Imamu apigwa msikitini kwa kuihama CUF

Imamu apigwa msikitini kwa kuihama CUF

Haikuwa busara kwa Rais Shein kufanya tukio kubwa la kisiasa la kupokea viongozi wa kidini waliohama chama.

Wewe ndie unatatizo, aliwapokea kama Viongozi wa dini au kama wananchi wakawaida wenye haki ya kikatiba ya kuwa chama chochote.

Mtu kstukia uliberal na Uislam unakataza Uliberal sasa mnampiga wannini.
 
Ina maana CUF hawataki mtu mwenye dini ya kiislamu kuwa mwanachama wa CCM?

Kweli hivi vyama vyetu vya siasa vina udini ndani yake, jaji Tendwa kaa macho.

istoshe nyie wote mlengo wenu si ni mmoja tu wa kiliberali?!!
 
Ubaguzi wa Wazanzibari na Udini wa CUF ndio utakaopelekea Jamhuri ya Watu wa Pemba na Jamhuri ya Watu wa Unguja mara tu baada ya Muungano wa Tanzania kufa.

Mimi maombi yangu ni huu muungano ufe, halafu tuwaache wenyewe. Na mtapoanza kuuana, marufuku kukimbilia huku
ssi hatujauwa albino kwa hyo hatuna laana ya kuuwana labda tanganyika
 
Majina ya Pemba mmmh eti Faki, Mfaki nimechoka hilo eneo maziwa ng'ombe.
 
Hawana haja ya kupiga Ustaadhi kwasababu cuf ni mke wa ccm.
Katoka kwa mke kaenda kwa mume.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Imamu wa msikiti wa Maziwa Ngo’mbeKisiwani Pemba, Omar Hussen Said (42), amepigwa na kujeruhiwa jicho baada yakutokea vurugu ndani ya msikiti wakati wa ibada ya Ijumaa iliyopita.

Vurugu hizo zimesababishwa na baadhi ya waumini wa msikiti huo ambao wanapingaImamu Said kuendelea kushika wadhifa huo kutokana na kitendo chake cha kujivuauanachama wa CUF na kujiunga na Chama tawala CCM mwaka huu.

Alisema wakati Imamu Said akitoamawadha ya Ijumaa katika membari ya msikiti, alivamiwa na kuanza kupigwa nakujeruhiwa jicho la kushoto na kutibiwa katika Hospitali ya Micheweni
CHANZO: NIPASHE
 
Tupambane na wahalifu na siyo kila tukio kuvishwa kofia ya udini.
 
Napinga kwa nguvu zote siasa za kuumizana. Kama mtu hawezi siasa akae mbali. Hivi hawa hawajui kama wako kwenye Serikali moja? Sasa ugomvi wa nini?
 
Inabidi kufanya juu chini kuhakikisha muungano unadumu,maana ukifa watatusumbua sana kuomba hifadhi kama wakimbizi wa kivita!nakushauri tusiwakatie tamaa wariberali hawa!!!

Mkuu, muungano ukidumu hawatapata akili hawa. Wataendelea kututukana kila leo na kusema tunafaidika nao. Sasa ni wakati wa kuwaonesha kuwa hatuishi kwa kula mwani wala karafuu, wabaki kwao na sisi tubakie kwetu.

Kama kutusumbua mbona hata sasa wanatusumbua, mi nikiona nyumba moja inakaa familia 7 na kila mtu ana watoto 9-13 pale Buguruni, Ilala na Kariakoo, naona ni uchafuzi wa mazingira kwa uzazi wa Kipemba
 
Tupambane na wahalifu na siyo kila tukio kuvishwa kofia ya udini.

Watu wamepigana msikitini sababu za kisiasa, hiyo haina tafsiri nyingine zaidi ya UDINI. Kwa nini wasipiganie sokoni? Acha unafiki, wewe ndio unavika dini za watu kofia ya uhalifu, wenyewe wako kwenye ibada zao za kawaida wewe unaita uhalifu
 
IMAMU wa msikiti wa Maziwa Ngo’mbe Kisiwani Pemba, Omar Hussen Said (42) amepigwa na kujeruhiwa jicho baada ya kutokea vurugu ndani ya msikiti wakati wa ibada ya Ijumaa Juni 7 mwaka, imefahamika jana.

Vurugu hizo zimesababishwa na baadhi ya waumini wa msikiti huo ambao wanapinga Imamu Said kuendelea kushika wadhifa huo kutokana na kitendo chake cha kujivua uanachama wa CUF na kujiunga na chama tawala CCM mwaka huu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishina Msaidizi (ACP) Mohammed Shakani, amethibitisha kutokea kwa vurugu hizo na watu watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na shambulio dhidi ya kiongozi wa dini Zanzibar.

Aliwataka watuhumiwa hao kuwa ni, Mfaki Ali Juma, Faki Ngome Juma na Abdallah Masoud, wote wakaazi wa Maziwa Ngo’mbe Wilaya ya Micheweni.

ACP Shakani, alisema kwamba Jeshi la Polisi linamsaka Mbwana Haji Mbwana ambaye ametoroka kwa kukimbilia kisiwani Unguja muda mfupi badaa ya tukio hilo.

“Watuhumiwa watafukishwa Mahakamani Jumatatu wakati Jeshi la Polisi tukiendelea kumsaka Mbwana Haji Mbwana ambaye ametorokea Unguja,’alisema ACP Shakani.

Aidha alisema kwamba tangu imamu Said kuamua kujivua uanachama wa chama cha wananchi CUF na kujiunga na CCM kumeibuka kikundi cha waumini ambao wanapiga kuendelea kuwa imamu wao kutokana kutokana na kitendo hicho.

Akifafanua kuhusu vurugu hizo, alisema kwamba wakati Imamu Said, akitoa mawadha ya Ijumaa katika membari ya msikiti alivamiwa na kuanza kupigwa na kujeruhiwa jicho la kushoto na kutibiwa katika hospitali ya Micheweni kisiwani Pemba.

Hata hivyo alisemas kwamba vurugu hizo zilithibitiwa na haraka kwa kutumia mtandao wa askari kazu waliokuwa wameimarisha ulinzi katika misikiti mbali mbali wakati wa ibada ya Ijumaa.

Alisema kwamba watu wanao tuhumiwa kuhusika na vurugu hizo wamekamatwa na kufunguliwa mashitaka katika kituo cha Polisi Micheweni.

Alisema kwamba Imamu Said anaendelea vizuri baada ya kupata tiba katika hospitali ya Micheweni wakati polisi inaendelea kumsaka mtuhumiwa mmoja.

ACP Shakani amewataka wananchi Kisiwani Pemba kujiepusha na vitendo vya kuchukua sheria mkononi kwa vile vinakwenda kinyume na misingi ya utawala wa sheria.

Imamu Said ni kati ya wanachama 30 wa Chama cha wananchi CUF waliamua kukiama chama cha wananchin CUF na kujiunga na CCM na walipokelewa Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM DK Ali Mohamed Shein Mey mwaka huu.

Pamoja na sheria Namba 5 ya vyama vya siasa ya Mwaka 1992 kukataza nyumba za ibada kutumika kwa shughuli za kisiasa bado tatizo hilo limendelea kujitokeza na kuathiri viongozi wa dini ikiwemo kupigwa risasi na kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi, amewataka wananchi Mkoa humo kujiepusha na vitendo vya vurugu ikiwemo kuchukua sheria mkononi.

Source: Nipashe

​
Amestahili kibano kikali zaidi kwa kukihama "chama cha DINI yetu" na kujiunga na chama cha mashetani aka CCM.
 
Watu wamepigana msikitini sababu za kisiasa, hiyo haina tafsiri nyingine zaidi ya UDINI. Kwa nini wasipiganie sokoni? Acha unafiki, wewe ndio unavika dini za watu kofia ya uhalifu, wenyewe wako kwenye ibada zao za kawaida wewe unaita uhalifu

Kweli umetoka pabaya, mbona umejawa jazba wewe unafikiri uhalifu kwa binadamu yeyote unaruhusiwa kama ukitokea kanisani au msikitini???????????????????? Kama unaelewa uelewe namaanisha tupambane na hawa wanapjificha kwenye vivuli vya dini au siasa kudhuru wenzao Burudika na goma la Prof J linalosema HAPO VIPI HAPO SAWA
 
Back
Top Bottom