Iliwahi kukutokea?

Iliwahi kukutokea?

Mkuu hakuna kitu hicho. Hicho anachodhani anaona ndo ujinga wenyewe,hakuna tofauti na mtu ambae anaona kisiki usiku na kuanza kukimbia akidhani anafukuzwa na kila akigeuka anaona anafukuzwa wakati kisiki amekiona maramoja tu. Wakati me nasoma primary,barabara ya kwenda shule katikati kulikuwa na pori kabla hujafika kijiji ambacho ndo kulikuwa na Shule. Karibu na barabara kwenye pori lile,kulikuwa na mbuyu mkubwa sana. Kwenye ule mbuyu,kulikuwa na story nyingi sana,nilikuwa najitahidi nikifika pale,nasimama hata nikojoe tu ili nione ile miujiza iliyokuwa inasemwa na wenzangu,cha ajabu sikuwahi kuona. Lkn me nikipita tu,wanaokuja nyuma yangu au waliopita kabla yangu,lazima watasimulia. Mara wamekuta watu wanapika,Mara wamekuta watu wanacheza,yaani ilinipa shida sana ile hali. Mpaka baadae nilipokuja kujua ni tatizo la akili. Nimesoma ile shule miaka yote 7,sikuwahi kuona chochote. Huyu baada ya kupotea,tayari fikra akazipeleka kwenye uchawi,hizo fikra ndo zimemfanya aone na vitu vingine vya kufikirika lkn kiuhalisia,hajaona kitu chochote kibaya ni Tafsiri zake tu kutokana na dhana ambayo ameijenga kichwani.
Siwezi kukubishia kwa kuwa hatukuwa pamoja .... ila nilichokiona ndo hicho nilichokionesha hapa ili nipate kujuzwa nini kinaendelea kwenye teknolojia ya wabongo.
 
eeeee kweli nimekumbuka, si yule dada ambaye alisema alikuwa Bariadi. Anaendeleaje? mume wake alikubali kuendelea kuishi naye? Ila Igoma kwenu kuna mambo mkuu.
Umekumbuka ... alafu mtu anajitokeza na kuleta ubishi usio wa maana. Wapo watu wengine wanaongelea matukio ya ajabu katika eneo hilo la mtaani kwetu. Binafsi nilikuwa nakataa lakini nilipoona mwenyewe kwa macho yangu ... mtu tulomsafirisha akaonekana tena wakafika hata maofisa wa serikali ... sihuhitaji tena kuwa mbishi kwa mambo nisiyoyajua.
 
Afadhali umemweleza .... hapa mtaani kuna mtu alikufa tukamzika ... after four months akaonekana mtaani tena. Namshangaa huyu jamaa anayeleta story za ajabu.
Huyo bwana anaongea kweli,habari yakupotea ilinikuta na mm tena mjira ya mchana nikitoka mtaa was Kongo,kuelekea Uhuru kupanda daladala kuelekea gongo la mboto, nikajikuta mnazi mmoja baada ya kuzunguka zaidi ya masaa mawili,naniliokolewa na rafiki yangu mmoja aliekuwa anapita eneo hilo,baada yakumueleza mkasa mzima hakuamini na akataka kuondoka nikamshika shati kwamba mpaka anipeleke,nilipofika Uhuru keepleft bdo kumbukumbu iliponirudia...so nikweli huwa inatokea.
 
Siwezi kukubishia kwa kuwa hatukuwa pamoja .... ila nilichokiona ndo hicho nilichokionesha hapa ili nipate kujuzwa nini kinaendelea kwenye teknolojia ya wabongo.
Kitendo tu cha kupata wazo la kuuliza watu kuliko kutumia simu uliyokuwa nayo,kinathibitisha kuwa una tatizo la akili. Na nnakuambia ukweli mkuu,usipochukua hatua utakuja kuwa kichaa kamili...!!! Ukiwa na tatizo la aina yako,unaweza kutoka nyumbani na shoka kwenda shamba ukaiweka begani,lkn ukafika sehemu ukakutana na watu ukakaa kidogo kupiga story,ukifika shamba unataka utumie shoka lako kukata miti uliyokusudia,unatafuta shoka hulioni na unaweza kurudi hadi kijijini ukiamini pale uliposimama kupiga story ulilisahau. Ukifika pale na kuuliza ndo utajua km una tatizo la akili maana wale utakaowauliza watakushangaa kutafuta shoka wakati unalo begani.
 
Huyo bwana anaongea kweli,habari yakupotea ilinikuta na mm tena mjira ya mchana nikitoka mtaa was Kongo,kuelekea Uhuru kupanda daladala kuelekea gongo la mboto, nikajikuta mnazi mmoja baada ya kuzunguka zaidi ya masaa mawili,naniliokolewa na rafiki yangu mmoja aliekuwa anapita eneo hilo,baada yakumueleza mkasa mzima hakuamini na akataka kuondoka nikamshika shati kwamba mpaka anipeleke,nilipofika Uhuru keepleft bdo kumbukumbu iliponirudia...so nikweli huwa inatokea.
Wasiowahi kupatwa na mambo hayo bora wakae kimya ..... yupo jamaa mwingine hapa kaniPM anadai alipotea kuanzia saa 2 usiku, akajikuta kesho yake yuko hospitali ... anachokikumbuka ni kwamba alipishana na mtu amebeba kitu kama mtoto (maiti) walipopishana .. akageuka nyuma kumuangalia .. hakumuona na huo ndo ulikuwa mwisho wa kumbukumbu yake.
 
Mkuu hakuna kitu hicho. Hicho anachodhani anaona ndo ujinga wenyewe,hakuna tofauti na mtu ambae anaona kisiki usiku na kuanza kukimbia akidhani anafukuzwa na kila akigeuka anaona anafukuzwa wakati kisiki amekiona maramoja tu. Wakati me nasoma primary,barabara ya kwenda shule katikati kulikuwa na pori kabla hujafika kijiji ambacho ndo kulikuwa na Shule. Karibu na barabara kwenye pori lile,kulikuwa na mbuyu mkubwa sana. Kwenye ule mbuyu,kulikuwa na story nyingi sana,nilikuwa najitahidi nikifika pale,nasimama hata nikojoe tu ili nione ile miujiza iliyokuwa inasemwa na wenzangu,cha ajabu sikuwahi kuona. Lkn me nikipita tu,wanaokuja nyuma yangu au waliopita kabla yangu,lazima watasimulia. Mara wamekuta watu wanapika,Mara wamekuta watu wanacheza,yaani ilinipa shida sana ile hali. Mpaka baadae nilipokuja kujua ni tatizo la akili. Nimesoma ile shule miaka yote 7,sikuwahi kuona chochote. Huyu baada ya kupotea,tayari fikra akazipeleka kwenye uchawi,hizo fikra ndo zimemfanya aone na vitu vingine vya kufikirika lkn kiuhalisia,hajaona kitu chochote kibaya ni Tafsiri zake tu kutokana na dhana ambayo ameijenga kichwani.
Hayo uliyokua unafanya nilifanya pia kwenye m'buyu wa kijijini kwetu lkn sikuona kitu kwako ila nilishuhudia kwa macho yangu mtu anafukuzwa na kivuli ndio ikawa mwisho wangu wa kufanya ujinga pale na nkawa sipiti tena hapo nikiwa mwenyewe
 
Nilikuwa naambiwa na watu kuwa kuna mchezo wa watu kupotea hasa usiku wakiwa wanaelekea majumbani kwao.

Jumamosi ilinitokea yaani nilikuwa nimebakiza kama nyumba moja tu kufika nyumbani; sikufika na badala yake nilijikuta natembea kwenye mashamba makubwa tu na nilikuwa nasikia sauti za watu lakini siwaoni.

Nilifika sehemu nikakuta watu wamekaa wamezunguka moto mkubwa, nikataka kuwasalimia ili niwaeleze kuwa nimepotea lakini nikapiga moyo konde nikapitiliza.Ilikuwa kama saa nne hivi usiku.

Baada ya kuzunguka sana nilijikuta niko pale pale nilipopotelea, nyumba moja toka nyumbani kwangu na hapo ndo walipotokea watu wanne wakaniuliza ninahangaika na nini usiku mbona sifiki.

Mmoja aliniuliza kama kweli napafahamu nyumbani kwangu nikamwambia napafahamu ... akanambia ''NENDA"

Nilipofika nyumbani nilikuwa nimechoka sana.

Hivi ni mchezo gani huo wanaofanya hawa jamaa? Nilipojaribu kuwauliza jamaa zangu wakanambia eti nisimwambie mtu kwani nikisema hali itajirudia tena!

Ebu niishie hapa ila nilichokigundua ni kwamba Afrika kuna teknolojia ya ajabu lakini haitumiki kwa faida.

Hapa mshana Jr naamini utakuwa na la kunishauri.


Kuna mdudu uliuganyaga,kule kwetu upo unaweza tembea wee mpaka ukutane na mtu akuambie unaenda wapi? hapo utastuka,ikitokea hujakutana na mtu unaweza tembea mpaka chalinze
 
Sijawahi kupotea
Ila nasikia Kariakoo kuna mdudu ukimkanyaga utazunguka hadi ukome
 
Hofu na Uoga hivi vitu nivya upotevu wa muda na saaaana humpa mtu imani mfu.

Hamna kitu km iyo !!.
 
Kuna mdudu uliuganyaga,kule kwetu upo unaweza tembea wee mpaka ukutane na mtu akuambie unaenda wapi? hapo utastuka,ikitokea hujakutana na mtu unaweza tembea mpaka chalinze
Huyo mdudu ana nguvu zipi za kumpoteza mtu?
 
Sijawahi kupotea
Ila nasikia Kariakoo kuna mdudu ukimkanyaga utazunguka hadi ukome
Hakuna kitu km hicho,kariakoo km una tatizo la kumbukumbu kila siku utapotea na kusingizia mdudu. Huyo mdudu Dunia ya leo utamkanyaga wapi na watu muda wote wamevaa viatu..!?? Mkuu kariakoo ndo mji wa biashara,ndo maana eneo lote la kariakoo barabara zimepewa majina,mitaa imepewa majina ili kukurahisishia kutambua unaenda wapi na utarudi vp...lkn pamoja na yote hayo,kariakoo panahitaji umakini vinginevyo kila siku utauliza njia ya kutokea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom