Ilikuwaje siku uliyofumania/ uliyofumaniwa?

Ilikuwaje siku uliyofumania/ uliyofumaniwa?

Kuna jamaa mmoja katika mahusiano hiyo siku nikaenda kwake, akapigiwa simu akasepa akaniacha.
Mimi nina tabia moja hata nikiwa kwangu nikiwa ndani lazima nifunge mlango na funguo.

Nikawa nakaanga chips jikoni, nikasikia mlango unagongwa, nikampigia simu kumuuliza kama asharudi, akanambia bado yupo alikokwenda.

Nikasogea dirishani kuchungulia nikamuona mdada mweupee halafu mwembamba tall kavaa dera😂 nikajua hapa kishaumana.
Nikamute sikufungua mlango.
Yule dada akanambia "Please funguo mlango najua ndani upo peke yako"

Nikamuuliza unataka nini? Akanambia we fungua!
Nikanyanyuka nikaenda zangu jikoni kuendelea kugeuza chips.

Nilichosahau ni kua dirisha nimefungua kioo.
Nikasikia kama mtu anahangaika nikakimbilia kuangalia Lahaula! Yule chizi anapenya dirishani🤣
Nilipigwa na butwaa! Nikiangalia ndani nipo mwenyewe.
Unitag ukiendelea na part two..
 
Mimi sikufumaniwa ila nilifatwa live na jamaa kwamba mke anauma, niachane na mke wake mara Moja na mambo yatakuwa yameisha kabisa. Mimi bado mdogo siwezi kuhimili adhabu zake, akasema angenipa hata mdogo wake ila kwa vile nishamtoba mke wake nikae mbali kabisa na familia yake. Kuanzia hapo sikurudia tena.
Braza naye akanifata akanambia amepewa mashitaka natembea na mke wa mtu, wakinifata nikatae kata kata ila niache mara moja.
 
Back
Top Bottom