Iliwahi kukutokea?

Iliwahi kukutokea?

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Nilikuwa naambiwa na watu kuwa kuna mchezo wa watu kupotea hasa usiku wakiwa wanaelekea majumbani kwao.

Jumamosi ilinitokea yaani nilikuwa nimebakiza kama nyumba moja tu kufika nyumbani; sikufika na badala yake nilijikuta natembea kwenye mashamba makubwa tu na nilikuwa nasikia sauti za watu lakini siwaoni.

Nilifika sehemu nikakuta watu wamekaa wamezunguka moto mkubwa, nikataka kuwasalimia ili niwaeleze kuwa nimepotea lakini nikapiga moyo konde nikapitiliza.Ilikuwa kama saa nne hivi usiku.

Baada ya kuzunguka sana nilijikuta niko pale pale nilipopotelea, nyumba moja toka nyumbani kwangu na hapo ndo walipotokea watu wanne wakaniuliza ninahangaika na nini usiku mbona sifiki.

Mmoja aliniuliza kama kweli napafahamu nyumbani kwangu nikamwambia napafahamu ... akanambia ''NENDA"

Nilipofika nyumbani nilikuwa nimechoka sana.

Hivi ni mchezo gani huo wanaofanya hawa jamaa? Nilipojaribu kuwauliza jamaa zangu wakanambia eti nisimwambie mtu kwani nikisema hali itajirudia tena!

Ebu niishie hapa ila nilichokigundua ni kwamba Afrika kuna teknolojia ya ajabu lakini haitumiki kwa faida.

Hapa mshana Jr naamini utakuwa na la kunishauri.
 
Pole sana
Je Ulikumbuka hata kumshukuru Mungu.?
 
Mshana Jr njoo.
Ila hapo kwenu kuna watu wachawi sana. Nasikia historia ya hapo ni kwamba, waliokuwa wanafukuzwa kwa ajili ya uchawi huko kwao miaka hiyo, mfano wenyeji wa Nasa na sehemu zingine walikimbilia hapo, enzi hizo pakiwa mapori. Ndio maana wanapaita I... kwa watu wazito.
Pole sana.
Karibu City Centre wameanza mambo yao hapa viwanja vya nane nane.
 
Uko sahihi kabisa ... ila naogopa kuja huko nane nane nisije nikapotezwa mazima!
 
Ujinga tu,unajaribu kuongeza chumvi kuhalalisha kupotea kwako. Ww ulipotea tu,hakuna tecnolojia yoyote iliyotumika. Ulipotea pengine ni mgeni lile eneo au km ni mwenyeji basi una matatizo ya kupoteza kumbukumbu. Na tatizo la kupoteza kumbukumbu si unajua ni tatizo la kwenye ubongo!?? Ndo maana unaweka visingizio ili usionekane mjinga. Au pengine una mawazo ya kuumiza sana ambayo yanakufanya usiwe makini. Njia nzuri ya kutibu tatizo lako,ni kukubali kuwa una hilo tatizo na ukiendelea kukataa unatengeneza mazingira ya kuja kupotea jumla na kuwa kichaa kamili.
 
Ahsante kwa ushauri ila kwa taarifa yako ...
Niko maeneo hayo tangu mwaka 2012; mengine siwezi kujitetea kwa kuwa una uhuru wa kuandika loloteunaloona linafaa toka kinywani mwako.
Niongeze chumvi ili nipate faida gani?
 
Zama tulikuwa na imani kuna mdudu ukimkannyaga lazima upotee hata kama umefika mlangoni kwako
 
Zama tulikuwa na imani kuna mdudu ukimkannyaga lazima upotee hata kama umefika mlangoni kwako
Hapo nilipopotelea ni njia panda ... na niliwahi kuambiwa njia panda ndo hao jamaa huwa wanaweka mambo yao ili mtu akifika hapo apotee hadi wamalize shughuli zao. Sijui ni kweli au la!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom