Basi sawsawa mkuuT
Tuendelee kuombeana uzima ...
Tanzania kubwa mzee,, ni eneo gani exactly km hutojaliHapa hapa Tanzania ... ulifikiri wapi tena?
ooh so Italian pub ilihamia Mz sio,,HUku ni Rocky city mkuu
Nitarejea kaka kuna kitu kilitokea nilikuwa sipati notifications za tagsNilikuwa naambiwa na watu kuwa kuna mchezo wa watu kupotea hasa usiku wakiwa wanaelekea majumbani kwao.
Jumamosi ilinitokea yaani nilikuwa nimebakiza kama nyumba moja tu kufika nyumbani; sikufika na badala yake nilijikuta natembea kwenye mashamba makubwa tu na nilikuwa nasikia sauti za watu lakini siwaoni.
Nilifika sehemu nikakuta watu wamekaa wamezunguka moto mkubwa, nikataka kuwasalimia ili niwaeleze kuwa nimepotea lakini nikapiga moyo konde nikapitiliza.Ilikuwa kama saa nne hivi usiku.
Baada ya kuzunguka sana nilijikuta niko pale pale nilipopotelea, nyumba moja toka nyumbani kwangu na hapo ndo walipotokea watu wanne wakaniuliza ninahangaika na nini usiku mbona sifiki.
Mmoja aliniuliza kama kweli napafahamu nyumbani kwangu nikamwambia napafahamu ... akanambia ''NENDA"
Nilipofika nyumbani nilikuwa nimechoka sana.
Hivi ni mchezo gani huo wanaofanya hawa jamaa? Nilipojaribu kuwauliza jamaa zangu wakanambia eti nisimwambie mtu kwani nikisema hali itajirudia tena!
Ebu niishie hapa ila nilichokigundua ni kwamba Afrika kuna teknolojia ya ajabu lakini haitumiki kwa faida.
Hapa mshana Jr naamini utakuwa na la kunishauri.
Nakuja bestMshana Jr njoo.
Ila hapo kwenu kuna watu wachawi sana. Nasikia historia ya hapo ni kwamba, waliokuwa wanafukuzwa kwa ajili ya uchawi huko kwao miaka hiyo, mfano wenyeji wa Nasa na sehemu zingine walikimbilia hapo, enzi hizo pakiwa mapori. Ndio maana wanapaita I... kwa watu wazito.
Pole sana.
Karibu City Centre wameanza mambo yao hapa viwanja vya nane nane.