Iliwahi kukutokea?

Iliwahi kukutokea?

Kama ulivuta bangi na ilikua ni Mara yako ya kwanza inaweza ikawa sababu
 
Nilikuwa naambiwa na watu kuwa kuna mchezo wa watu kupotea hasa usiku wakiwa wanaelekea majumbani kwao.
Jumamosi ilinitokea ... yaani nilikuwa nimebakiza kama nyumba moja tu kufika nyumbani; sikufika na badala yake nilijikuta natembea kwenye mashamba makubwa tu na nilikuwa nasikia sauti za watu lakini siwaoni.
Nilifika sehemu nikakuta watu wamekaa wamezunguka moto mkubwa .. nikataka kuwasalimia ili niwaeleze kuwa nimepotea .. lakini nikapiga moyo konde nikapitiliza ... ilikuwa kama saa nne hivi usiku.
Baada ya kuzunguka sana .. nilijikuta niko pale pale nilipopotelea .. nyumba moja toka nyumbani kwangu na hapo ndo walipotokea watu wanne wakaniuliza ninahangaika na nini usiku mbona sifiki. Mmoja aliniuliza kama kweli napafahamu nyumbani kwangu nikamwambia napafahamu ... akanambia ''NENDA"
Nilipofika nyumbani nilikuwa nimechoka sana ...
Hivi ni mchezo gani huo wanaofanya hawa jamaa? Nilipojaribu kuwauliza jamaa zangu ... wakanambia eti nisimwambie mtu kwani nikisema hali itajirudia tena!
Ebu niishie hapa ila nilichokigundua ni kwamba ...
Africa kuna teknolojia ya ajabu lakini haitumiki kwa faida. ....

Hapa mshana Jr naamini utakuwa na la kunishauri.
Hukuweza hata kupiga simu kutafuta msaada?
 
Kama ulivuta bangi na ilikua ni Mara yako ya kwanza inaweza ikawa sababu
Sikuwahi kuvuta bangi na sina mpango huo ....
Nilikuwa sijanywa hata bia ...
Nilikuwa na akili zangu timamu ... lakini ghafla nilijiikuta niko sehemu nisiyoielewa ...
 
Mshana Jr njoo.
Ila hapo kwenu kuna watu wachawi sana. Nasikia historia ya hapo ni kwamba, waliokuwa wanafukuzwa kwa ajili ya uchawi huko kwao miaka hiyo, mfano wenyeji wa Nasa na sehemu zingine walikimbilia hapo, enzi hizo pakiwa mapori. Ndio maana wanapaita I... kwa watu wazito.
Pole sana.
Karibu City Centre wameanza mambo yao hapa viwanja vya nane nane.
Kumbe na wewe ni wa huku,karibu Italian Pub au huku chini Ndama mida ya jioni upate bia moja mbili
 
Ujinga tu,unajaribu kuongeza chumvi kuhalalisha kupotea kwako. Ww ulipotea tu,hakuna tecnolojia yoyote iliyotumika. Ulipotea pengine ni mgeni lile eneo au km ni mwenyeji basi una matatizo ya kupoteza kumbukumbu. Na tatizo la kupoteza kumbukumbu si unajua ni tatizo la kwenye ubongo!?? Ndo maana unaweka visingizio ili usionekane mjinga. Au pengine una mawazo ya kuumiza sana ambayo yanakufanya usiwe makini. Njia nzuri ya kutibu tatizo lako,ni kukubali kuwa una hilo tatizo na ukiendelea kukataa unatengeneza mazingira ya kuja kupotea jumla na kuwa kichaa kamili.
Haya mambo yapo sana,kwa kua wewe hayajakutokea usiwabishie yaliyowakuta
 
NAKAZIA! Watu wengi wanaugua magonjwa ya akili lakini wapo wachache magonjwa haya hujidhihirisha kwa muda mfupi na kupotea.
Nna jamaangu enzi hizo tukifanya kazi ya kusambaza bidhaa za vyakula za jumla, sasa sehemu ile tulishakaa zaidi ya miaka miwili.
Cha ajabu siku moja tumepiga kazi hadi saa tano asubuhi mimi nikarudi dukani(ofisini kwa bosi wetu kupeleka hela za mauzo) tangu saa tano hiyo hadi saa nane jamaangu hajarudi.
Ghafla nikamwona amepitia speed na baiskeli pale barabarani/nje ya ofisi huku akionekana kuchoka sana, nikachukua phoenix yangu nikamfukuzia speed nakawa namuita huku yeye akionekana kutojali ile sauti yangu wakat ni rafikiangu sana.
Nikaongeza speed nikampita alafu nikaenda kusimama mbele yake huku nikitegema atasimama anianbie kulikoni tangu saa tano hajarudi kazini.
Kusimama vile jamaa alionekana kuwa kama hanijui vile!
Kumbuka mimi na yeye tulikuwa tuna utani sana hivyo nikasimama mbele yake nakumtaka asimame.
Jamaa alipofika karibu zaidi na kuniona vyema akatupa baiskeli kule akaja mbio kunishukuru eti alikuwa amepotelea palepale mtaani [emoji23]
Kiujumla sikumwelewa vyema lakini alionekana alikumbwa na tatizo la kumbukumbu kwa maana mtaa ule sio mjini alafu tulikuwa tumeshakaa zaidi ya miaka miwili
 
Sikuwahi kuvuta bangi na sina mpango huo ....
Nilikuwa sijanywa hata bia ...
Nilikuwa na akili zangu timamu ... lakini ghafla nilijiikuta niko sehemu nisiyoielewa ...
Ngoja Mshanajr aje aisee unaeza kuwa ulipita makazi yasiyokuhusu
 
Haya mambo yapo sana,kwa kua wewe hayajakutokea usiwabishie yaliyowakuta
Afadhali umemweleza .... hapa mtaani kuna mtu alikufa tukamzika ... after four months akaonekana mtaani tena. Namshangaa huyu jamaa anayeleta story za ajabu.
 
Nitakuja naye hapo Italian Pub!
Nasikia wale City Centre tayari wako Nyamhongolo na wale wahudumu wao wa mwaka jana (wavaa nusu uchi). Nimeshangaa maana hata mwezi wa nane haujaanza ila wao tayari wameweka kambi pale kiwanjani.
Kumbe na wewe ni wa huku,karibu Italian Pub au huku chini Ndama mida ya jioni upate bia moja mbili
 
Nashukuru jamaa yangu .. nimefurahi kusikia sauti yako! Jioni tuko pamoja.
Jioni tukutane pale National, hoteli ya Comfort ili tukiachana pale kitu anaenda na njia yake (I mean ni katikati ya kwako na kwangu...) hahahah
 
Haya mambo yapo sana,kwa kua wewe hayajakutokea usiwabishie yaliyowakuta
Mkuu hakuna kitu hicho. Hicho anachodhani anaona ndo ujinga wenyewe,hakuna tofauti na mtu ambae anaona kisiki usiku na kuanza kukimbia akidhani anafukuzwa na kila akigeuka anaona anafukuzwa wakati kisiki amekiona maramoja tu. Wakati me nasoma primary,barabara ya kwenda shule katikati kulikuwa na pori kabla hujafika kijiji ambacho ndo kulikuwa na Shule. Karibu na barabara kwenye pori lile,kulikuwa na mbuyu mkubwa sana. Kwenye ule mbuyu,kulikuwa na story nyingi sana,nilikuwa najitahidi nikifika pale,nasimama hata nikojoe tu ili nione ile miujiza iliyokuwa inasemwa na wenzangu,cha ajabu sikuwahi kuona. Lkn me nikipita tu,wanaokuja nyuma yangu au waliopita kabla yangu,lazima watasimulia. Mara wamekuta watu wanapika,Mara wamekuta watu wanacheza,yaani ilinipa shida sana ile hali. Mpaka baadae nilipokuja kujua ni tatizo la akili. Nimesoma ile shule miaka yote 7,sikuwahi kuona chochote. Huyu baada ya kupotea,tayari fikra akazipeleka kwenye uchawi,hizo fikra ndo zimemfanya aone na vitu vingine vya kufikirika lkn kiuhalisia,hajaona kitu chochote kibaya ni Tafsiri zake tu kutokana na dhana ambayo ameijenga kichwani.
 
Afadhali umemweleza .... hapa mtaani kuna mtu alikufa tukamzika ... after four months akaonekana mtaani tena. Namshangaa huyu jamaa anayeleta story za ajabu.
eeeee kweli nimekumbuka, si yule dada ambaye alisema alikuwa Bariadi. Anaendeleaje? mume wake alikubali kuendelea kuishi naye? Ila Igoma kwenu kuna mambo mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom