Ili ripoti ya mchanga wa Dhahabu iaminiwe, ingeandaliwa na Taasisi huru sio maafisa wa serikali!

Mimi nadhani kilichofanywa na serikali ni sahihi. Acacia walitoa data zao na kama tulikuwa na utata kuziamini tumefanya uchunguzi wetu na tumepata data zetu ambazo zinaonyesha utata mkubwa. Sasa hapo ndipo tunaita ni mgogoro na aje mtu wa tatu sasa ili tulinganishe izo data. Otherwise inakuaje rahisi mtu kuamini data za mwekezaji na hapo hapo apinge data za serikali.
 
Ama kweli wewe ni Dr Akili...!!

Sasa kama dhahabu ni ya kwenu, ikawaje mmewapa watu wa mataifa mengine kuchimba na kupeleka kwao huku ninyi mkilipwa sijui kitu gani kile..... mrahaba !??

Kama ni ya kwenu, kweli mikataba ya kuchimba dhahabu yenu mnaenda mnaandaliwa na wazungu kisha inaenda kusainiwa London tena hotelini bila hata wananchi kupitia bunge lao kujua nini kilichomo ktk clauses za mikataba hiyo ??

I think, let us pay the price of our stupid deeds .....

Naona kila dalili kuwa, pamoja na tume na kujifanya wanatishana kutumbuana, hakuna lolote litakalobadilika.....

Ni kwa sababu, mimi huwa ikifikiaga hatua ya kujadili mikataba hii ya raslimali zetu za asili inazozihusisha mult national companies, mara zote na -refer mkataba wa ufuaji umeme wa Richmond > Symbion na IPTL ambayo serikali hiihii chini ya CCM hiihii ilingia na kusaini....

Na badala yake ilishamaliza mabilioni ya dollar kutaka kuirekebisha ama kuivunja eti kwa kuiona haifai, ya kinyonyaji pasipo mafanikio huku tukiendelea kuliwa taratibu tukijiona.....!!

Sembuse hii ya madini ? Sina hakika pia kama Magufuli, atauweza mfupa huu .....

Hata hivyo, namuunga mkono na namtakia kila la kheri ktk kujaribu kwake naye....
Tumekusikia Kitaturu. Sasa unataka hali hii iendelee milele? Kuna usemi fulani wa pwani 'Mzigo mzito mpatie Mnyamwezi utafika'. Sasa tumempata huyo mnyamwezi, kuwa na imani mzigo utafika.
 
Kamati iliyoundwa kuandaa taarifa kuhusu mchanga wa Dhahabu katika makontena imejaa maafisa wa serikali ambao kiapo chao kiko kwa mwajiri wao,haitarajiwi wafanye insubordination kwa kupinga hoja za mwajiri wao ambaye kuna video na maandishi yanamnukuu akiwa tayari na jibu kuhusu mchanga huo.

Kwa ushauri wangu,serikali haiwezi kuwa na kesi halafu ikaiamua yenyewe,

Yaani serikali inalalamika kuibiwa,mgodi unasema hauibi,ni nani mtu wa kati wa kuwaamua watu hawa wawili? Mtu wa kati aliye huru na asiye na hofu ya kufutwa kazi kwa atakachoandikwa na atakayekuwa na uwezo wa kukataa maelekezo kutoka popote pale na kwenye utaalam wa kutosha(sio wa kufundisha madarakani tu?) Ni wazi wajumbe wengi wa kamati ni maafisa waajiriwa katika idara mbalimbali serikalini na watarudi katika ajira zao baada ya ripoti,na mkuu wao wa ajira ndiye aliyewapa ujumbe wa kamati!!

ilitakiwa Taasisi huru ya kimataifa,isiyoegemea upande wa mgodi wala serikali iteuliwe,ipewe kazi ya uchambuzi

Hawa maafisa wa serikali waliojaa kwenye kamati tena bila uwakilishi wa migodi ni ngumu kuwaamini,

Huu mchezo lazima uanze upya na utafika mbali!!

Na kuna upande utalipia gharama kubwa kama fidia!!
Serikali haiwezi kujipima unaongea nini wewe? Haki za asili kwa nani wakati unaochunguzwa ni mchanga siyo watu.

Huu utetezi hauna miguu ya kusimamia kabisa.
 
Katika hili LAZIMA NISEME,Hakuna kampuni ya Madini hata moja inayopata hasara kuchimba madini Tanzania wanapata faida ya kufa mtu Ndugu zangu pitieni Taarifa za kampuni moja tu ya SHANTA GOLD katika Mgodi wa LUIKA halafu sikilizeni Taarifa zao wanakotoa pesa ndio hasira ziwapande zaidi,halafu tujiulize Tanzania ina migodi mingapi?hawa jamaa wameweza kuzalisha Ounce 500,000 kwa mwaka 2016 na kwa bei ya sasa ni $1259.57 kwa Ounce ambapo ni sawa na $Mil 629,785,000 kwa TZS 1.385,527,000,000 ikumbukwe 1 Ounce = 28.3495231 Grams ambapo ni Gram 14,175,000 au Kilo 14,175 ambazo ni Tani 14.18 hivi

Asante sana
 
watetezi wa majambazi ya rasilimali zetu yanaranda randa tu kusambaza sumu zao; mmefeli.
 
Tumekusikia Kitaturu. Sasa unataka hali hii iendelee milele? Kuna usemi fulani wa pwani 'Mzigo mzito mpatie Mnyamwezi utafika'. Sasa tumempata huyo mnyamwezi, kuwa na imani mzigo utafika.

No, mimi ni Mtanzania halisi, maskini kabisa wa kipato cha chini mno. Sipendi na sitaki hii hali iendelee....

Lakini, kwa mbali naona kabisa hizi ni politics zilezile za CCM..

Magufuli huyu anachokifanya ni kujaribu kukata matawi ya mti tu badala ya kukata sina la mti na kung 'oa mizizi yake kitu ambacho kimeshasemwa sana na wadau mbalimbali humu na nje huko.....

Hakuna kitu, lakini narudia tena kusema tuendeleeni kuhemka hivyohivyo na matukio lakini, the fact remains that, hatuwezi kupambana na hawa mabepari....

Tulishajinyonga kwa mikataba ambayo hawahawa kina Magufuli na wenzake huko CCM walisaini.....

Hawa jamaa siyo wajinga wa kiwango tunavyofikiri, they know exactly what they are doing na wanajua fika engo watakayotunyongea.....

Mimi yangu macho na masikio.........namtakia kila la kheri and....... the drama continues............
 
Kwani hiyo dhahabu ni ya kimataifa? Dhahabu ni mali yetu, sisi tunakagua/ kuchunguza mali yetu. Tukigungua wanatuibia tunawatimua. Full stop. Tunaweza hata kuwalaza lock up kwa kosa la wizi na sheria inachukua mkondo wake. Mwizi popote hana immunity in front of the law.
Unaakili sana my brother.. I was about to say the same thing..thanks and be blessed
 
Mimi nadhani kilichofanywa na serikali ni sahihi. Acacia walitoa data zao na kama tulikuwa na utata kuziamini tumefanya uchunguzi wetu na tumepata data zetu ambazo zinaonyesha utata mkubwa. Sasa hapo ndipo tunaita ni mgogoro na aje mtu wa tatu sasa ili tulinganishe izo data. Otherwise inakuaje rahisi mtu kuamini data za mwekezaji na hapo hapo apinge data za serikali.

This is the point I waited to be said by someone in this discussion and you've done it bro..!!

Lakini kuna kuna watu humu instead wanatoa conclusion za ajabu ajabu tu utafikiri tumeshinda vita vile....

The fact ni kwamba, mchezo ndo tu umeanza na ni dkk ya 2 au 3 bado 87 na zile za majeruhi juu....

Obviousily mtu wa tatu hapa ni ile mahakama yao mabepari ya kimataifa ya kusuluhuhisha migogoro ya kibiashara ambako tuliipeleka IPTL na Standard Chartres Bank wakatubwaga na tunaendea kugugumilia maumivu ya mkataba ulisaininiwa na CCM na Magufuli huyuhuyu akiwemo na tunailipa IPTL kila siku zaidi ya Tshs 400M wazalishe umeme ama wasizalishe !!!

Sasa kama tunadhani, kilichoonwa na sijui tume ama kamati ni strong evidence kwamba hawa jamaa wana violate mikataba tuliyoingia nao na kwa hiyo wanatuibia, then let us go there....

But, experience ya hii kitu mimi i aniambia tunakwenda kupigwa bao tu huko tena baya la dobo, kisha tuamuliwe kulipa na gharama ya fidia ya kuzuia biashara ya watu kuendelea na zaidi kuchafua kampuni zao kimataifa na kuwatia hasara....!!

Huko sasa siyo mwendo wa tume wala ripoti ya Prof. Mruma tena, bali ni mlikubaliana nini ktk mikataba yenu, baasi....!!!

Yaani, kwangu sioni lolote litakalobadilika zaidi kwamba, hawa jamaa (wazungu) ni wajanja kutuzidi kwa mbali sana na ktk haya ambayo maskini kina Prof. Muhongo na wengine tayari wameshakuwa mbuzi wa kafara kwa hasira za papo kwa papo za msukuma wa Chato !!!
 
Kaka una-refer kwa Tanzania ama nchi nyingine? Maana Tanzania hakuna kitu kama ku-adhere to professionalism.
Naona kamati imefanya kazi yake vizuri kulingana na hadidu za rejea walizopewa. Tatizo ni pale unapogundua kuwa hadidu za rejea hazijazingatia utaalam
We acha aendelee na vituko vyake,huku ilani ya ccm ameshindwa kuitekeleza
 
Ni mali yetu watanzania. Tulijaariwa na Mwenyezi Mungu kama ambavyo waarabu walijaariwa mafuta. Dhahabu ni ya watanzania. Si ya hao wazungu wako. Na wala si yako maana wewe si mtanzania, haikuhusu na ni bora ungekaa kimya tu.
Pole kwa kuishi kwa mazoea kifupi huna dhahabu aisee maana hata kile kilicho chako chaweza kuwa si chako pale wenye nguvu ya kukipata na kukifanya chao wanapo kuwepo
 
Unapotoa bei ya dhahabu ili kujustify kuwa kampuni inapata pesa nyingi sana basi ni muhimu pia kuambatanisha na gharama za uzalishaji kwa kila ounce. Ni angalizo tu...
Ndugu hio ndio shida ya wabongo. Wao ni kukurupuka tuu. Wao kitu wanachoangalia ni unazalisha kiasi gani halafu wanatimes na bei bila kuangalia bei ya uzalishaji, mishahara ya wafanyakazi na .........
 
Kamati iliyoundwa kuandaa taarifa kuhusu mchanga wa Dhahabu katika makontena imejaa maafisa wa serikali ambao kiapo chao kiko kwa mwajiri wao,haitarajiwi wafanye insubordination kwa kupinga hoja za mwajiri wao ambaye kuna video na maandishi yanamnukuu akiwa tayari na jibu kuhusu mchanga huo.

Kwa ushauri wangu,serikali haiwezi kuwa na kesi halafu ikaiamua yenyewe,

Yaani serikali inalalamika kuibiwa,mgodi unasema hauibi,ni nani mtu wa kati wa kuwaamua watu hawa wawili? Mtu wa kati aliye huru na asiye na hofu ya kufutwa kazi kwa atakachoandikwa na atakayekuwa na uwezo wa kukataa maelekezo kutoka popote pale na kwenye utaalam wa kutosha(sio wa kufundisha madarakani tu?) Ni wazi wajumbe wengi wa kamati ni maafisa waajiriwa katika idara mbalimbali serikalini na watarudi katika ajira zao baada ya ripoti,na mkuu wao wa ajira ndiye aliyewapa ujumbe wa kamati!!

ilitakiwa Taasisi huru ya kimataifa,isiyoegemea upande wa mgodi wala serikali iteuliwe,ipewe kazi ya uchambuzi

Hawa maafisa wa serikali waliojaa kwenye kamati tena bila uwakilishi wa migodi ni ngumu kuwaamini,

Huu mchezo lazima uanze upya na utafika mbali!!

Na kuna upande utalipia gharama kubwa kama fidia!!
Mbona tume ya Nappe iliyoundwa kuchunguza "uvamizi" wa clouds media iliundwa na wana habari pia ila mliiinga mkono??
Acheni unafiki!
 
Mkuu kama wewe ni raia wa Tanzania nakushauri ukane tu huo uraia. Tuache sisi tukabiliane nao hawa wezi. Wewe umeisha ogopa law of land. Tukimaliza hili utaomba upya uraia na tutakupa lakini tutajua kuwa tayari wewe umeishakatwa mkia.
Inaonekana hufahamu kilichokuwa kinachunguzwa.

Concentrate inafahamika kuwa ni concentrate ya dhahabu, shaba na copper. Ndiyo maana inapelekwa nje kuuzwa. Ule siyo mchanga unaopelekwa kwaajili ya kujengea. Kinachotafutwa ni je concentrate ile ina mineral grade kama ilivyoripotiwa na kampuni au ni dhahabu 90% kama alivyotamka boss wa PTA. Kitu ambacho kwa ujumla yeyote mwenye akili anajua haiwezekani.
 
Mwisho wa siku muuamuzi ni mchunguzi huru hata hao watuhumiwa katika kujibu wamesha sema wao hawaja wahi kudanganya. Ila uzuri wenyewe mchanga uko na majaratasi yake yako. Tani 20 tume inesena tani 23. Kwenye uzito mchunguzu huru apime tuone nani mkweli. Nina chojua mimi mwizi ukimkamata redihendedi hakuvali ngo burden ya kuproove kuwa yeye ni mwuzi iko juu ya mkamataji, hili lazima serikali inalijua.

Na washawasha!
 
Back
Top Bottom