Imeniuma sana, mke wangu anatembea na baba yake mdogo

Imeniuma sana, mke wangu anatembea na baba yake mdogo

bullar
Imeeleweka zingine MBWEMBWE kifupi huna mke,usifadhaishwe na MTU uliyekutana naye ukubwañi..shukuru una mtoto mmoja wangekuwa wanne?
 
Umeandika kwa hisia Kali sana" kwa mtazamo wangu,

Pole sana kwa yaliyokukuta kijana , na hili ni fundisho kwa vijana wenzio ambao wapo ktk stage km ya kwako,

% kubwa waliowahi kuwapeleka shule hadi kupata kazi mke/ mchumba/ mchepuko relationship ili-fail kwa namna moja au nyingine

Ni vizuri kumsaidia binadamu mwenzio in the name of love but don't expect much in return.

Ushauri:
Mungu ameongea na wewe kwa lugha ambayo hujaielewa , nenda kamshukuru kwa imani yako.
 
Pole sana...kisasi sio suluhu,ila elewa kuwa M'Mungu nae ana namna ya kukuonesha kama mtu huyu anakufaa maishani au laa...Pesa si kitu mbele ya thamani yako. Kashindwa kukuheshimu wewe,je ataweza kuwaheshimu nduguzo?? Nenda kwa wakwezo muitishe kikao na yeye akiwepo na uufunge ukurasa ili isije semwa ulimtelekeza. Pole sana kaka.
 
Pole sana yangu.. kiufupi hawa viumbe ndo walivyo, ushaur wangu kwako achana naye we angalia mtoto tuuu na baada ya mda utapata mke mwema na muombe sana mungu... kuhusu suala la familia yake kwa sasa achana nayo fanya mambo yako kaka huku ukijua jukumu lako ni mtoto... ikitokea akajuta na kuja kukuomba msahamaha mwambie mimi ni binadamu kama wewe so niko tayari kukusamehe but siko tayari kurudiana na wewe.. chukua tahadhari kaka dunia imevaa shuka usije ukalamba matapishi tena.. songa mbele kaka.. nawasilisha
 
Pole sana yangu.. kiufupi hawa viumbe ndo walivyo, ushaur wangu kwako achana naye we angalia mtoto tuuu na baada ya mda utapata mke mwema na muombe sana mungu... kuhusu suala la familia yake kwa sasa achana nayo fanya mambo yako kaka huku ukijua jukumu lako ni mtoto... ikitokea akajuta na kuja kukuomba msahamaha mwambie mimi ni binadamu kama wewe so niko tayari kukusamehe but siko tayari kurudiana na wewe.. chukua tahadhari kaka dunia imevaa shuka usije ukalamba matapishi tena.. songa mbele kaka.. nawasilisha
Asante
 
halali yake coz siyo mkeo ila umezaa nae,mwache ale bata.mtoto miaka mi4 bado hujamtolea mali.
 
Mchumba hasomeshwi na kuishi na mwanamke kinyumba bila ndoa lazima ile kwako au kwake one day. KISASI kizuri ni kutafuta mafanikio ya nguvu na kisha oa mwanamke mrembo kuliko yeye na mpotezee kimawasiano usimtafute tena hata ukikutafuta yy mblock na mlee mwanao
 
Ndio maana wanawake huwa wanatudharau wanaume. tumekuwa wajinga kupita kiasi. unamuita mtu mkeo kumbe hata mahari hujatoa. unasomesha mtu hata mahari hujatoa, ndoa hujafunga nae. Ukiambiwa kuwa huyo mtoto sio wako si ndio utachanganyikiwa kabisa.
Ushauri wangu kwako ni kwamba, Muache kwa amani, kiroho safi kabisa, na usimudhuru yeye wala mtoto. Ni jambo gumu lakini jitahidi. kwa ufupi huyo mwanamke hakupendi kabisa na huyo mzee anampa jeuri sana. so achana naye.
 
Brodha...I understand the situation you are in

Ni wakati mgumu..Unaweza kufanya maamuzi ya Pupa

Lakini u need to calm down...Get ur concrete evidence...hapa inaonekana umepanic bila kuwa na concrene evidence ...hapo huna ushahidi wa mwisho kuwa mkeo anatembea na babake mdogo

Cha kufanya mpe likizo mkeo.....jitahidi kumsahau though najua ni vigumu...get a chick out there to keep you busy....then mtakie maisha mema...Duniani humu kuna wanawake wazuri sana.....why uendelee kuhangaika na wanawake wabaya?
 
Japo ukweli unauma lkn inabidi ukubaliane nao, huyo mwanamke ameshakudharau sana yani wewe unaonekana sio type yake kabisa, hivyo chukua hatua ya kuanza maisha mapya, usilipize kisasi kwani haitosaidia. Hata hao ndugu zake wanaelewa kabisa kinachoendelelea hivyo wala usihangaike kumshitakia kwao unajichoresha, be a man just move on because time is the best unswer to you and her. Wakumfikilia hivi sasa ni mtoto wako tu.
 
Pole sana rafiki,najua inauma sana na wakuambiwa hawezi kashiriki maumivu unayoyapitia ila kumbuka pia kisasi ni cha Mungu mwenyewe.
Unaweza kuingia katika kulipa kisasi ukajikuta umeingiza maumivu mengi tena makubwa zaidi ya hayo unayoyapitia sasa rafiki.

Nakukumbusha pia hakuna dawa nzuri ktk maisha ya mwanadanu hasa ya moyo kama kusamehe na kujitahidi kusahau,japo ni ngumu ila jaribu kufanya hivyo rafiki naamini utakua na amani moyoni.

Kumbuka pia unaye kijana mdogo tayari nakushauri zaidi fikiria namna ya kumlea vizuri ktk hekma na kimo akimpendeza Mungu pamoja na wanadamu.
Mungu akutangulie na kukuongoza kwa maamuzi sahihi ambayo hutajuta tena kama sasa rafiki.Pole sana.
 
NB: UKITAKA UMSOMESHE MKEO HAKIKISHA UMEMZALISHA WATOTO 3
 
Hakuna revenge ya ukweli kama kufanikiwa aisee. Sasaa wewe unakaa kuwaza nae asikie uchungu kwani ana mimba? Kwanza fanya arrangements kujua kama huyo mtoto ni wako, kishs komaa kutafuta hela. Inavyoonekana huna hela kama huyo mpinzani wako kwa mkeo.
 
Haya mambo nayajua kaka .....kwa ulivyosimulia hina ubavu wa kumuacha seems unampenda sna....hizo msg zinazokushauri unazisoma kwa jicho moja na hufiki mwisho..soma ya kwangu kwa raha..kwamba acha hasira ziishe umrudie bana kwan pamewekwa alama!!! Btw tupe huo ujanja uliotumia kama hutojali share nasi wadau wenzio
 
Pole sana kaka maana dunia hadaa ulimwengu shujaa, achana na huyo mwanamke hakufai maana ni msaliti, kwani ikiwa hujamuoa ni hivyo je ukimuweka ndani jumla si itakuwa balaa?. Pili sikushauri ulipe kisasi kwani ukimya ni jibu zuri sana kwa mpumbavu na mungu hulipa duniani, we piga kimya usimkohoe abadani tafuta mwanamke mzuri kuliko yeye siku mkikutana ashindwe hata kukupa salamu yake. Mnapochagua wanawake muwe mnamshirikisha mungu maana wengine wana vitigo vyao huko mtakuja kuumizana bure muache familia inateseka. Hebu mpotezee na uangalie maisha mengine na mwanamke mwengine tena wanaume syie si wa kulalamika maana wanawake ni wengi sana kuliko wanaume chagua mwengine huyo keshakuwa jipu, nikweli inamuma lkn mtu akishaamua kaamua ukimfuatilia zaidi sanasana atazidi kukuchefua.
 
Back
Top Bottom