo wa kukusanya wengi kwa maneno yake. Ninachosema Jee, hatuoni vitendo vyao?
 
Ukimuona mtu na akili zake anaenda kwa babu kutafuta uzima, ujue kahangaika sana muda mrefu sasa hanabudi kuenda kujaribu ili apate uponyaji ambao kautafuta bilamafanikio kwa muda mrefu. Mtu kama maggid na wapambe wake, hawajapatwa na matatizo km ya hiv, kifua kikuu, saratani, na kisukari wakaonja adha yake.pemgine km wangeshapata wangetushuhudia kuwa wao japokuwa wanaumwa hawawezi kwenda ila wanasubiri kuendelea na mateso yao hadi wafe.... Pengine hapo wanganza nishawishi nami kwa hoja zao... Lakini kupayuka tu huku wengine wakipata taaaaaaabu kiafya haiingii akilini mwangu!!!
 
Ndugu Zangu,

JANA usiku muda mfupi kabla ya taarifa ya habari, TBC1, kulikuwa na mahojiano ya mwandishi wa TBC na Babu wa Loliondo.

Kati ya aliyoyaongea, Babu anasema, kuwa Mungu ndiye aliyepanga bei ya tiba ya kikombe iwe shilingi mia tano. Kuwa alimwonyesha mia tano! Na Mungu akamwambia wageni walipe dola moja!

Tafsiri yangu;

Pamoja na kuwa mwandishi hakumuuliza Babu maswali magumu, bado Babu wa Loliondo hakunisogeza hata hatua moja kutoka kwenye msimamo wangu. Kuwa tiba ya Babu ni Abrakadabra.

Tujiulize swali moja tu; hivi Mungu huyo ni Mungu gani anayebagua waja wake. Kuwa wengine walipe mia tano na wengine dola moja?

Jamani, hivi Mungu huyu wa Babu wa Loliondo naye anafuatilia exchange rate kila siku? Itakuwaje basi, shilingi ikipanda au kushuka thamani dhidi ya dola ya Marekani? Babu itabidi aoteshwe haraka ndoto nyingine ili abadilishe bei ya kikombe!

Na kwenye taarifa ya habari iliyofuatia ikaripotiwa, kuwa Serikali imeshindwa kutoa tamko jana juu ya tiba ya Babu kwa vile Babu amesema kamati iliyoundwa iende kwanza Loliondo!

”Mnajua tena mambo haya ya imani!” Alitamka mwanakamati mmoja kwenye TBC1. Na leo imeandikwa kwenye gazeti moja, kuwa Serikali itatoa tamko leo juu ya tiba ya ' Babu'.

Naam. Tamko hili liharakishwe kutolewa kabla ' Babu' hajaoteshwa ndoto, kuwa ' Tamko Lisitishwe hadi itakapotamkwa tena!'. Na nani? Fikiri mwenyewe.

Si ilipata kusemwa, kuwa kila kukicha, kuna kioja kinazuka kutoka Afrika!


Maggid
Iringa,
Jumapili, Machi 27, 2011


Mkuu Maggid hongera na pole kwa muda wako mzuri wa kufukuza upepo
na kisaikolojia unapata tabu kujua ukweli huu kuhusu babu na ndiyo maana
umetoa wito wa fikiri mwenyewe katika maandishi ya reds hapo juu.....

Kifupi mkuu hujafikisha lengo au kumwelewa babu na hata serikali inajua
ukweli na hata mimi pia ila tofauti na wewe kama ''great thinker'' kama jf ina-
vyotaka tuwe tunafikri.... kwamba katika masuala ya iman huwezi ukawa na
fikara yakinifu kwasababu:
1.Imani yoyote ile huwezi ukahoji juu ya fikara....you cannot reason on
faith.....fikara huishia katika upeo butu kuhoji juu ya imani ya mtu na kima-
ntiki huwa hatuwezi kupata hitimisho(conclusion) juu ya imani na ukweli
wake na ndiyo maana hata ''philosophers'' wengi waliuawa kwasababu ya kuhoji
imani kwa mfano Galileo aliuawa kwa kuhoji imani juu ya jua kutembea(movement)
ambapo wakristo waliiamini hivyo na yeye alipinga na kusema jua lipo tuli
na halitembei.
2.Kuhusu babu na tiba yake ni swala la imani na hata kama atasema kile kikombe
ni lazima kiwe cha rangi nyeupe au nyeusi kiimani yupo sahihi kabisa na hata kama
fikara zako hazikubaliani na hilo maana unaweza ukatuuliza tena kuwa kuna uhusiano
gani kati ya dawa na rangi ya kikombe cha dawa au tiba hivyo imani inabaki kuwa imani tu..kwamba doubts juu ya imani(faith) ndiyo ukamilifu wake.

3.Mkuu labda kitu ambacho ninahisi wewe hunacho katika elimu ya fikara ni
utaalamu juu ya fikara za imani na dini mbalimbali ambapo kama ungezijua basi
usingepata tabu ya kuhoji mantiki ya babu na tiba yake na pia hujachelewa anza hata leo kufuatilia masuala ya imani na uwepo wake.

4.Mwisho nahitimisha kwa kusema kwamba zipo imani nyingi kama watu kusema
ng'ombe ni Mungu, mwanadamu ni Mungu,sanamu ni Mungu,jua ni Mumgu,nyota ni Mungu,nyoka ni Mungu,maji ni Mungu,hewa ni Mungu n.k lakini pia huwezi kutumia
fikara kuhoji kwa kutumia fikara(thinking or reasoning) hivyo mwacheni babu na
dawa yake na kama utampinga wewe siyo ''great thinker'' anayejua nini maana ya
''great thinking''.

''we cannot reason on faith and this is because faith has no physical evidence on its existence.''
 
Hii thread ni crap,kama mtu huna la kufanya ni bora unyamaze. Hujalazimishwa umuamini au usimuamini babu.

Usitafute mass ya watu ikuunge mkono,kwani hamna shujaa ktk hili. Ningesema wewe ni mpumbavu,ila ngoja nikuache..
 
Hamna hiyo taarifa me niko loliondo na ni mkaz wa huku kila siku gari zinaflow kwa babu.
Kwa yeyote mwenye kutaka kuhakikisha anaweza piga simu any traffic Control Tower haswa Arusha Control Tower!Notam pia imetoka
 
Back
Top Bottom