Imeniuma sana, mke wangu anatembea na baba yake mdogo

Imeniuma sana, mke wangu anatembea na baba yake mdogo

Wanajamvi nimekuja na simanzi kubwa sana moyoni. Sijawahi kuumia kiasi hiki, maelezo ni marefu lakini ngoja nifupishe ili nisiwachoshe.

In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume. Ingawa mazingira ya kikazi yametufanya tuwe mbali kidogo lakini nmekuwa najitahid kufika kwake mara kwa mara sababu sio mbali sana(sisi ni watu wa Kanda ya Ziwa ki-makazi lakini sio kwetu).

Tatizo limekuja kuna tetesi nilipewa na dada yake kuhusu mahusiano kati ya mke wangu na mzee mmoja mwenye umri wa miaka 46. Mbaya zaidi ni baba yake mdogo na mke wangu ingawa walikwishatalakina na mkewe ambaye ni mama mdogo wa mke wangu kitambo kidogo kimepita.

Chanzo cha wao kukutana ilikua mke wangu ali carry somo moja apo UDSM ikabidi arudi kufanya hio course basi huyo mzee akamchukua aende nyumbani kwake amuangalizie wanae huku akienda chuo basi mchezo ukaanzia apo mzee kamrubuni mke wangu kuanza kutoka nae.

Kama mwanzo nilivoeleza, dada wa mke wangu aliniambia hicho kitu ila nikapuuzia sababu huwa na tabia ya uchonganishi pia huwa mahusiano yetu sio mazuri.

Nilichoamua nikafanya uchunguzi mwenyewe kwa njia zangu ninazozijua nikagundua ukweli. Mimi ni mtu wa IT basi nakaja kugundua hata baadhi ya vitu kama simu, camera, mavazi na pesa mke wangu analeta huwa vinatoka kwa huyo mzee maana nlikua napatwa shaka na spendings zake kulingana na kipato chake cha ualimu.

Basi tumeenda hivo lakini ndani kukawa na visa kikitoka hiki kinakuja kile ikafikia akaanza kuninyima sex anadai simfikishi wakati namjua vzuri na huwa namfkikisha, kwa hilo sina shaka hata tone.

Nikirudi nyuma kidogo mimi ndio nimemsomesha chuo tangu mwaka wa kwanza mpaka kamaliza na nimegharamika mambo mengi juu yake. Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4 sasa.

Muda huu na andika post hii mke wangu yupo Dar, nimemuuilza yupo kwa nani hasemi. Nimeumia sana ikabidi niongeee na mama mkwe nikamueleza situation. Akampigia simu mwanae, kilichofuata akanitusi na kunitamkia maneno ambayo yamenichafua sana nafsi yangu.

Namnukuu "Unampigia simu mama akusaidie nini?, kama nato** si mimi wewe inakuhusu nini? Na nakuapia lazima nit**we huku ili utulie."

Imeniuma sana mpaka sasa moyo wangu umefunga siwez tena tena endelea nae ingawa nampenda na bila mimi asingekua hapo alipo leo" Nimejizuia sana kulipa kisasi nimeshindwa ukizingatia familia yao nimeibeba sana kwa mambo mengi.

Nikumbushe kitu, ukwel ni kwamba nilikuwa sijatoa mahari mpaka sasa ingawa tuliishi nae kama mke na mume. Lakini mpango ulikua mwezi huu na nilikua nimekwisha andaa kila kitu. Hata nashindwa nianze vipi kuwaeleza wazee.Nina mengi nimeyaruka kuyaeleza maana mimi si mwandishi mzuri. Natamani ningemsimulia mtu aandike.

Naomba ushauri wenu wadau na maswali pia kama yapo ila kama nitapata mtu wa kunipa njia nzuri ya kisasi nitafurahi.

Asanteni

Kaka kuishi kanda ya ziwa naona hakujakusaidia kabisa,ni kwa muda gani umeishi huko kwetu?
Pole sana kwa dharau za maneno ya hovyo aliyokuonyeshea huyo mkeo.
 
Tulia kwanza usifanye maamuzi ukiwa Na hasira maana utafanya maamuzi yasiyo sahihi muombe sana Mungu ikiwezekana funga katika maombi Mungu atakushindia kila kitu kinasababu labda Mungu anataka kukuepusha Na laana ya Jambo Fulani ndio maana katumia MTU Wa familia yao kukufunulia Mungu utuonyesha mambo magumu yanayoumiza ili tuepukane Na vitu Fulani simama omba Mungu atakushindia jua kuna vitu lazima vitokee hili mambo mengine yafanyike jiulize kwanini Mungu amemtuma ndugu Yake kipindi hiki unachotaka kuoa kwa nini iwe sasa tafakari muulize Mungu atakujibu
 
In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume.
Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4 sasa.

Mh! sijakuelewa hapo!

Hata hivyo una bahati sana. Wengine wanatembea na baba zao wa kuwazaa kabisa. Kama ulikuwa hujui ndio sasa umeyaona. Haya ni mambo ya kawaida sana katika dunia hii. Sisi wengine tunakushangaa. Hatujaona jipya hapo katika hii dunia.
 
In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume.
Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4 sasa.

Mh! sijakuelewa hapo!
miaka 3 yote aliku chuo tume ishi nae baada ya chuo.
 
Wanajamvi nimekuja na simanzi kubwa sana moyoni. Sijawahi kuumia kiasi hiki, maelezo ni marefu lakini ngoja nifupishe ili nisiwachoshe.

In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume. Ingawa mazingira ya kikazi yametufanya tuwe mbali kidogo lakini nmekuwa najitahid kufika kwake mara kwa mara sababu sio mbali sana(sisi ni watu wa Kanda ya Ziwa ki-makazi lakini sio kwetu).

Tatizo limekuja kuna tetesi nilipewa na dada yake kuhusu mahusiano kati ya mke wangu na mzee mmoja mwenye umri wa miaka 46. Mbaya zaidi ni baba yake mdogo na mke wangu ingawa walikwishatalakina na mkewe ambaye ni mama mdogo wa mke wangu kitambo kidogo kimepita.

Chanzo cha wao kukutana ilikua mke wangu ali carry somo moja apo UDSM ikabidi arudi kufanya hio course basi huyo mzee akamchukua aende nyumbani kwake amuangalizie wanae huku akienda chuo basi mchezo ukaanzia apo mzee kamrubuni mke wangu kuanza kutoka nae.

Kama mwanzo nilivoeleza, dada wa mke wangu aliniambia hicho kitu ila nikapuuzia sababu huwa na tabia ya uchonganishi pia huwa mahusiano yetu sio mazuri.

Nilichoamua nikafanya uchunguzi mwenyewe kwa njia zangu ninazozijua nikagundua ukweli. Mimi ni mtu wa IT basi nakaja kugundua hata baadhi ya vitu kama simu, camera, mavazi na pesa mke wangu analeta huwa vinatoka kwa huyo mzee maana nlikua napatwa shaka na spendings zake kulingana na kipato chake cha ualimu.

Basi tumeenda hivo lakini ndani kukawa na visa kikitoka hiki kinakuja kile ikafikia akaanza kuninyima sex anadai simfikishi wakati namjua vzuri na huwa namfkikisha, kwa hilo sina shaka hata tone.

Nikirudi nyuma kidogo mimi ndio nimemsomesha chuo tangu mwaka wa kwanza mpaka kamaliza na nimegharamika mambo mengi juu yake. Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4 sasa.

Muda huu na andika post hii mke wangu yupo Dar, nimemuuilza yupo kwa nani hasemi. Nimeumia sana ikabidi niongeee na mama mkwe nikamueleza situation. Akampigia simu mwanae, kilichofuata akanitusi na kunitamkia maneno ambayo yamenichafua sana nafsi yangu.

Namnukuu "Unampigia simu mama akusaidie nini?, kama nato** si mimi wewe inakuhusu nini? Na nakuapia lazima nit**we huku ili utulie."

Imeniuma sana mpaka sasa moyo wangu umefunga siwez tena tena endelea nae ingawa nampenda na bila mimi asingekua hapo alipo leo" Nimejizuia sana kulipa kisasi nimeshindwa ukizingatia familia yao nimeibeba sana kwa mambo mengi.

Nikumbushe kitu, ukwel ni kwamba nilikuwa sijatoa mahari mpaka sasa ingawa tuliishi nae kama mke na mume. Lakini mpango ulikua mwezi huu na nilikua nimekwisha andaa kila kitu. Hata nashindwa nianze vipi kuwaeleza wazee.Nina mengi nimeyaruka kuyaeleza maana mimi si mwandishi mzuri. Natamani ningemsimulia mtu aandike.

Naomba ushauri wenu wadau na maswali pia kama yapo ila kama nitapata mtu wa kunipa njia nzuri ya kisasi nitafurahi.

Asanteni

Pole sana mzazi! Hivi kama huwezi kumuacha au kumtaliki mwanamke kwa sababu ya uzinzi utamuacha lini na kwa sababu ipi nyingine!? Anafanya kitu hicho kwa sababu zake mahsusi iwe za kuwa sex maniac au kipato cha ziada, huwezi kumbadilisha kirahisi kama hutaki kuchizika au siku moja kuja kujikuta una kesi mbaya ya jinai, au kumbaka, au shambulio la aibu au hata kumtoa roho!?! Piga teke aondoke haraka sana ili uanze healing process , kumsahau na kuanza maisha mapya bila yeye au na mtu mwingine atakayekupenda, kukuamini na kukuheshimu. Mind you the beautiful ones are not yet born! Piga moyo konde mtoto wa kiume, kanyaga twende, wachana na hilo pepo. Best wishes.
 
You have nailed it.
Niongeze kitu hapo mimi nime lelewa na mama wa kambo baada ya mama yangu kufariki, maisha nliyo yapitia sikupenda mwanangu aishi tena nliteseka Sana

Mkuu pole sana yani imeniuma utadhani nimetendewa mimi hayo madhila, kuna mahala ulikosea katika kanuni za kummiliki mwanamke ila sitazungumzia hilo kwa sasa maana sio muhimu.
Kwakuwa sisi wote wakiume ngoja nikupe siri ya kuzishinda stress za wanawake washenzi maana pia nmekutana nao mara kadhaa maishani.
Kwanza hakuna adhabu nzuri mno kwa mwanamke kama kupiga kimya, awkward silence, pindi akifanya upuuzi wa aina yoyote ile. Huwa inampa tafsiri itakayomchanganya sana akili yake mbaya zaidi ukifanya hivyo kwa muda mrefu au mazima kabisa atajuta na kuumia zaidi kwa kuwa umempuuza kitu ambacho wanawake wote duniani hawakipendi. Uzuri wa adhabu hii inaonesha ni jinsi gani una ukomavu kama kidume badala ya kumpiga au kurushiana maneno.

Lakini pia, nahitaji ukomae sana kuushinda moyo kipindi hiki man, kumbukumbu za mapenzi yenu zitakujia sana na utatamani kumpigia umbembeleze ukidhani itasadia kumrejesha. Usifanye hivyo tafadhali, zingatia sana hilo man. Itakuwa rahisi sana kwako kumuacha aende kuliko kung'ang'ania arudie kukupenda. Fanya yote yatakayoweza kuondoa mawazo juu yake ila kwa wakongwe huwa tunatumia strategy ya kuopoa mwanamke mwingine chap wa kupoozea maumivu.

Kingine ni mtoto wako, una jukumu la kuhakikisha mnnakula bata sana mkiwa pamoja nae kwa kipindi chote ambacho unajiweka sawa kuanza mwanzo mpya, kama una ndugu yako unaemuamini waweza mpeleka akaishi nae kwa muda wakati unajipangia mkakati wa namna utakavyomlea baada ya kupata mwanamke mwengine mwenye kujielewa. Tafta beki 3 utaekuwa umempa jukumu la kumtunza mtoto kipindi hiko ukiwa mawindoni, choose the finest woman down to earth ni ngumu ila jitahidi bado wapo.

Ni pm nikupe tips juu ya kummiliki mwanamke bullar
 
Msondo ngoma waliimba. Kinachonishangaza ndugu sama, unang'ang'ania mpenzi asie kupenda, kilichobaki oa mwingine.
(masharubu) Kwakua bado unampenda mkeo, vumilia, jaribu kumuomba mungu atakusikia.


(momba) mambo hayo yanatokea, mara nyingi kwenye ndoa, nayo husababishwa na wanandoa wenyewe, sababu ya tamaa ya pesa au uroda.
 
hiyo avata yako ina ujumbe ndani yake..... anyway huyo mwanamke hakufai, fikiria your kid.... hao ni viumbe hatari sana.
 
Pole. Ukishirikisha ndg na jamaa watakushauri ujinga wa kusamehe na kuwa na subira. Mwanamke akishafika hapo latu harudi nyuma. Yatajirudia rudia.siku hazigandi.... Songa.mbele
Mungu amekufunulia hayo ili uchukue hatua. Ukishindwa kuchukua uamuzi wa kumwacha utajuta.
 
Avatar yako inaonyesha na wewe mtu wa wanawake sana, na siku zote kwenye mahusiano kila mmoja anavutia kwake,sikiliza moyo wako maana hatujui kati yako ww na yy nani msaliti
 
huyo ni baba mdogo wa damu au kimjini mjini??kama amekutamkia maneno hayo basi jua huyo hakufai achana nae kabisa japo inauma
 
acha kumuita mke keshakuwa mamdogo huyo, we tafuta size yako upunguze stress za kumsomesha mamdogo
 
baba usipoteze muda na huyo mwanamke ilimradi ushatoa mambo yake kwa mama mkwe...ukweli ujulikane tu af usepe uwe huru..usilete mambo ya nampenda sanasasa.....tafuta mtot mwingine.....kweli makucha huonekana baadae...ndio anakutamkia hayo sijui lazimanito** afa na baba mdogo duh...laana hii
 
Sio mke huyo, mkuuu. Ila yatakiwa kuwa mpole piga zako kimya achana nae huyo dunia itamfunza hata usihangaike na visasi

Tafuta namna ya kule kid wako
 
Tupa kule kamanda.
Kheri nusu shari kuliko shari kabisa.

Ukipoteza pesa kulipa mahari na kufunga ndoa utakufa kwa presha
 
bila mimi asingekua hapo alipo leo

Mkuu...katika vyote sina ushauri ila kwa hili lazima niseme.

Mungu amekutumia kufikisha riziki kwake na kwa familia yake. Amini usiamini, hata isingekuwa wewe kama alipangiwa kupata elimu hiyo angeipata. (refer hadithi yangu ya WATOTO 100)

Baada ya kusema hayo ushauri wa mapenzi/mahusiano huwa ni mgumu sana. Kinadharia ningeweza kusema hapo huna chako ila bana mapenzi!!!! Tulia utafakari sana uamue mwenyewe bila/kwa ushauri kidogo saaana kutoka kwa watu.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Back
Top Bottom