Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,804
- 145,637
Yaani huu ndio upeo wa hoja zako? Siamini kuwa binaadamu hungangania kitu hata kama kimechuja.
Pengine hukujijua kuwa uthibitisho wa kuwepo kwa mungu ni uwepo wako wewe? Usishangae na wala usilazimishe vitu wakati wewe mwenyewe umeumbwa katika mambo ambayo huwezi kuyagusa. Uthibitisho wa kuwepo kwa mungu ni uwepo wa wewe na kama unabisha basi thibitisha kuwa picha fulani au video fulani inaonyesha kuwa wewe huwezi kuwa kithibitisho cha kuwepo mungu.
Ninachokwambia mimi ni kuwa Mungu kakuumba nawe kataa na uniambie wewe umeteremkaje sijui wapi?
Uwepo wangu unathibitishaje kuwepo kwa mungu, twende point moja baada ya nyingine.
Uwepo wangu unathibitishaje kuwepo kwa mungu?
Ukisema hivi bila kunionyesha ni vipi wewe ndiye unayelazimisha.
Nithibitishie kwamba mungu kaniumba, kwa mifano isiyokiukika.