Julius K. Nyerere: Ikulu ni pahali patakatifu, sio pango la wanyang'anyi

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,395
4,056
"Mimi sikuchaguliwa na watanzania ili niifanye Ikulu kuwa Pango la wanyanganyi"



Pili naomba tujadili hali ya ikulu yetu, je ni pango la wanyanganyi au ni mahali patakatifu?
 
Na mimi nimeisikia leo ITV na imenikumbusha mbali na imenikumbusha mengi maana nilijikuta nikitokwa machozi nilipotafakali na kugundua kuwa sasa ikulu yetu imeshageuzwa ni Pango la wanyang'anyi.
Nyerere alikuwa ni nabii wa nyakati zetu!:(
 
nimeisikia hio hotuba kiboko.naona kuna viongozi lazima walihamisha channel loool.manake unaweza ukajistukia hivi hivi kwamba unalengwa lol.
 
Ukisikiliza hotuba za Mwalimu, unaweza sema huyu jamaa alikua nabii, manake yote aliyokua anaonya ndiyo yanatokea sasa.

Ikulu imekua pango la majambazi,

Mwalimu alisema kiongozi sio tu awe mwadilifu bali awe na uwezo wa kuwaambia marafiki zake, ndugu na jamaa kuwa ikulu ni mahali patakatifu. JK anaweza hilo?
 
Kusoma ni rahisi sana lakini vitendo ni vigumu sana. Nilisikiliza nakatamani Mwenyezi Mungu amrudishe Mwl. Nyerere japo nusu dk wakati alipokuwa anasoma ile hotuba alafu amnase vibao viwili tu then arudii akapumzike.
 
Wakati JK anasoma ile hotuba yake ndipo hapo nilitamani Mwl. arudishwe kwa nusu dk tu
 
kwa kweli mwalimu alikuwa kama anafunuliwa vile na Mungu.Kama ingekuwa watu wanarudi kwa kweli angelia machozi kwa yanayotokea sahizi.Ni kama walikuwa wanambeza alipokuwa anatoa ile hotuba na walikuwa wanaona anawapotezea wakati.
 
Na mimi nimeisikia leo ITV na imenikumbusha mbali na imenikumbusha mengi maana nilijikuta nikitokwa machozi nilipotafakali na kugundua kuwa sasa ikulu yetu imeshageuzwa ni Pango la wanyang'anyi.
Nyerere alikuwa ni nabii wa nyakati zetu!:(

Mkuu Mchukia fisadi,

Unajua unaposikiliza hotuba za Mwl Nyerere unaweza kudhani alikuwa akijua kuna siku Tanzania itakuja kuangukia kwenye mikono ya wanyang'anyi.Unaweza kushangaa viongozi wa wakati wake kama Ben Mkapa,Kingunge N Mwiru,Basil P Mramba na wengineo kibao walijifunza nini na wakaja kufanya nini.

Utashangaa zaidi hawa viongozi jinsi walivyo na ujasiri wa kuudhuria na kutoa matamko mbali mbali kuhusiana na uadilifu wa Mwl Nyerere.

Mwl Nyerere bora ameshatangulia mbele ya haki kwasababu angeyaona mambo yanayofanywa na hawa viongozi aliotuachia tena wengine alishiriki kuwapigia debe kwamba ni wasafi sijui angekuwaje au angewaambia nini watanzania.
 
Nyerere played a part in creating the current circumstances. Hivyo ilikuwa rahisi kwake kutabiri haya...
 
hao mafisadi hotuba walikuwa wanaisikiliza vizuri tu
si haba walikuwa wakishushia na nyama choma kwa kinywaji ...
kuna watu hawana haya hapa duniani loh
 
Nyerere played a part in creating the current circumstances. Hivyo ilikuwa rahisi kwake kutabiri haya...

There is some element of truth in this. Lakini naona kuwa kuna watu walikuwa wakiomba sana Nyerere afe, walikuwa wanamuona kikwazo cha wanayotaka kufanya.

Kunawengine walikuwa wezi hata wakati wa nyerere, lakini alikuwa anawakalia kimya tu. Si kama hakujua kama Kingunge ni mnafiki, na si kweli kama hakujua EL ni fisadi au huyu na yule ni watu ovyo. Hakuwa na uwezo kama malaika kudean na wote.
 
Nyerere played a part in creating the current circumstances. Hivyo ilikuwa rahisi kwake kutabiri haya...
Hotuba ile kwa Waandishi ilikuwa ni miaka 10 baada ya kuwa ameondoka madarakani. Aliamini kabisa kuwa Rais ambaye angechaguliwa baada ya Mzee Ruksa angeziona zile nyufa. Akaja Mkapa. Haikuwa. Amekuja JK, mambo yanaelekea kumwelemea zaidi kwa kuwa alichokitaka yeye ni Urais.
 
There is some element of truth in this. Lakini naona kuwa kuna watu walikuwa wakiomba sana Nyerere afe, walikuwa wanamuona kikwazo cha wanayotaka kufanya.

Kunawengine walikuwa wezi hata wakati wa nyerere, lakini alikuwa anawakalia kimya tu. Si kama hakujua kama Kingunge ni mnafiki, na si kweli kama hakujua EL ni fisadi au huyu na yule ni watu ovyo. Hakuwa na uwezo kama malaika kudean na wote.

Lakini ndo ame-create system iliyopo sasa. Angejitoa muhanga kama ni mzalendo kweli na kuua system nzima. System yetu kwa sasa tunatawaliwa na Chama badala ya Serikali. Hivyo serikali inakuwa inalinda chama badala ya wananchi. Kama kweli alikuwa na moyo wa uzalendo na kuyaona hayo yote...angeruhusu vyama vingi wakati ule ule alipokuwa anatoka madarakani. Na angepunguza nguvu ya chama chake. Sasa ujinga aliofanya yeye ndo tumebaki ku-deal nao sisi. CCM imekuwa mwiba wa maendeleo badala ya chama kinacholeta maendeleo. CCM imebaki jina tu ndani ni MUOZO. Na kama aliona haya si nafuu angekarabati muda wote. I like him, but huyu mzee ametufikisha hapa mwenyewe. Sasa we have to clean up his mess!
 
Hotuba ile kwa Waandishi ilikuwa ni miaka 10 baada ya kuwa ameondoka madarakani. Aliamini kabisa kuwa Rais ambaye angechaguliwa baada ya Mzee Ruksa angeziona zile nyufa. Akaja Mkapa. Haikuwa. Amekuja JK, mambo yanaelekea kumwelemea zaidi kwa kuwa alichokitaka yeye ni Urais.

Serikali ya Mkapa si ndo imecheza rafu kubwa kupita zote. Mikataba yote mibovu inayotuumiza sasa si ilikuwa signed wakati wake? Ndo wanyang'anyi hasa walipotinga Ikulu...hahaha
 
Urais ni kazi ya watu, kazi yoyote ya kuhudumia watu ni kazi ya kumtumikia Mungu!

Hii ni kazi tukufu na Ikulu ni mahali patukufu hapataki kuwa sehemu ya mzaha, uongo, ulaghai na unyang'anyi ambao tunauona leo ukisimamiwa na watawala wetu tuliowaamini na kuwapa idhini wakae Ikulu.
Kama Ikulu ingelisema wale wote waliohusika na wizi wa EPA, Deep Green Finance, Mwananchi Gold, IPTL, RITES, n.k wawajibishwe kwa mjibu wa SHERIA bila woga wala upendeleo na kwa dhati, idara husika zingelihakikisha wahusika wa Kagoda wanashughulikiwa, wahusika wote waliolitumia jeshi letu tukufu kwa manufaa yao ya kifedhuri wangewajibishwa na wala hakuna mwanajeshi ambaye angelileta fujo kupinga kwa sababu hili ni jeshi la wananchi kwa ajili ya wananchi. Wale wote waliohusika na mikataba mibovu ilitufikisha hapa tulipo wangelikuwa viranja katika magereza yetu na si kwenye majukwaa ya kuomba kuwatumikia watu..... wengine wakiwawekea watanzania safi vipingamizi ili wasiweze kupambana na hasira za wananchi katika masanduku ya kura... hawa wote wangelikuwa wanawajibika kadri ya matendo yao na Tanzania yetu ingelikuwa na matumaini makubwa na amani kama waasisi wa taifa hili walivyotaka Tanzania iwe.

Wale wote ambao wanatufanyia mzaha katika zoezi muhimu la uchaguzi wasingefanya vile wanavyofanya, wasingelithubutu!

Tunataka mtu atakayeomba kwenda Ikulu afanye hivyo kwa manufaa yetu sote na si kulinda maslahi ya wachache, vinginevyo malaika wa watanzania maskini wanaopoteza maisha kwa kukosa huduma za msingi (kwa sababu haki yao imetwaliwa na hao wachache wanaolindwa na watawala wetu) itawaandama na kuwafanya waweweseke na kuaibika mbele ya dunia.

Mungu Ibariki Tanzania na Nguvu zako kuu zishuke kwa wale wote wanaoifanyia mzaha kazi yako
 
Hivi inakuwaje hawa wagombea wa nafasi mbalimbali wakiongozwa na huyu jamaa mwenye kauli zinazoishia na neno "zaidi " wanapojigamba wamefanya hiki na kile, mimi najiuliza inamaana wao waliteuliwa kwenda kuuza sura?

Kwani mtu unapoajiriwa lengo la mwajiri wako si ili wewe ufanyekazi na mwisho wa siku aione na ajuwe anakulipa mshahara kwa kazi hiyo! sasa haya majigambo ya ndugu zetu waliopewa mamlaka na umma kuanza kusema wamejenga kisima, madaraja, shule, vyuo, n.k wanamaanisha nini?

Kwani wao wakati wanaomba uongozi walifikiri wanaenda kuuza nyuso zao na mwisho wa siku walipwe, acheni ujinga bwana kuutumikia umma ni kwa mujibu wa ajira zenu sasa mnapotuambia mmejenga hiki na kile kana kwamba ni msaada wakati hizi ni hela zetu mimi inanikera sana, mwisho mtakuja kutuambia hata mambo ya nguoni mwenu kwamba mmefanya hivi, sipendi kabisa kauli hizi mfu,
 
Sihitaji kwenda kula mayai Ikulu asema Slaa

Monday, 20 September 2010
Boniface Meena, Hai


MGOMBEA wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk Willbroad Slaa, amesema haitaji kura za wananchi zimpeleke Ikulu, ili kwenda kula mayai na kwamba anazihitaji ili akawatumikie.

Dk Slaa ambaye jana alifanya mikutano ya kampeni 12 katika jimbo la Hai, kukiwa na shamrashamra za pikipiki zaidi ya 30 na magari zaidi ya 20 katika msafara wake, alisema CCM wanahitaji kuingia Ikulu ili wakafanye anasa, kama anazozifanya Rais Jakaya Kikwete na uongozi wake.


Alisema hata hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa 'Ikulu si mahali pa mchezo' na kwamba msingi huo yeye hahitaji kwenda kufanya mchezo kama wanaoucheza CCM.


Mgombea huyo alisema badala yake, yeye anakwenda kuwatumikia wananchi maskini.


"Ndugu zangu sasa hivi hatuwabipu CCM bali tunapiga kweli na lazima wapokee kwa kuwa tunahitaji kuingia ikulu kulikomboa taifa hili lililopo mikononi mwa mafisadi,"alisema Dk Slaa.


Alisema Rais Kikwete amegeuza taasisi ya urais kuwa ya kisanii kitu ambacho ni hatari kwa taifa la watu kama Tanzania.


"Chadema tutakufa au kupona ili kulikomboa taifa letu linaloangamia na nyie wananchi ndiyo nguvu yetu ya kutuingiza ikulu kufanikisha mpango wetu,"alisema.


Akizungumzia suala la elimu katika jimbo hilo, Dk Slaa alisema takwimu zilizotolewa bungeni na serikali zinaonyesha kuwa jimbo lina walimu katika shule za sekondari 15 tu, jambo ambalo alisema ni la aibu.


Alisema hata barabara zake zinatia aibu wakati serikali imetenga kiasi cha Sh1 bilioni, kwa ajili ya barabara, Sh13 bilioni kama ruzuku ya uendeshaji na Sh26 bilioni, kwa ajili ya maendeleo.


"Hizi fedha zimekwenda wapi. Mbona barabara hazionekani, miradi ya maendeleo haionekani. Yani fedha zote hizi hakuna kinachoonekana, naombeni mnipe mbunge wa Chadema na madiwani wake tuchukue halmashauri ili tulete maendeleo,"alisema.


Kwa upande wake, mgombea wa kiti cha ubunge wa jimbo hilo kupitia tiketi ya Chadema, Freeman Mbowe, alisema mwaka huu si mwaka wa utani bali wa mapambano ya kuingia ikulu.


"Kikwete aanze kukusanya kandambili na vitu vingine na CCM wasifikiri hivi sasa tunatania ni mapambano ya kufa au kupona kama alivyo sema Dk Slaa mpaka tuingie ikulu,"alisema.


"Safari hii tutalinda kura ipasavyo na polisi wasiingilie na watuache tucheze ngoma hii sisi na CCM, polisi siwaogopi, wala siwaogopi usalama wa taifa bali nawaheshimu suala la siasa tuachieni,"alisema Mbowe


SOURCE; Sihitaji kwenda kula mayai Ikulu asema Slaa
 
Kikwete hataki kabisa kusikiliza kanda za namna hii. Ndivyo aliniambia.................anasema alipelekwa na hao walanguzi sasa nyie mnawafanyia roho mbaya tu............... tena anakachukia hako kababa kalikotoa matamshi hayo............ shauri zenu nyie mchokozeni tu!
 
Nice speech, huyu mzee alikuwa na hekima sana, sijui ni kwanini aliiacha nchi ifikie hali hii iliyonayo hivi sasa. Huwa naamini matatizo mengi na umaskini mkubwa unaoikabili hii nchi ulisababishwa na yeye kwa kushindwa kuweka vipaumbele makini wakati wa uongozi wake.
 
Back
Top Bottom