Ikulu sio mahali kukimbili na si pango la walanguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu sio mahali kukimbili na si pango la walanguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nguluvisonzo, Mar 1, 2011.

 1. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimeamini maneno Hayati Mwl.Nyerere kama kichwa cha habari kinavyosema,pia wana jf hii ndio habari yangu ya leo.
  Nimemsikiliza Raisi hotuba yake,kwenye suala la siasa na usalama wa nchi natofautiana naye kwa asilimia mia moja,kwanza kabisa nadiriki kusema anajaribu kutisha wananchi waogope kuwa wawakilishi wao ati wanataka kuindoa serikali halali madarakani kitu hiki sijawahi kukisikia naona anaogopa kivuli chake,je suala la udini halipo tena?au ameona hiyo propaganda imefeli?na anakuja na mpya?
  Siku zote serikali yenye matatizo huwa inaweweseka sana,maana hatma yake mbele ya safari haipo,na siku zote serikali inapoamua kwa makusudi kufinyanga haki za wananchi wake haiko salama hata kidogo,maana IKULU imegeuka mahakama,ukumbi wa disco kwa wachache waliodhamilia kuhujumu mali na rasilimali ya nchi yetu na ulanguzi.Ikulu haijali shida za watanzania wengi ambao ni masikini.Mikataba mibovu,bei za bidhaa muhimu kwa maisha ya binadamu kupanda hovyo hovyo,lakini Ikulu inaona ni sawa tu.Je ni kwanini JK anailaumu chadema kwa kufanya maandamano nchi nzima wakieneza chuki dhidi ya serikali yake.Hali halisi ya serikali;serikali hii inamatatizo makubwa sana hasa ya kuwanyonya watanzania kwa kufanyakazi yenye ubinafsi,yaani kuwaneemesha wachache na gharama kuwabebesha masikini Ikulu ikiwa kimya na tena kutowatambua wamiliki wa hizo biashara je ni serikali gani duniani isiyotambua wabia wake wa biashara.
  Kwa mtazamo wangu,kwanini CHADEMA inakwenda moja kwa moja kwa wananchi kwa kundaa maandamano na mikutano kuwaeleza moja kwa moja maovu ya Serikali,sababu iko moja kubwa,ni kufinyangwa kwa haki na sheria za nchi kuwanyima wawakilishi wa wananchi kuwashilisha matatizo yanayowakabili sehemu husika,asisahau vitendo vya spika Anne Makinda katika nguvu zake kuzuia hoja muhimu ambazo kama angeruhusu wasingekuwa na uwezo au nguvu za kuzizungumzia katika majukwaa.
  Ukiruhusu Ikulu ikatumike kama pango la walanguzi ujue unaharibu maisha ya serikali, ni ajabu kwa kiongozi kulalamikia chama cha upinzani eti kinataka kupindua serikali yake,lakini anasahau jinsi serikali yake ilivyoshindwa kazi.kinachotakiwa aweke urafiki kando na kutoa adhabu stahiki kwa wakosefu na kuhakikisha serikali inasimamia vizuri raslimali za nchi kwa manufaa ya watanzania na si vinginevyo,Chama chochote makini huindoa serikali legelege madarakani kwa hoja ambazo zinasababishwa na hiyo serikali,hivyo JK usilalamike imalisha serikali yako kuwa mkali uone matokeo la sivyo 2015 ni karibu wenzako wameanza kujenga msingi/mtaji wa 2015.
   
Loading...