Nyerere ndiye mkufunzi mkuu wa Mkapa na JK. Kwa hiyo kama wanafunzi wake wamechemsha basi na yeye si mwalimu mzuri.
Mkapa ndiye aliyemjenga Dr. Slaa mwaka 1995 pale alipomtupia virago vya uteuzi wa kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Karatu na kumkweza kipenzi chake Bw. Patrick Qorro. Vile vile Mkapa ndiye aliyeongeza sifa za mgombea Uraisi wa CCM mwaka 2005 ili kumnufaisha swahiba wake JK. Na JK miaka mitano iliyopita ametetea ufisadi kwa nguvu zote na wananchi wamepoteza imani naye. Kwa nini Mkapa asionekane ameiua ccm kwa kukusudia?
JK ccm ndiyo inamfia mikononi mwake kwa kushindwa kusoma alama za wakati na kwa kuelewa uchaguzi huu ni referendum on governance alipaswa asigombee lakini yeye kwa uroho wa madaraka alitumia madaraka yake vibaya ndani ya chama tawala na kuwazuia wana ccm wengine wasijitokeze na wasimpinge. Alipanua demokrasia ya ubunge na udiwani lakini alisita kuifikisha hiyo demokrasia kwenye nafasi ya uraisi. Kwa kubinya demokrasia ndani ya chama chake ngazi ya Uraisi na kwa kula sahani moja na mafisadi JK amechangia kulikoni
Sasa ni nani kati ya hawa abebeshwe mzigo wa kuiua ccm?
Nimechagua Nyerere.
Mwaka 1999. Saa 5 kasoro hivi asubuhi. ***** Secondari, Mbeya. Mkapa anatangaza kifo cha Baba wa Taifa. Nililia machozi. Kikwete ameanguka zaidi ya mara 10. Huwa ninawashangaa wanaolia.
Anyway. Nyerere kama muasisi ametufikisha hapa tulipo.
Amewajenga Watanzania katika nidhamu ya woga. Watanania wanasifika kwa amani na utulivu. Lakini nadhani walitakiwa kusifika kwa uoga na kutokuthubutu.
Sijui niseme nini, lakini nadhani Nyerere ni chanzo cha matatizo yetu leo hii
dakika za mwisho kabla ya kuachana nilifurahi nilipoona jamaa kakiri mbele yangu kwamba " Anatambua ya kuwa watu wengi wamepoteza matumaini na serikali iliyoko madarakani" na huo ndo ukweli!
Sasa kwanini umtukane MS? Hayo uliyoandika yanafahamika kwa kila mtu, siyo usalama tu hata jeshini wanajua hali ya serikali ni mbaya.
Jamani watu wamechelewa sana kumchoka jk mimi mwezi wa kwanza tu tayali nilikuwa nipo hoi!
Mbeya ndo usiseme wamechoka kweli wamelazimishwa kupelekewa mbolea ya Minjingu imegoma, always wanatumia CAN but kwa sasa ipo juu sana hiyo mbolea toka 30,000 mpaka 120,000. Siyo mnakaamijini huko hata hamjui tabu anayopata mkulima! Tumechoka na jk.
Malaria sugu una lolote la kuchangia katika hili? nakupa nafasi ili walau wanaokulipa kwa kuanzisha thread mbalimbali ndani ya JF waone kwamba unafanya kazi kwa kuchangia na hii! hata kama ni upupu we lete tu .....tumeshakufahamu wewe na mtu mwenye akili za kiwango gani!
Wakuu hamjasikia zile ahadi za jk? eti atajenga machinga comples 5! Hivi na ccm wamemchoka yuko peke yake anafikiriaa vitu vya ajabu! Machinga complex ndo vipaumbele vya watanzania! Haya ni maajabu ya karne. Pumba zimeanza kumwagika!
kuna washauli wake wanamhalibia jamani mi naona kama siyo akili yake vile! na usisahau Reli toka tegeta mpaka posta, barabara za juu ameludia tena. WATAKAO MCHAGUA VILAZA SANA HAO BORA YA YEYE!
wakuu hamjasikia zile ahadi za jk? Eti atajenga machinga comples 5! Hivi na ccm wamemchoka yuko peke yake anafikiriaa vitu vya ajabu! Machinga complex ndo vipaumbele vya watanzania! Haya ni maajabu ya karne. Pumba zimeanza kumwagika!