Ikulu ya Magogoni iko hatarini kutumbukia baharini

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,885
6,885
06_11_v883um.jpg

Aibu hii ambayo ni kielelezo kisichofichika Ikulu ya Dar es Salaam langu kuu la kutokea baharini bada ya kuvuka barabara (ocean road) unakumbana na mmommonyoko huu. Hata kutunza mazingiara yanayozunguka Ikulu yanatushinda, ila tu kuhangaikia mambo binafsi tu.​
 
Barabara ya Ocean Road iko hatarini kuporomoka, na mmommonyoko huu kitokee kimbunga kama cha Japan Ikulu itasombwa na gharika ya Indian Ocean.

Tangu Mzee Ruksa afanye ukarabari wa majengo, hakuna anayefikiria kushughulikia madhari na mazingira yanayoizunguka, labda bajeti huwa finyu?​
 
Hivi wale wahusika wa mazingira kazi yao ni nini?? Tena kuna waziri wa mazingira.....

kazi yao, kuishambulia chadema, kuhudhuria mikutano ya bunge ili kuipigania ccm isimezwe na chadema, kuwa wageni rasmi kwenye minuso na mishiko, kufungua semina , makongamano na kuboresha mazingira ya utoaji tiba ya babu loliondo. kama kuna kazi nyingine nimesahau mnikumbushe.

its too narrow indeed!!
 
bora ikulu ikumbwe na gharika kama la noah ili waamie dodoma.watu miaka zaidi ya 20hawataki kuenda mji mkuu.lazima toko kwenye rekodi ya dunia ktk kukaa muda mrefu bila kuamia mji mkuu.
 
bora ikulu ikumbwe na gharika kama la noah ili waamie dodoma.watu miaka zaidi ya 20hawataki kuenda mji mkuu.lazima toko kwenye rekodi ya dunia ktk kukaa muda mrefu bila kuamia mji mkuu.

hiyo itakuwandoto za alinacha kuhamia DOM, ikisambaratishwa watahamia bagamoyo
 
Mie nikajua ni lile gofu lililo pale kwa waziri mkuu ambalo linatia aibu sana ndani ya ikulu... sijui linafugia majini??
 
sasa kama hapo ndio karibu kabisa na ikulu wanashindwa hata kuzuia mmomonyoko kama huo sasa hizo harakati za utunzaji wa mazingira ujue ni ulaji tu wa mihela yetu ya kodi na hii inaonesha mwenye nyumba haijui vizuri nyumba hake kwakuwa kutwa yupo busy na safari.:typing:
 
Kila ninapokatiza maeneo yale huwa najitahidi kutoangalia pembeni kwani mazingira yanayoizunguka IKULU yetu ni aibu tupu na hayaridhishi kwa hadhi yake. Kuna miti imekatwa upande wa kutokea baharini na mpaka sasa hakuna replacement yake. Mmomnyoko utaiathiri Ikulu endapo hatua za dharura hazitachukuliwa.
Najiuliza nini kiinachosababisha kasi ya ujenzi wa maghorofa kwenye maeneo yanayoizunguka IKULU??

Kuna madudu mengi yanayohitaji ufumbuzi lakini wahusika wanajifanya hawahusiki
 
Wacha itumbukie wanafaida gani hawa zaid ya kula kiyoyozi na kodi zetu? Waje wakae uswaz waone shurba za mgao wa umeme kudadaaadeki!
 
kazi yao, kuishambulia chadema, kuhudhuria mikutano ya bunge ili kuipigania ccm isimezwe na chadema, kuwa wageni rasmi kwenye minuso na mishiko, kufungua semina , makongamano na kuboresha mazingira ya utoaji tiba ya babu loliondo. Kama kuna kazi nyingine nimesahau mnikumbushe.

Its too narrow indeed!!

hivi jamani kwanza naomba samahani sisi wengine hatuna vyama na wala hatutalajii kujiunga na vyama, hivi hakuna hata siku moja ishu za kijamii tukazijadili bila kuweka mambo ya vyama vya cdm ccm, wengine twasikia vibaya na hatupendi kuona kilka suala mwawek mambo ya vyama, kwani hata kama cdmwangepata nafasi hiyo wangeweza kutekeleza hayo ambayo ccm imeshindwa au inayafanyia mzaha? Tuondoe mambo ya cdm na ccm tuchangia hoja bila kuwataja hao, mbona sijasikia cuf na wengine wakitajwa?
 
Mmomonyoko huu kwa kweli unaonekana kutowasumbua wanaikulu, nadhani kuna dhana nzima ya kupuuza miongoni mwa wanaohusika na kwa jina la kawaida ninawaita wapuuzi, na pia ukiwa ndani ya pantoni unatoka mjini kuja kigamboni, sehemu ya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere nayo inaelekea kubaya kwani nako mmomonyoko unaonekana dhahiri.
tafadhari wahusika waache upuuzi wa masuala ya msingi
 
hiyo itakuwandoto za alinacha kuhamia DOM, ikisambaratishwa watahamia bagamoyo

Hawajali kuilinda hiyo ya magogoni kwani wameishahamia Msoga; kila ijumaa tunasimamishwa foleni masaa mengi tu Mkwelele anapokwenda nyumbani kwao!!
 
Ikibomoka/kukumbwa na mafuriko itasaidia kuondoa WAKAAZI WA MJENGO HUO wasitusaidia kwenye jitihada zetu za maendeleo
 
hivi jamani kwanza naomba samahani sisi wengine hatuna vyama na wala hatutalajii kujiunga na vyama, hivi hakuna hata siku moja ishu za kijamii tukazijadili bila kuweka mambo ya vyama vya cdm ccm, wengine twasikia vibaya na hatupendi kuona kilka suala mwawek mambo ya vyama, kwani hata kama cdmwangepata nafasi hiyo wangeweza kutekeleza hayo ambayo ccm imeshindwa au inayafanyia mzaha? Tuondoe mambo ya cdm na ccm tuchangia hoja bila kuwataja hao, mbona sijasikia cuf na wengine wakitajwa?

huwezi kuzungumzia maisha yako ya kila siku bila kuhusisha siasa,nikwa njia ya siasa serikali moja inapatikana,hamsha akili zako mkuu,na siasa ya leo bila CCM na CDM bado hujaongelea siasa watu wakakusikiliza kwa umakini.
 
hivi jamani kwanza naomba samahani sisi wengine hatuna vyama na wala hatutalajii kujiunga na vyama, hivi hakuna hata siku moja ishu za kijamii tukazijadili bila kuweka mambo ya vyama vya cdm ccm, wengine twasikia vibaya na hatupendi kuona kilka suala mwawek mambo ya vyama, kwani hata kama cdmwangepata nafasi hiyo wangeweza kutekeleza hayo ambayo ccm imeshindwa au inayafanyia mzaha? Tuondoe mambo ya cdm na ccm tuchangia hoja bila kuwataja hao, mbona sijasikia cuf na wengine wakitajwa?
Ni kwa sababu mambo mengi ya kijamii yanatawaliwa na wanasiasa, na huwezi kuongelea wanasiasa bila kugusa vyama vya siasa!
 
Viongozi wetu wapo na itikadi za kufikiria zaidi lini ataondoka madarakani na kiasi gani, suala la uboreshaji wa mazingira yanayozunguka Ikulu kwa sasa hawayaoni ila kujenga majengo binafsi watakayoishi baada ya kustaafu.
 
Ikibomoka/kukumbwa na mafuriko itasaidia kuondoa WAKAAZI WA MJENGO HUO wasitusaidia kwenye jitihada zetu za maendeleo

Kila siku utaona wanausalama wanalandalanda maeneo hayo tena kwa kutembea kwa miguu, nashangaa hawaoni mmommonyoko huo na kutahadharisha wahusika?
Waziri wa Mazingira ameshindwa tu kuona tatizo linaloelekea kuikumba ikulu, je atafanya nini kwa maeneo mengine?
 
Back
Top Bottom