Imetokea loliondo

Imetokea loliondo

Ya babu Loliondo tuliambiwa ni mungu kaotesha, tena wakasema neema ya mungu imeshuka Tz; ya Tarakea tukaambaiwa bikira maria na yesu ndiyo wameotesha; sasa ya Mbeya tunaambiwa ni maruani (majini) yameotesha!!!!!!; WOW!!!!!wote wameonyeshwa mizizi ya kunywesha waTz walio katika barabara ya kwenda kufa!!!!; Hivi kumbe watu wanaogopa kufa kiasi cha kuwa tayari kwa lo lote!!!!????? Sasa tumwamini yupi wanaJF????? Maana kwa wote tunaambiwa wanaponya magonjwa sugu yote!!!!!!!!!!!!!! ingawa mpaka sasa hatujathibitishiwa kwa vipimo vya hospitali kama kuna aliyeponakwa ye yote!!!!!!!!!!!! Kweli wahenga waliosema wajinga ndiyo waliwao walitabiri bila kujua Tz ya leo mwaka 2011!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Maana hapa hata sirikali ya ****** na ****** mwenyewe wote wameliwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mtu wa MUngu,
Unangoja uthibitishiwe na nani?
Siamini kama huna ndugu, jamaa au rafiki aliteenda huko Samunge!
 
Ya babu Loliondo tuliambiwa ni mungu kaotesha; Tarakea tukaambaiwa bikira maria na yesu ndiyo wameotesha; sasa ya Mbeya tunaambiwa ni maruani (majini) yameotesha; wote wameonyeshwa mizizi ya kunywesha; sasa tuamini lipi wanaJF????? Maana kwa wote tunaambiwa wanaponya magonjwa sugu yote!!!!!!!!!!!!!! ingawa mpaka sasa hatujathibitishiwa kwa vipimo vya hospitali kama kuna aliyepona!!!!!!!!!!!! Kweli wahenga waliosema wajinga ndiyo waliwao walitabiri bila kujua Tz ya leo mwaka 2011!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Na bado watazinduka wengine kudai mizizi imewatuma au maruweruwe wamewatuma.
 
Nyenyere: mimi siumwi hata nikapate kikombe cha babu, ukizingatia kwamba babu kasema kile kikombe sii kinga ila ni tiba. Kilichonisukuma kuandika ni baada ya kuona watu waliojitwalia hati miliki ya kuamua ni nani ni wa Mungu na ni nani sio. Waliopomshambulia babu wa watu kwa nukuu kibao za kumshusha shimoni bila hoja zilizo wazi. Nilipotafakari niligundua kwamba babu wa loliondo ni mnyenyekevu mno, maana kama neema ya kuponya kimiujiza aliyoipa ingelikuwa kwa baazi ya wahubiri wa mijini ninaowafahamu basi hata maisha ya fahari ya Gadaffi yangekuwa cha mtoto. Babu hajaweka mabango ya kujitangaza wala kukodi Tv za kumtangaza kama wafanyavyo wahubiri wengi na kutangaza kutoa uponyaji wa kila namna hata maombi ya kupata utajiri. Je wanasikilizwa? Sidhani kama wanasikilizwa maana kwa jinsi walivyo wengi wangesikilizwa Tanzania kusingekuwa tena na wagonjwa ama masikini. Mimi sii mshabiki wa babu ila ni mfuasi wa kweli. Kweli inasema je kuhusu kisa cha kama cha babu? Wenye hekima hawakimbilii kuhukumu bali kama Gamalieli hushauri watu wajiepushe isije ikawa wanapingana na Mungu mwenyewe. Kama jambo lililovuta hisia za wengi likichukuliwa kwa subira yenye saburi mwisho wa yote itajulikana kweli, kama ni la Mungu au laa. Au labda kuwe na jibu la moja kwa moja kwa mtu aliyefunuliwa wazi wazi kwamba Mungu amesema nae vinginevyo.
Maana unabii wowote sharti kwanza ufasiriwe na kisha upimwe kabla ya kuamuliwa ukubaliwe au la. HARAKA YA KUHUKUMU INATOKA WAPI?
Unapouliza kwamba je watu walioenda kwa babu walimwomba Yesu kwanza? Waliomba ama hawakuomba sii kazi yako, kwani hata kama wapo walioomba wewe sii mthibitishaji wa imani ya mwombaji kwa kukubali ama kukataa. Mwenye jukumu hili ni Mungu peke yake.
Kwa habari zangu binafsi mimi simwamini Mungu kwa kufuata miujiza kwani neema yake iliishakunivuta kwake na sasa sipo tena katika hali ya kumfuata kupitia hisia ama msisimko wowote. Pasiwepo na muujiza wa aina yeyote hata mbingu zigeuke kuwa shaba, bado Mungu kwangu anabaki kuwa Mungu tena mwenye kumiliki hali zote ama ni nzuri an mbaya.
Nilitamka manabii watakatifu nikaona kama wewe ni wale wanaosema kuwa mwisho wa manabii ni kwa mitume wa Yesu, na sijui pia utakuwa kwenye kundi la wasioamini miujiza ya uponyaji maana wapo wanaosema ulikomea kwa mitume wa Yesu.
Kama unabii ulikoma, simaanishi hawa wanaofyetuliwa na vyuo vya teologia, basi andiko la kwamba Yesu alipopaa aliachilia vipawa, wengine manabii, mitume, wachungaji, wainjilisti na waalimu
 
Wakati mwingine sio vibaya tukawa tunajiuliza hivi wakati wa enzi za akina Yesu Kristo na Mtume Mohamed, watu walikuwa wanaumwa magonjwa gani, na walikuwa wanatumia dawa gani? Walikuwa na hospitali za kupima viwango vya dawa walizokuwa wanakunywa? Ni nani aliyekuwa anawashauri watumie aina ya dawa walizokuwa wanakunywa?
 
Dawa ya kwanza kabisa kwa mgonjwa yeyote hapa duniani ni "imani" ya kuwa atapona. Nadhani kwa kiasi kikubwa "imani" ndio inayotuponya. Kuna watu wengi ninaowafahamu ambao ni wagonjwa wameenda kwa Babu Loliondo, leo hii huwezi kuamini, WAMEPONA. Mimi nashauri tusidharau jambo hili, inaweza kuwa ni neema ya Mwenyezi Mungu kaamua kutuletea hapa Tanzania, au ndio mkenge wenyewe, sasa ubaya wake ni kuwa, ukidharau halafu ikawa kweli, nayo ina madhara yake, maana utakuwa umekosa, lakini ukiamini, ukaenda halafu ikawa kweli, in a faida kubwa, maana utakuwa umepata ulichokuwa unakitaka.
 
Umeolewa na Wakenya nini? Mbona umeshupaa ki hivyo? Kwani wao hawana wanachopata kutoka TZ? Nina marafiki zangu wengi sana Wakenya tunaofanya nao kazi kwenye Shirika moja wakija semina huku kwetu wananihangaisha sana kuwapeleka madukani kwa ajili ya kununua Khanga na Vitenge. Kila mara wanatamani mikutano yetui tuifanyie Mwanza ili wapate bidhaa ya kupeleka kwao wewe unasemaje wewe!!!

Umewafagiliaaaaaaaaaa!! Mara panadol mara blue band sijui kitu gani kwenda zako huko!

Read between the lines!
 
mbona huna hoja yoyote? Swala la BABU kutoa kikombe halafu unasema tunawategema wakenya kwa vitu vingi!
Huyo waziri atafunga soko la kibiashara kwa mtazamo wako?
Huna jipya hebu ondoa topic.
KWANZA HUJASOMEA UCHUMI.

Read between the lines!
 
<br />
<br />
unaongea pumba tu...we huna uzalendo.nani alikwambia hapa tz panadol hatutengenezi?mara obama mara sijui ujinga gani,naona utakua na matatizo ya akili si bure.kujikomba tu kwa wakenya kaolewe basi huko

Read between the lines!
 
Huyu jamaa tangu ajiunge hapa JF yeye ni KUMPINGA tu Babu...............

Huhitaji kumwambia mtu wa makamu kama kwa babu kunafaa kwenda au hakufai............

Nikiuguliwa leo na ndugu yangu kitu kama Kansa au AIDS, unafikiri hata ntakumbuka maneno yako?

Nikienda, sina uhakika ndugu yangu atapona ila nisipoenda, NINA UHAKIKA ATAKUFA.

Na wewe tangu nijiunge, ni kunipinga mimi tu! Wanaokwenda huko sio wote wamakamu!!!!
 
Manabii wa uongo wataongezeka wakilitumia jina la bwana kuponya wagonjwa na hata kufanya mambo makubwa ya ajabu...
 
Mediaman, sikuelewi lengo lako mkuu, huna hoja nyingine? Kama babu wa Loliondo anatumiwa na shetani au ni mganga wa kienyeji wewe hiyo haikuhusu na tumeshakuchoka na umbea na majungu yako. THE JUDGEMENT DAY IS COMING,Mungu ndiye atakayehukumu acha watu wapate kikombe na watamtukuza Mungu wao wa mbinguni kwa uponyaji.... Think twice guy hii issue ingekuwa inafanywa na Mzungu au mtu nje ya Tanzania nahisi ungeipigia sana debe maana mitanzania ndio ilivyo... Kwani wanadamu waliopata ujuzi wa kugundua dawa zinatibu magonjwa mengine walipewa maono na nani? au inakuuma kwa kuwa babu kasema amepewa maono na Mungu?
Acha unafiki muda unaokaa kwenye computer ungeutumia maabara kufanyia kazi vipimo vya wagonjwa(ulijitambulisha ni mtu wa maabara hospital ya Mt Meru). Ingekua ni bora zaidi kuliko kutuzingua hapa jamvini. UNABOA MKUU
 
Ya babu Loliondo tuliambiwa ni mungu kaotesha, tena wakasema neema ya mungu imeshuka Tz; ya Tarakea tukaambaiwa bikira maria na yesu ndiyo wameotesha; sasa ya Mbeya tunaambiwa ni maruani (majini) yameotesha!!!!!!; WOW!!!!!wote wameonyeshwa mizizi ya kunywesha waTz walio katika barabara ya kwenda kufa!!!!; Hivi kumbe watu wanaogopa kufa kiasi cha kuwa tayari kwa lo lote!!!!????? Sasa tumwamini yupi wanaJF????? Maana kwa wote tunaambiwa wanaponya magonjwa sugu yote!!!!!!!!!!!!!! ingawa mpaka sasa hatujathibitishiwa kwa vipimo vya hospitali kama kuna aliyeponakwa ye yote!!!!!!!!!!!! Kweli wahenga waliosema wajinga ndiyo waliwao walitabiri bila kujua Tz ya leo mwaka 2011!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Maana hapa hata sirikali ya ****** na ****** mwenyewe wote wameliwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Ulisahau kuwa Tanzania ilonekana ni nchi ya kwanza Afrika kwa ushirikina? Usishangae.
 
umeongea ukweli kabisa kama dawa mbona mababu kibao wanazijua dawa za asili lakini kwanini watu mpaka viongozi waende kwa babu huyu tu na je tanzania ina waganga wangapi na wachungaji wangapi!
Anaejuwa kudanganya zaidi ndio atawapata Watanzania kwani wengi wameshakata tamaa ya kupata ukweli. Waianzia na Ujamaa wakadanganyika, ikaja uwazi na ukweli wakadanganyika, ikaja Maisha bora kwa kila Mtanzania wakadanganyika na sasa haya ya Maandamano na Babu wa Loliondo ndio uongo wa sasa. Wacha wajanja watudanganye na sie tuko nyuma yao.
 
Ndugu zangu,
Kumekuwa na misimamo mingi na kinzani kuhusu uwezo wa dawa ya Babu wa Loliondo kutibu magonjwa sugu. Misimamo mingine ni ya kiimani kwamba kama ni huduma hiyo inatolewa kwa imani kwa nini Babu atoze hela Sh. 500? Wenye msimamo huu wanarejea Biblia pale Yesu Kristo aliposema mmepewa bure toeni bure. Kwa hiyo, wenye msimamo huu wanasema hiyo kasoro ni dalili tosha kuwa huduma ya Babu haijatoka kwa Mungu. Lakini vilevile, wapo wanaoipinga huduma ya Babu siyo kwa imani bali kwa mtazamo tofauti kwamba hiyo ni biashara kama zilivyo biashara zingine tu. Hao wanasema Babu ametumia ujanja wa kuweka gharama ndogo sana ya tiba ambayo ni Sh. 500 lakini ana uhakika na msururu wa wateja utakaojaa kuitaka tiba hiyo unatosha kumfanya yeye awe tajiri pengine kuliko wote katika nchi hii. Hao wanasema hesabu za Babu zimejikita katika uwingi wa watu wanaosumbuliwa na magonjwa ambayo Babu ameyatangaza kuwa anatibu.

Ni jambo lililo wazi kuwa hivi sasa nchi yetu na pengine Dunia nzima afya limekuwa ni suala linaloisumbua sana jamii. Magonjwa ya ukimwi, kisukari, pumu, kansa, n.k. yanasumbua na kupoteza maisha ya watu wengi. Hali hii pengine kwa nchi yetu ni mbaya zaidi kutokana na huduma za afya kuwa duni sana. Na ndiyo maana viongozi takriban wote na wananchi wa kawaida wenye uwezo wamekuwa wakienda nchi za nje kufuata tiba bora. Sasa katikati ya hali hii anapojitokeza mtu wa aina ya Babu akatibu wagonjwa na wagonjwa hao wakashuhudia hadharani kwamba wamepona tena siyo mmoja wala wawili, ni wengi, unatarajia mwitikio utakuwaje?

Ndugu zangu tusidanganyane tena tuache porojo. Inawezekana tunafanya hivyo kwa sababu tuna afya njema. Hatujui kuumwa maana yake ni nini. Kwa mtu ambaye miaka yote amekuwa akiumwa tena kuumwa haswa na amekuwa akiombewa na kupata tiba kila hospitali kubwa hapa nchini bila mafanikio, anaposikia wagonjwa wenzie wamepona unatarajia nini? Kwa nini nae asiende kujaribu kama alivyojaribu kwenye hizo hospitali na hayo maombi? Kwa nini aendelee kutegemea tiba ambazo miaka na miaka zimeshindwa kumponya?

Kuna shemeji yangu ambaye amekuwa akisumbuliwa na ukimwi kwa miaka takriban saba. Mkewe alifariki kwa ugonjwa huo. Sasa ni wikiya tatu tangu apate kikombe cha Babu amecheki afya yake hospitalini yupo negative. Hospitali ya kwanza ilikuwa ni Agakhan Dar es Salaam, ya pili ilikuwa ni Regency na ya tatu ni Burhan. Sehemu zote ni negative. Pia, kuna watu wameshuhudia wamepona kisukari, pumu na vidonda vya tumbo. Acheni wagonjwa waende bwana. Wanaokufa ni kutokana na uchivu wa safari ya njia ndefu na mbovu. Muhimu ni kwa ndugu kuhakikisha kuwa mgonjwa aliyezidiwa anaenda kwa Babu huku akiendela na tiba.
 
vivuli vya vyeti vya hospitali kabla na baada ya kikombe viko wapi sasa?
 
Thanx for sharing this, lakini tutaaminije bila evidence?
 
Mimi hii tiba ya babu inanishangaza sana!hv hakuna mwana Jf aliyeenda huko atuthibitishie kwa vyeti?kuna documentary moja iliwekwaga hapa jf na jamaa wa NTV inakatisha tamaa kidogo kuhusu hii tiba,bado nina mashaka mashaka.
 
evidence plz! Vngnevyo ndo zile, zile, story za kusadkika! Mm mpk sshv nna ndg mwny sukar na presha alienda kupata kkombe bt up 2 nw bdo anaumw na amerudia dawa zake.
 
Back
Top Bottom