Ili ripoti ya mchanga wa Dhahabu iaminiwe, ingeandaliwa na Taasisi huru sio maafisa wa serikali!

Binafsi sitarajii report hii kuwa kinyume na tamko la raisi. In fact, raisi alishasema tunaibiwa na hiyo maana yake ni kwamba alishatoa hukumu (japo yeye si mahakama); na hapakuwa hata na haja ya kupoteza muda bali kuwaadhibu wezi.

Ki ukweli, ukiona report inapokelewa kwa mbwembwe mubashara ni kwa sababu imekidhi matarajio ya aliyeunda tume!
 
Kwa mwenendo huu Wa kukosoa kila hatua nzuri ya udhibiti mianya inayofanywa na Serikali, NI UTHIBITISHO TOSHA kuwa WENGI TULIKUWA TUNAJIHUSISHA na MAMBO ya "AJABU AJABU''
 
Kama Rais alisema tunaibiwa,na mgodi unasema hatuibi,unadhani ni nani wa kuiamua hiyo kesi?

Muajiriwa wa rais? Ndio maana nikasema Taasisi huru isiyo chini ya mgodi wala serikali ambayo haitwakuwa biased au hata kuonekana au kuhisiwa kwamba iko biased
Unachokifumbia macho ni kuwa si suala LA kusema tu! Ni suala LA vipimo! Vipimo hutoa namba! Na namba hazidanganyi!
Kilichofanywa na tume ni kupima mchanga, kama una dhahabu vipimo vitaonyesha! Kama hauna dhahabu vipimo vitaonesha pia! Hapo povu weka pembeni ziache namba ziongee!
 
Hizi tume zote kisheria hazina nguvu kwa sababu MDAs zote ambazo makampuni yalisaini na serikali zinatamka wazi kuwa kama kutakuwa na kutokukubaliana juu ya ukokotoaji wa mahesabu kuhusiana na kodi atatafutwa mtu wa kati aliyekubaliwa na pande zote mbili, na huyo uamuzi wake hautapingwa na upande wowote. Na hilo limewahi kufanyika kwa mgodi wa Geita.

Lakini pia MDAs kama ile ya Buzwagi inatamka wazi kuwa kama kutakuwa na jambo lolote ambalo upande wowote unahisi upande mwingine umekiuka, pande zote zitalazimika kukutana na kujadiliana ili kupata suluhu. Wakishindwa kufikia makubaliano, shauri litaamuliwa according to the Law of the Land (na kisheria hapo itamaanisha kwa sheria za Uingereza, mahali ambapo mkataba ulisainiwa).
 
Unapotoa bei ya dhahabu ili kujustify kuwa kampuni inapata pesa nyingi sana basi ni muhimu pia kuambatanisha na gharama za uzalishaji kwa kila ounce. Ni angalizo tu...
Kama hawapati faida si waondoke! Wezi wakubwa hawa hawajawahi kukiri kupata faida hata mwaka mmoja! Sasa kwa nini hawafungi migodi yao kama hawapati faida?
Nina hasira Nao acha tu!
 
Kamati iliyoundwa kuandaa taarifa kuhusu mchanga wa Dhahabu katika makontena imejaa maafisa wa serikali ambao kiapo chao kiko kwa mwajiri wao,haitarajiwi wafanye insubordination kwa kupinga hoja za mwajiri wao ambaye kuna video na maandishi yanamnukuu akiwa tayari na jibu kuhusu mchanga huo.

Kwa ushauri wangu,serikali haiwezi kuwa na kesi halafu ikaiamua yenyewe,

Yaani serikali inalalamika kuibiwa,mgodi unasema hauibi,ni nani mtu wa kati wa kuwaamua watu hawa wawili? Mtu wa kati aliye huru na asiye na hofu ya kufutwa kazi kwa atakachoandikwa na atakayekuwa na uwezo wa kukataa maelekezo kutoka popote pale na kwenye utaalam wa kutosha(sio wa kufundisha madarakani tu?) Ni wazi wajumbe wengi wa kamati ni maafisa waajiriwa katika idara mbalimbali serikalini na watarudi katika ajira zao baada ya ripoti,na mkuu wao wa ajira ndiye aliyewapa ujumbe wa kamati!!

ilitakiwa Taasisi huru ya kimataifa,isiyoegemea upande wa mgodi wala serikali iteuliwe,ipewe kazi ya uchambuzi

Hawa maafisa wa serikali waliojaa kwenye kamati tena bila uwakilishi wa migodi ni ngumu kuwaamini,

Huu mchezo lazima uanze upya na utafika mbali!!

Na kuna upande utalipia gharama kubwa kama fidia!!
I suspect ur intelligence
 
Kama hawapati faida si waondoke! Wezi wakubwa hawa hawajawahi kukiri kupata faida hata mwaka mmoja! Sasa kwa nini hawafungi migodi yao kama hawapati faida?
Nina hasira Nao acha tu!

Shanta utawaonea, wanazalisha dhahabu kwa gharama ndogo sana ukilinganisha na bei ya dhahabu.
 
Mtoa maada wewe siyo mzalendo hata kidogo!! Afu nahisi wewe mwizi fisadi mkubwa!! Ungekuw mzalendo ungetoa ushauri huu mapema mwazoni maana kama kazi hii haina credibility basi wameshakula kodi zetu !!! Kwa hiyo kaa kimya we we!! Vingenivo hovyo kabisa !!
 
Inaonekana hufahamu kilichokuwa kinachunguzwa.

Concentrate inafahamika kuwa ni concentrate ya dhahabu, shaba na copper. Ndiyo maana inapelekwa nje kuuzwa. Ule siyo mchanga unaopelekwa kwaajili ya kujengea. Kinachotafutwa ni je concentrate ile ina mineral grade kama ilivyoripotiwa na kampuni au ni dhahabu 90% kama alivyotamka boss wa PTA. Kitu ambacho kwa ujumla yeyote mwenye akili anajua haiwezekani.

Unachokifumbia macho ni kuwa si suala LA kusema tu! Ni suala LA vipimo! Vipimo hutoa namba! Na namba hazidanganyi!
Kilichofanywa na tume ni kupima mchanga, kama una dhahabu vipimo vitaonyesha! Kama hauna dhahabu vipimo vitaonesha pia! Hapo povu weka pembeni ziache namba ziongee!
 
Hii ni hatua nzuri na serikali inastahili pongezi kwa hilo.
Hata hivyo, ni muhimu kuchukua tahadhari, wasomi wengi ni wazuri wa kuandika nadharia, kuyaweka waliyoandika kwenye vitendo vyenye ufanisi ni changamoto.
 
Inaonekana hufahamu kilichokuwa kinachunguzwa.

Concentrate inafahamika kuwa ni concentrate ya dhahabu, shaba na copper. Ndiyo maana inapelekwa nje kuuzwa. Ule siyo mchanga unaopelekwa kwaajili ya kujengea. Kinachotafutwa ni je concentrate ile ina mineral grade kama ilivyoripotiwa na kampuni au ni dhahabu 90% kama alivyotamka boss wa PTA. Kitu ambacho kwa ujumla yeyote mwenye akili anajua haiwezekani.
Si ndiyo ninasema namba zitaonesha! Mbona una wasi wasi?
 
umenena!! hii shughuli ingekuwa na mtu asiye na maslahi. ukizingatia mzee alishasema sio lazika kila mara serikali ishindwe. mwenye macho na masikio atajua jamaa anataka nini katika hili
 
umenena!! hii shughuli ingekuwa na mtu asiye na maslahi. ukizingatia mzee alishasema sio lazika kila mara serikali ishindwe. mwenye macho na masikio atajua jamaa anataka nini katika hili
 
Katika hili LAZIMA NISEME,Hakuna kampuni ya Madini hata moja inayopata hasara kuchimba madini Tanzania wanapata faida ya kufa mtu Ndugu zangu pitieni Taarifa za kampuni moja tu ya SHANTA GOLD katika Mgodi wa LUIKA halafu sikilizeni Taarifa zao wanakotoa pesa ndio hasira ziwapande zaidi,halafu tujiulize Tanzania ina migodi mingapi?hawa jamaa wameweza kuzalisha Ounce 500,000 kwa mwaka 2016 na kwa bei ya sasa ni $1259.57 kwa Ounce ambapo ni sawa na $Mil 629,785,000 kwa TZS 1.385,527,000,000 ikumbukwe 1 Ounce = 28.3495231 Grams ambapo ni Gram 14,175,000 au Kilo 14,175 ambazo ni Tani 14.18 hivi

Wewe ni muongo kupindukia nenda kwenye soko la dunia angalia bei ya dhahabu kwa soko la dunia na sio kukaa humu kutunga ujinga.
 
Si ndiyo ninasema namba zitaonesha! Mbona una wasi wasi?
Wasiwasi wa nini? Nilikuwa nasahihisha ulipopotosha kuonesha kama vile mchanga ule kuwa na dhahabu ni kosa wakati unatakiwa kuwa na dhahabu.

Na pia nikatoa comment kwa kauli ya boss wa PTA kuwa mchanga ule 90% ulikuwa dhahabu. Unahitaji uwe mjinga hasa usiyejua hata elementary chemistry na physics kuamini kwa specific gravity ya gold ijae container zima halafu ibebwe na lorry na ipite kwenye barabara zetu hizi na madaraja bila ya hayo madaraja, container lenyewe kupasuka au kuvunjika. Inahitaji ujinga wa hali ya juu kulikubali hilo.

Ni sawa ukasikia kuwa kuna mtu amemwona mwizi amebeba kilo 10,000 za maharage kwenye mfuko wa plastic (rambo), alikuwa amejitwisha kichwani, akaingia na mzigo ndani ya basi.
 
Kwani hiyo dhahabu ni ya kimataifa? Dhahabu ni mali yetu, sisi tunakagua/ kuchunguza mali yetu. Tukigungua wanatuibia tunawatimua. Full stop. Tunaweza hata kuwalaza lock up kwa kosa la wizi na sheria inachukua mkondo wake. Mwizi popote hana immunity in front of the law.
Bongoland kila mtu ana majibu yachangamoto zetu
 
Back
Top Bottom