Huu uzi unaelekea kusikojulikana.
Ninaamini Mungu anaishi na ndiye muweza wa yote.
Naamini kuwa Mungu wangu yuko katika nafsi tatu - Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Na hizi ni nafsi tatu, Mungu mmoja.
Naamini kuwa Yesu ndiye Mungu wangu na ndiye mwenye mamlaka Mbinguni na duniani. Tena ndiye anayeokoa hata leo.
Naamini NENO la huyu Mungu wangu, Yesu Kristo linalosema;
"Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli"
Na kwamba;
"Mungu hachunguziki"
Na kwamba;
"Niliyowafunulia ninyi ni ya kwenu ninyi na watoto wenu"
Na kwamba;
"Mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu"
Na kwamba;
"Kwa Bwana Yesu kila goti litapigwa"
Na kwamba;
"Lisilowezekana kwa wanadam, kwa Mungu linawezekana"
Hivyo basi;
Ikiwa mtu haamini kuwa Mungu anaishi na ili aamini kuwa anaishi anataka kuthibitishiwa kama aulizavyo KIRANGA, mimi nasema hili kwa imani yangu kwa huyu Mungu wangu haliwezekani maana "hachunguziki".
Na ikiwa ili KIRANGA au yeyote asiyeamini kuwa Mungu yupo ataamini kwa kutaka kuthibitishiwa basi hilo halitatokea.
Na kwa mantiki hiyo, ni heri kufunga mjadala huu kwa kuacha asiyeamini uwepo wa Mungu aendelee kutoamini na aebdelee kumdhihaki Mungu ambaye mimi naamini yupo.
Na ikiwa anamdhihaki Mungu ninayemwamini kwa vile "hachunguziki", basi sio ajabu akiamuni kuwa mimi ninayemuamini huyo Mungu ambaye yeye hamuamini, kuwa mimi ni mjinga. Aendelee kuamini hivyomaana uthibitisho anaoutaka ili aamini hataupata maana hili linawnda kinyume na maana halisi ya imani kwa Mkristo - kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo (yasiyoonekana au yasiyothibitishika).
Kwa sababu hiyo;
Haipo sababu ya kuendelea kupoteza muda kwa kuulizana maswali ambayo kwa hakika majibu yake imiwa sharti ni kuthibitisha Mungu yupo, hayatapatikana.
Hii ina maana;
Anayeamini moyoni mwake kuwa yuko sahihi basi afurahie kuwa ni mshindi au muelewa kuliko yule anayeamini vinginevyo.
Mimi najua;
Mungu ninayemwamini hachunguziki. Na hakuna anayelazimishwa kuamini uwepo wa Mungu. Ni hiari. Hivyo ikiwa asiyeamini uwepo wa Mungu kwa sababu tunaoamini hatumthibitishii hilo na akaona tunaoamini ni wajinga yeye ndiye mwerevu, je hili linapunguza nini? Na aendelee kuamini hivyo. Haidhuru. Yeye ni mshindi.
Lakini, nasema tena;
Haiwezekani kuthibitisha uwepo wa Mungu kwa namna ya kibinadam wanaotumia milango mitano ya faham kutambua. Kumtambua Mungu kunahusisha imani na imani haithibitishiki maana ni hakika ya mambo yasiyoonekana.
Kuna sababu ya kuendelea kuulizana Mungu yupo au hayupo? Mimi nasema hakuna sababu. Ila anayeona kuna sababu na aendelee, ila nina hakika uzi huu unaelekea kusikojulikana.
Dotnet.