Imeniuma sana, mke wangu anatembea na baba yake mdogo

bullar

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
9,454
20,800
Wanajamvi nimekuja na simanzi kubwa sana moyoni. Sijawahi kuumia kiasi hiki, maelezo ni marefu lakini ngoja nifupishe ili nisiwachoshe.

In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume. Ingawa mazingira ya kikazi yametufanya tuwe mbali kidogo lakini nmekuwa najitahid kufika kwake mara kwa mara sababu sio mbali sana(sisi ni watu wa Kanda ya Ziwa ki-makazi lakini sio kwetu).

Tatizo limekuja kuna tetesi nilipewa na dada yake kuhusu mahusiano kati ya mke wangu na mzee mmoja mwenye umri wa miaka 46. Mbaya zaidi ni baba yake mdogo na mke wangu ingawa walikwishatalakina na mkewe ambaye ni mama mdogo wa mke wangu kitambo kidogo kimepita.

Chanzo cha wao kukutana ilikua mke wangu ali carry somo moja apo UDSM ikabidi arudi kufanya hio course basi huyo mzee akamchukua aende nyumbani kwake amuangalizie wanae huku akienda chuo basi mchezo ukaanzia apo mzee kamrubuni mke wangu kuanza kutoka nae.

Kama mwanzo nilivoeleza, dada wa mke wangu aliniambia hicho kitu ila nikapuuzia sababu huwa na tabia ya uchonganishi pia huwa mahusiano yetu sio mazuri.

Nilichoamua nikafanya uchunguzi mwenyewe kwa njia zangu ninazozijua nikagundua ukweli. Mimi ni mtu wa IT basi nakaja kugundua hata baadhi ya vitu kama simu, camera, mavazi na pesa mke wangu analeta huwa vinatoka kwa huyo mzee maana nlikua napatwa shaka na spendings zake kulingana na kipato chake cha ualimu.

Basi tumeenda hivo lakini ndani kukawa na visa kikitoka hiki kinakuja kile ikafikia akaanza kuninyima sex anadai simfikishi wakati namjua vzuri na huwa namfkikisha, kwa hilo sina shaka hata tone.

Nikirudi nyuma kidogo mimi ndio nimemsomesha chuo tangu mwaka wa kwanza mpaka kamaliza na nimegharamika mambo mengi juu yake. Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4 sasa.

Muda huu na andika post hii mke wangu yupo Dar, nimemuuilza yupo kwa nani hasemi. Nimeumia sana ikabidi niongeee na mama mkwe nikamueleza situation. Akampigia simu mwanae, kilichofuata akanitusi na kunitamkia maneno ambayo yamenichafua sana nafsi yangu.

Namnukuu "Unampigia simu mama akusaidie nini?, kama nato** si mimi wewe inakuhusu nini? Na nakuapia lazima nit**we huku ili utulie."

Imeniuma sana mpaka sasa moyo wangu umefunga siwez tena tena endelea nae ingawa nampenda na bila mimi asingekua hapo alipo leo" Nimejizuia sana kulipa kisasi nimeshindwa ukizingatia familia yao nimeibeba sana kwa mambo mengi.

Nikumbushe kitu, ukwel ni kwamba nilikuwa sijatoa mahari mpaka sasa ingawa tuliishi nae kama mke na mume. Lakini mpango ulikua mwezi huu na nilikua nimekwisha andaa kila kitu. Hata nashindwa nianze vipi kuwaeleza wazee.Nina mengi nimeyaruka kuyaeleza maana mimi si mwandishi mzuri. Natamani ningemsimulia mtu aandike.

Naomba ushauri wenu wadau na maswali pia kama yapo ila kama nitapata mtu wa kunipa njia nzuri ya kisasi nitafurahi.

Asanteni
 
Pole sana Kaka,mimi sijaoa lakin kwa akili yangu na nnavojua kidini,kijamii hata kimila pia haruhusiwi kulipa kisasi,maana tayr una familia ya mtoto mmja hutakiwi kukua katika mazingira ya majuto kwa kukosa makes ya wazazi wawili calm down pls sikiliza ushauri wa watu lakini sio namna ya kulipa kisasi hawa ni viumbe dhaifu sana
 
Pole, ni part ya life yako nw. Ni ww utakayeamua nn ufanye. That's satanic work tu, just relax tu kama wiki hivi. Fanya kama hujaumizwa na matusi yake, omba kwa ajil yake. Send her gud SMSs every night.
Tafuta sehemu nzuri tulivu, ili kupumzika kutokana na stress ulizonazo nw. I'm sure baada ya muda atajutia makosa yake, be ready kumusamehe..
 
Ni vizuri kumshauri mtu kutokana na ushauri alioomba huwezi kujua wakati anaandika alikuwa ktk hali gani,pili amekiri kwamba yeye sio mwandishi mzuri!Kila mtu ana mapungufu yake,ni bora kama hauna ushauri wa kumpa mtu ukae kimya kuliko kuanza kumkejeli.
 
Mwanamke akishafikia hatua hiyo ni wachache sana ambao wanaweza kupata ufahamu wa kurudi nyuma na kuwa na mapenzi na ww kama mwanzo,kwangu mimi napenda mwanamke ambae anaweza kuniheshimu na kunipenda upendo unapotoweka na kuanza kuumizwa hua siwezi kukubali maumivu kama hayo!Maisha yenyewe mafupi kwa nini kuumizana,kwa hiyo uamuzi unao wewe kunyoa au kusuka.Muda mwingine ni wenda wazimu kufikiri kwamba mwanamke akishageuka nyoka anaweza kurudi tena kwenye hali yake,atarudi kwako tu baada ya kutendwa kule alipoenda au kutoswa.
 
Mkuu pole sana, but inaonekana mkeo heshima imeshashuka sana kwako na anajua kama unampenda sana,lakin sielew kwann ulimpigia mama yake cjui ulitegemea atakusaidiaje! ulidhan kwamb anaweza mwambia mke wako kukusaliti?nakushauri usifanye kisasi chochote lakin jitenge nae mda huu huu ambao analeta dharau kabla hajakuganda kama ruba wakati wameachana na huyo mzee wake, umesema unampenda sana lakin mapenzi yasikufanye kuwa mtumwa mkuu, anyway lkn wewe ndo muamuzi wa mwsho maana mapenzi magum sana aisee
 
Wewe si ulishaambiwa kuwa humrizishi??

Pia sex si huwa anakunyima??

Kakuapia lazima ato*****huko jiji la mwendokasi si ndio??

Mkuu wewe ulishapigwa kibuti siku mingi sema hujiongezi unajidai unajua kupendaa.

Kwanza ulitumia IT gani kumgundua ana kucheat? Ushauri wangu jiongeze lea mtoto tafuta anaerizika na wewe huyo sio saiz yako waachie wanaume wa darslam wafanye yao.

Pia ukipata buda na wewe jisomeshe zaidi kwa Hasira.
 
nme sema nna tatizo la uandishi lkn kwa mnayo yaelewa naomba mni saidie ushauri
Pole saana mkuu, husilipe kisasi utafungwa bure, wanawake wapo wengi kama vipi bora umuache, yaani huyo ameonyesha dharau kubwa, ulimbukeni unamsumbua ila atajuta hapo mbele, hizo gharama ulizotumia samehe tu
 
Back
Top Bottom